Enjoying your free trial? Only 9 days left! Upgrade Now
Brand-New
Dashboard lnterface
ln the Making
We are proud to announce that we are developing a fresh new dashboard interface to improve user experience.
We invite you to preview our new dashboard and have a try. Some features will become unavailable, but they will be added in the future.
Don't hesitate to try it out as it's easy to switch back to the interface you're used to.
No, try later
Go to new dashboard
Published on Dec 17,2021
Like
Share
Download
Create a Flipbook Now
Read more
Published on Dec 17,2021
Kiswahili
Darasa la Saba
Kitabu cha Mwanafunzi
Read More
Home Explore Kiswahili. Darasa la Saba
Publications:
Followers:
Follow
Publications
Read Text Version
More from TIE ADMIN
P:01



P:02

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Kiswahili Kitabu cha Mwanafunzi Darasa la Saba FOR ONLINE USE ONLY Taasisi ya Elimu Tanzania i KISWAHILI_STD VII.indd 1 7/23/21 3:28 PM

P:03

FOR ONLINE USE ONLY © Taasisi ya Elimu TanzanDiaO, 2N02O0 T DUPLICATE Toleo la Kwanza 2020 Chapa ya Pili 2021 FOR ONLINEISBN: 978-9987-09-154-6 USE ONLY Taasisi ya Elimu Tanzania S.L.P. 35094 Dar es Salaam - Tanzania Simu: +255 735 041 170 /+255 735 041 168 Baruapepe: [email protected] Tovuti: www.tie.go.tz Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili, kurudufu, kuchapisha, kutafsiri wala kukitoa kitabu hiki kwa namna yoyote ile bila idhini ya maandishi kutoka Taasisi ya ElimuTanzania. ii KISWAHILI_STD VII.indd 2 7/23/21 3:28 PM

P:04

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY DO NOT DUPLICATE Yaliyomo Ukurasa Shukurani ���������������������������������������������������������������������������������������������� v Utangulizi ��������������������������������������������������������������������������������������������� vi Sura ya Kwanza Mashairi �������������������������������������������������������������������������������������������������� 1 Sura ya Pili Utenzi ��������������������������������������������������������������������������������������������������� 14 Sura ya Tatu Ngonjera ����������������������������������������������������������������������������������������������� 20 Sura ya Nne Vitendawili �������������������������������������������������������������������������������������������� 27 Sura ya Tano Tutumie methali zetu ���������������������������������������������������������������������������� 35 Sura ya Sita Matumizi ya nahau ������������������������������������������������������������������������������� 45 Sura ya Saba Aina za maneno ����������������������������������������������������������������������������������� 53 Sura ya Nane Hadithi �������������������������������������������������������������������������������������������������� 63 Sura ya Tisa Risala ��������������������������������������������������������������������������������������������������� 71 Sura ya Kumi Kusoma magazeti ��������������������������������������������������������������������������������� 83 Sura ya Kumi na Moja Barua ya kirafiki na rasmi ��������������������������������������������������������������������� 91 iii KISWAHILI_STD VII.indd 3 7/23/21 3:28 PM

P:05

FOR ONLINE USE ONLY Sura ya Kumi na Mbili DO NOT DUPLICATE Kadi za mialiko ����������������������������������������������������������������������������������� 101 Sura ya Kumi na Tatu Insha ��������������������������������������������������������������������������������������������������� 108 Sura ya Kumi na Nne Hotuba ������������������������������������������������������������������������������������������������ 116 Sura ya Kumi na Tano Ufupisho ��������������������������������������������������������������������������������������������� 123 Sura ya Kumi na Sita Uwasilishaji wa hoja ��������������������������������������������������������������������������� 131 FOR ONLINE USE ONLY iv KISWAHILI_STD VII.indd 4 7/23/21 3:28 PM

P:06

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Shukurani Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inatambua na kuthamini mchango muhimu wa washiriki waliofanikisha uandishi wa kitabu hiki cha mwanafunzi. TET inatoa shukurani za dhati kwa mchango uliotolewa na wataalamu wafuatao: Waandishi: Mwl. Rose S. Chipindula, Mwl. Melina A. Yohana, Mwl. Samwel M. Magutu, Mwl. Tumaini M. Mahendeka, Mwl. Adelgot J. B. Mapunda, Mwl. Aurelia F. Mutajunwa, Mwl. Jivitius C. Sabatho na Mwl. Monica W. Manyanga FOR ONLINE USE ONLYWahariri: Prof. David P. B. Massamba, Prof. Kulikoyela K. Kahigi, Dkt. Rehema O. Stephano, Dkt. Adventina A. Buberwa, Mwl. Titus Mpemba, Mwl. Saul S. Bichwa (Maudhui) na Bw. Mussa R. Kaoneka (Lugha - BAKITA) Msanifu: Bw. Silvanus A. Mihambo Wachoraji: Bw. Fikiri A. Msimbe na Alama Art and Media Production Limited Mratibu: Mwl. Rose S. Chipindula Pia, TET inatoa shukurani kwa walimu wote walioshiriki katika ujaribishaji wa kitabu hiki cha mwanafunzi. Vilevile, TET inatoa shukurani za pekee kwa shirika la “Global Partnership for Education (GPE)” kupitia mradi wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) uitwao “Literacy and Numeracy Education Support (LANES II)” kwa ufadhili wao uliofanikisha kazi ya uandishi na uchapaji wa kitabu hiki. Aidha, TET inatoa shukurani za pekee kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kusimamia kwa karibu zoezi zima la uandishi na uchapaji wa kitabu hiki. Dkt. Aneth A. Komba Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Elimu Tanzania v KISWAHILI_STD VII.indd 5 7/23/21 3:28 PM

P:07

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Utangulizi Kitabu hiki ni cha tano katika mfululizo wa vitabu vitano vya somo la Kiswahili kuanzia Darasa la Tatu hadi la Saba, kilichoandaliwa mahususi kwako mwanafunzi wa Darasa la Saba. Kitabu hiki kimeandaliwa kulingana na muhtasari wa somo la Kiswahili wa mwaka 2019 uliotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kitabu kinalenga kukuza uwezo wako wa kuzungumza, kusikiliza, kusoma na kuandika kwa lugha ya Kiswahili. Pia, kitabu kimelenga kukuwezesha kutumia msamiati wa lugha ya Kiswahili kwa namna mbalimbali, na hivyo, kukujengea uwezo wa kupanga mawazo kwa mpangilio na mtiririko unaotakiwa. Kitabu kina hadithi, habari, mashairi, ngonjera na majigambo. Vyote hivyo vitakuwezesha kujifunza kwa ufanisi. Kitabu kimesheheni maswali ya kupima ufahamu wako na mazoezi mbalimbali yanayojenga ujuzi wako katika somo la Kiswahili. Hivyo basi, unapaswa kufanya kazi zote zilizomo kwenye kitabu hiki pamoja na kazi zingine utakazopewa na mwalimu. FOR ONLINE USE ONLY vi KISWAHILI_STD VII.indd 6 7/23/21 3:28 PM

P:08

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY DO NOT DUPLICATE Sura ya Kwanza Mashairi Utangulizi Ulipokuwa Darasa la Sita, ulijifunza kughani mashairi na kubaini mawazo makuu. Pia, ulijifunza kutunga shairi la kimapokeo kwa kuzingatia kanuni zake na kufafanua maana za taswira zilizomo katika shairi na kuzihusisha na maisha ya kila siku. Katika sura hii, utajifunza zaidi sifa za mashairi ya kimapokeo na mashairi ya kisasa. Utachambua maudhui yaliyomo katika mashairi ya kimapokeo na ya kisasa. Vilevile, utatunga mashairi ya kimapokeo na ya kisasa. Maarifa utakayoyapata katika sura hii, yatakusaidia kuwa mtunzi mahiri wa mashairi. Fikiri Mambo ya kuzingatia katika utunzi wa mashairi Ufahamu Soma shairi hili, kisha jibu maswali yanayofuata. 1. Kiswahili naazimu, sifayo inayokabwa, Kwa wasiokufahamu, niimbe ilivyo kubwa, Toka kama chemchemu, furika palipozibwa, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 2. Toka kama mlizamu, juu kwa wingi furika, Uoneshe umuhimu, kwa wasiokutamka, Ndipo waingiwe hamu, mapajani kukuweka, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 1 KISWAHILI_STD VII.indd 1 7/23/21 3:28 PM

P:09

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY3. Lugha yangu ya utotoD, OhaNdiOleTo nDimUePkuLaIC, ATE Tangu ulimi mzito, sasa kusema najua, 7/23/21 3:28 PM Pori, bahari na mto, napita nikitumia, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 4. Sababu ya kuipenda, lugha yangu ninatoa, Natumia toka ganda, na kiini chanelea, Lugha nyingine nakonda, wakati nikitumia, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 5. Lugha kama Kiarabu, Kirumi na Kingereza, Kweli mi’ nimejaribu, kila hali kuigiza, Lakini sawa na bubu, nisemapo wanibeza, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 6. Kila mtu lugha yake, ndiye mtumishi mwema, Kila mkuu na pake, hana hadhi akihama, Kiswahili univike, joho lako la heshima, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 7. Lugha ngeni ni elimu, hili sana naelewa, Tena sitishwi ugumu, kujifunza ninajuwa, Lakini huwa mtamu, ulimi wa kulelewa, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 8. Mtu kwa usemi wake, wanyama milio yao, Simba kwa ngurumo yake, ni tisho kwa kondoo, Bali kwa makinda yake, hupendeza masikio, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 9. Kiswahili kikikopa, si ila ndiyo tabia, Na lugha zilonenepa, jambo hili hutumia, Lugha bila ya kukopa, muhali kujitanua, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 10. Kiswahili ni tajiri, kwa fasaha na methali, Na mimi ninafikiri, kimekwishafika mbali, Kimeweza kufasiri, taaluma mbalimbali, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 2 KISWAHILI_STD VII.indd 2

P:10

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY11. Maneno bila hesabDuO, bNadOo TwaDtuUkPuLanICdiAkaT, E Nami nadhani karibu, siku njema itafika, 7/23/21 3:28 PM Yawe katika vitabu, na vinywa kuyatamka, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu.   12. Maneno ya uthabiti, yasiyo na ukakasi, Mengi pia tofauti, kwa fasaha na wepesi, Yenye ladha ya sauti, bado kuona kamusi, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 13. Yaandikwe haya yote, kufuata taratibu, Tuweke juhudi zote, kamusi iwe ajibu, Isifike kila pote, katika zote janibu, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 14. Kiswahili kina sifa, kwa nahau na maana, Hufanya na mataifa, mengi kusikilizana, Kikitoa taarifa, kwa wengi huwa bayana, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 15. Lugha hii ni ya mbele, ingawa leo i nyuma, Walakini polepole, sifa yake inavuma, Itafikia kilele, cha fahari na heshima, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 16. Kiswahili ni Naili, kwa kazi ya ushairi, Ambao hutoa mbali, rutuba hadi Misiri, Masika na jua kali, kila siku husafiri, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 17. Hata tele likijaa, titi jingine si zuri, Mwana aliye na njaa, kunyonya hana hiyari, Lugha ya kigeni pia, ni kaidi kwa amri, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 18. Ninashukuru fahari, sikuumbwa kuwa bubu, Titi jingine si zuri, hili nimelijaribu, Cheo changu hata ari, nikaona laharibu, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. 3 KISWAHILI_STD VII.indd 3

P:11

FOR ONLINE USE ONLY 19. Kukaa bure siwezi, nDdipOo NniOkaTjikDusUuPruL,ICATE Kuandika beti hizi, kama zitapata nuru, Ndiyo ya kwangu makuzi, zikikosa haidhuru, Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu. Shaaban Robert (1947) Pambo la Lugha, uk: 27 – 31. Shairi limefanyiwa marekebisho. Zoezi la kwanza: Ufahamu 1. Onesha vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa kwanza. 2. Kituo katika shairi hili ni kipi? 3. Kituo hicho kina mizani ngapi? 4. Kifungu “mapajani kukuweka” kama kilivyotumika katika ubeti wa pili kina maana gani? 5. Kanuni gani inaelekeza kwamba vina vya mwisho katika shairi la kimapokeo vifanane? 6. Eleza maudhui yanayojitokeza katika ubeti wa kwanza, wa pili na wa tatu. 7. Nini maana ya mstari wa tatu katika ubeti wa nne na wa tano katika shairi hili? 8. Mstari “Kila mtu lugha yake, ndiye mtumishi mwema,” maana yake nini? 9. Eleza kwa kifupi ujumbe wa shairi hili. 10. Pendekeza kichwa cha shairi hili. FOR ONLINE USE ONLYZoezi la pili: Msamiati Tunga sentensi mbili kwa kila neno. 6. beza 7. muhali 1. azimu 8. pote 2. kabwa 9. janibu 3. chemchemi 10. jikusuru 4. mlizamu 5. kiini 4 KISWAHILI_STD VII.indd 4 7/23/21 3:28 PM

P:12

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY DO NOT DUPLICATE Zoezi la 3: Miundo Tunga sentensi tatu kwa kila muundo. 1. …… lakini …… Mfano: Mbele yao alikatiza mbwa mkali lakini hakuwadhuru. 2. …… la …… Mfano: Kasha la kiberiti limeanguka chini. 3. …… za …… Mfano: Kelele za chura zilinipotezea usingizi. Zoezi la 4: Methali Kamilisha methali zifuatazo kwa kutumia maneno yaliyopo kwenye kisanduku. Mfano: Dunia ni kitu dhaifu haifai kujitangaza. ni mateke, amnyimaye punda adesi, jina jema, kuliko mwongo, kama hukijui ulacho, ni nyumba ya njaa, halichukuliwi shoka, haifai kujitangaza, usilitukane, ni mtoto kucheka, usikatae wito 1. ………………… huleta heshima. 2. Jambo la ukucha ………………… 3. Daraja lililokuvusha ………………… 4. Furaha ya mzazi ………………… 5. Fadhila za punda ………………… 6. …………………kamwepushia mashuzi. 7. Afadhali jirani mchawi ………………… 8. Usifunue kinywa, ………………… 9. Zohali ………………… 10. Kataa neno ………………… Zoezi la 5: Mazoezi ya lugha A. Pigia mstari vihusishi katika sentensi zifuatazo: Mfano: Baba amenunua ng’ombe wa maziwa. Viti vya shangazi vimepotea. (i) Mpera umeota katikati ya mipapai. (ii) Mtoto ameokota ganda la muwa. 5 KISWAHILI_STD VII.indd 5 7/23/21 3:28 PM

P:13

FOR ONLINE USE ONLY (iii) Mimi ninapendaDdOagNaaOwTaDkuUkPaaLnIgCaA. TE (iv) Nyumba yetu imejengwa kando ya bahari. (v) Mama anapasua mbao za kuuza. (vi) Kiti nilichokalia jana ni cha mtoto. (vii) Nyafuru amesimama ukingoni mwa barabara. (viii) Makoba amebeba viti vya mjomba. (ix) Mbwa wetu anakunywa maji kwa kulapa. (x) Kulwa ameokota embe chini ya mwembe. B. Andika umoja au wingi wa maneno yafuatayo: FOR ONLINE USE ONLYNa. Umoja Wingi Mfano: chama vyama ungo nyungo (i) chura (ii) vigoda (iii) mtu (iv) simba (v) nyoka (vi) soda (vii) kopo (viii) milima (ix) chuma (x) majengo C. Badili sentensi zifuatazo kuwa katika wakati uliopo hali ya kuendelea. Mfano: Mimi nitacheza mpira kwa uwezo wangu wote. Mimi ninacheza mpira kwa uwezo wangu wote. (i) Juma hujifunza kutunga shairi. (ii) Mwanakwao alikula chakula chote. (iii) Shangazi ameenda kumwandikisha mdogo wangu shuleni. (iv) Kikundi chetu kitafuga kuku wa nyama. (v) Sisi tulipanda Mlima Meru. (vi) Watoto wa baba mdogo walipalilia shamba lao. (vii) Ufugaji wa nyuki uliwaneemesha vijana wa Mzee Hango. (viii) Mwalimu Kabaka alitufundisha tabia njema. (ix) Kabati litakalonunuliwa kesho litawekwa hapa. (x) Merama amekunywa uji wa ulezi. 6 KISWAHILI_STD VII.indd 6 7/23/21 3:28 PM

P:14

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYD. Andika KWELI kwDaOsNenOteTnsDi UyaPLkwICeAli TnEa SI KWELI kwa sentensi isiyo ya kweli katika nafasi uliyopewa. Mfano: Shairi la kimapokeo hufuata kanuni za urari wa vina na mizani. KWELI (i) Mshororo ni mstari katika ubeti. ________ (ii) Shairi si lazima liwe na mghanaji na waghaniwa. ________ (iii) Shairi halibebi ujumbe wowote katika jamii. ________ (iv) Kituo ni mstari wa mwisho katika ubeti wa shairi. ________ (v) Wakati mwingine shairi lina mizani nane. ________ (vi) Aya si ubeti katika shairi. ________ (vii) Katika kuhesabu mizani ya mshororo tunahesabu idadi ya silabi. ________ (viii) Shairi la kimapokeo si lazima vina vya kati na vya mwisho kufanana katika beti zote. ________ (ix) Unaweza kutumia methali katika utunzi wa shairi. ________ (x) Hatutumii kiulizo katika shairi la kimapokeo. ________ E. Pigia mstari vitenzi vikuu, kisha weka herufi T chini ya neno linalohusika. Mfano: Bibi yangu anafuga nyuki. T (i) Leo tumecheza mpira kwa furaha kubwa. (ii) Mimi ninawapenda sana baba na mama. (iii) Otaigo ameandika insha kwa mwandiko mzuri sana. (iv) Kisima kimebomoka mara tu baada ya mvua. (v) Wiki ijayo tutakuwa tunafanya mtihani. (vi) Mtendaji wa kijiji alikuwa anagawa pembejeo. (vii) Wanafunzi wa shule yetu walishinda mechi kwa kishindo. (viii) Baba yao atakuwa anapalilia mikorosho. (ix) Nyumbani kwetu tunauza mafuta ya alizeti. (x) Mtoto alianguka vibaya sana. 7 KISWAHILI_STD VII.indd 7 7/23/21 3:28 PM

P:15

FOR ONLINE USE ONLY F. Oanisha maelezo yDa OkifuNnOgTu ADUnaPBLICkwAaTkEuandika herufi ya jibu sahihi kutoka kifungu B kwenye nafasi iliyoachwa wazi. Mfano: kuwa gizani i Kifungu B Na. Kifungu A (a) shairi (i) Maneno yenye maana sawa _______ (ii) Chakula cha ng’ombe (b) msemo ________ FOR ONLINE(iii) Mwanaume vitani _______(c) kujua jambo USE ONLY (iv) Maneno ya soni ________ (d) maneno ya aibu (v) Sehemu ya juu ya nyumba (e) methali _______ (vi) Mtu anayeonesha njia ______ (f) nyasi (vii) Semi fupi zinazotumia maneno (g) visawe ya kawaida, lakini yakiwa na maana iliyojificha na iliyo tofauti na maana ya kawaida _____ (viii) Huwasilisha ujumbe kwa njia (h) hapati ngeu ya kichogoni ya mkato _____ (ix) Fungu la maneno lenye maana (i) kutojua jambo mahsusi linalotoa fundisho kwa jamii______ (x) Usemi wenye pande mbili (j) nahau zinazokamilishana ____ (k) kiongozi (l) paa 8 KISWAHILI_STD VII.indd 8 7/23/21 3:28 PM

P:16

FOR ONLINE USE ONLY Zoezi la 6: UtunDgaOji NOT DUPLICATE Chagua mada yoyote, kisha itungie shairi la kimapokeo lenye beti tano. Ufahamu Soma shairi hili, kisha jibu maswali yanayofuata. 1. Nitakapojua kutunga vizuri, 7. Nitaandika shairi Siku moja nitaandika shairi Kuelezea raha niliyoipata Kuwashukuru wazazi. Kwa kuguswa na upendo wao, FOR ONLINE USE ONLY Ulonifanya niote ndoto tamutamu. 2. Nitamshukuru mama,   Alenibeba tumboni 8. Nitakapojua kutunga vizuri, Kwa muda wa miezi tisa, Nitaandika shairi, Akiniengaenga kwa upendo. Kuwashukuru wazazi. 3. Nitamweleza nilivyohisi 9. Wazazi wamenifunza Furaha yake Ukuu wa upendo, Kila alipokuwa nami, Ukuu wa tumaini; Akisemezana nami, Wamenifunza Au akinielekeza. Kuwa mnyenyekevu; Wamenifunza 4. Mamangu Kuwa mwenye bidii; Alinibeba mgongoni, Wamenifunza Akiniimbia nyimbo, Kuwa muungwana; Kunituliza. Wamenifunza Kuwa mcheshi; 5. Nitamshukuru babangu Wamenifunza Alesaidiana na mama Kuwa mwenye furaha. Kunibeba na kuniengaenga, Alenipakata kwa huba 10. Nitaandika shairi Akihakikisha Kuwashukuru wazazi Sihangaishwi Kwa kunizaa, Na maradhi ya utotoni. Kunilea, Kunitunza, 6. Nitamweleza nilivyoihisi Kunipenda, Furaha yake Kunifunza. Kila akiniona Na kuongea nami. 11. Nitaandika shairi Kuwashukuru wazazi, Nitakapojua kutunga vizuri. 9 KISWAHILI_STD VII.indd 9 7/23/21 3:28 PM

P:17

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Zoezi la 7: Ufahamu 1. Mshairi anasema kuwa ni lini atatunga shairi? 2. Kwa nini mshairi atamshukuru baba yake? 3. Upendo wa wazazi ulimfanya mtunzi aote ndoto gani? 4. Mshairi amesema wazazi wake wamemfunza nini? 5. Kwa mujibu wa shairi hili, majukumu ya baba na mama au mlezi yanatofautiana? 6. Mshairi anasema furaha yake ilitokana na nini? 7. Kwa nini tunatakiwa kuwapenda wazazi? 8. Ubeti wa nane una mishororo mingapi? 9. Pendekeza kichwa cha shairi hili. 10. Je, shairi hilo lina urari wa vina na mizani? FOR ONLINE USE ONLYZoezi la 8: Msamiati Tunga sentensi mbili kwa kila neno. Mfano: Niliguswa sana na shairi alilotunga mwalimu. Wanafunzi waliguswa na matokeo mazuri ya Darasa la Saba. 1. engaenga 6. huba 2. hisi 7. hakikisha 3. semezana 8. hangaisha 4. elekeza 9. guswa 5. tuliza 10. muungwana Zoezi la 9: Miundo Tunga sentensi mbili kwa kila muundo. 1. Hata hivyo ……… Mfano: Hata hivyo, shangazi amechoka kula wali. 2. ………….. kwetu ……….. Mfano: Shuleni kwetu tumestawisha mahindi. 3. ………… pahala pa__……………… Mfano: Mwaki amesimama pahala pazuri. 4. Badala ya ……………… Mfano: Badala ya kununua gari, anunue bajaji. 10 KISWAHILI_STD VII.indd 10 7/23/21 3:28 PM

P:18

FOR ONLINE USE ONLY Zoezi la 10: MazoezDi yOa lNugOhTa DUPLICATE A. Pigia mstari vielezi katika sentensi zifuatazo: Mfano: Mama atafika kesho jioni. Wanafunzi waliimba wimbo vizuri. (i) Binamu yangu analima kwa bidii. (ii) Mtoto wa mjomba anacheza polepole. (iii) Wanafunzi wameingia darasani. (iv) Baba mkubwa anaishi Tarime. FOR ONLINE(v) Mwalimu atafika saa tatu kamili. USE ONLY (vi) Hapa pameinuka sana. (vii) Mama atafika kesho jioni. (viii) Ndama wataingia zizini. (ix) Kinyonga anatembea kwa maringo. (x) Maji ya kunywa yalimwagika mwaaa! B. Andika visawe vya maneno yafuatayo: Mfano: wali - ubwabwa mlingoti - nguzo (i) kenda (vi) makamo (ii) binadamu (vii) nidhamu (iii) kitendo (viii) bao (iv) ng’atuka (ix) kiasi (v) ning’iniza (x) nchi C. Badili sentensi hizi kuwa katika hali ya mazoea. Mfano: Wazazi wanakarabati shule ya kijiji. Wazazi hukarabati shule ya kijiji. (i) Watanzania wanapenda mpira wa miguu. (ii) Doto alisafiri umbali mrefu kwenda shuleni. (iii) Mtoto amelia kwa sauti kubwa. (iv) Nchama alifika ofisini saa mbili asubuhi. (v) Watoto wanacheza mpira kwa bidii. (vi) Ng’ombe wetu alitoa maziwa mengi. (vii) Wanafunzi waligawiwa vitabu kwa ajili ya kujisomea. (viii) Jogoo aliwika saa kumi alfajiri. (ix) Mwajuma ataogelea bwawani. (x) Kitigwa alikwenda bandarini kuchukua mizigo. 11 KISWAHILI_STD VII.indd 11 7/23/21 3:28 PM

P:19

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYD. Badili sentensi zifuaDtaOzoNkOuwTaDkUatPikLaICwAakTaEti ujao. Mfano: Utukutu wangu uliniponza. Utukutu wangu utaniponza. (i) Musa anaimba vizuri nyimbo za kwao. (ii) Baba anaendesha gari mpaka nje ya nchi. (iii) Sisi tunaishi Kijiji cha Nyarero. (iv) Mlevi ameanguka kwenye mtaro. (v) Wao walikula wali jana. (vi) Dagaa wamepungua sokoni. (vii) Mvua za masika zimeanza kunyesha. (viii) Kilimo cha matunda kimemsomeshea watoto. (ix) Mwanariadha ametunukiwa medali ya dhahabu. (x) Kidado anajua kupika ugali. E. Tunga sentensi mbili kwa kila neno. Kila sentensi iwe na maana tofauti. taa, paa, kaa, koo, kioo, mbuzi, paka, tembo, laki, kata Mfano: Robina alikata mti uliopo uani. Didani anaishi Kata ya Manzese. F. Jibu maswali yafuatayo kwa kupigia mstari jibu sahihi. Mfano: Anakula ugali kwa kijiko. Neno kwa katika sentensi hii ni: kitenzi, kielezi, kihusishi, kihisishi (i) Kaka anacheza mpira vizuri. Neno vizuri katika sentensi hii ni: (kitenzi, kivumishi, kiwakilishi, kielezi) (ii) Mtoto mzuri anafua nguo zake. Neno mzuri katika sentensi hii ni: (kivumishi, kitenzi, kielezi, kiwakilishi) (iii) Damari anapika pilau. Neno Damari katika sentensi hii ni: (kiunganishi, kitenzi, nomino, kiwakilishi) (iv) Mihogo ________ tayari kwa kusagwa unga. (imenyauka, imekauka, imeungua, imechanua) (v) Kaka ameuza viatu ________ vya ngozi. (chao, chake, vyake, yake) 12 KISWAHILI_STD VII.indd 12 7/23/21 3:28 PM

P:20

FOR ONLINE USE ONLY (vi) Mimi ni mtotoDwOa N__O__T_D__U_PkuLzICaliAwTaEnyumbani kwetu. (moja, mbili, pili, chanzoni) (vii) Maneno ya yule kijana ________ sana. (yaliniusi, yaliniudhi, yaliniuzi, yaliniuthi) (viii) Baba amenunua nguo zilizotengenezwa kwa ________ ya kondoo. (safi, supu, sufu, sufi) (ix) Neno ambalo ni tofauti na mengine ni: (panzi, mende, kinyonga, mbu) (x) Moja kati ya yafuatayo ni jina lililo tofauti na mengine: (batamzinga, kanga, batamaji, batabukini) G. Kamilisha methali zifuatazo: Mfano: Mimi nyumba ya udongo, sihimili kishindo. Inafaa kusemea mgomba, ungali wima. (i) Maneno ni daraja, ………………………. (ii) Mfukuzwa kwao, …………………….. (iii) Jiwe la kutupa ngomani ……………….. (iv) Raha haiji ila ……………………………. (v) Riziki kama ajali,………………………… (vi) …………………….. ukienda haurudi. (vii) ………………………, huonana kwa nyaraka. (viii) Mpanda farasi wawili………………….. (ix) Kimya kitanguliapo,………………………….. (x) ………………………………, mtii. Zoezi la 11: Utungaji Tunga shairi la kisasa lenye beti nne kuhusu mada yoyote uipendayo, kisha chambua maudhui na taswira katika shairi hilo. FOR ONLINE USE ONLY 13 KISWAHILI_STD VII.indd 13 7/23/21 3:28 PM

P:21

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Sura ya Pili Utenzi Utangulizi Katika sura hii, utaghani utenzi kwa kuzingatia vina na mizani na kueleza ujumbe uliomo. Hii itakusaidia kuwa mtunzi mzuri wa tenzi. FOR ONLINE Fikiri USE ONLYSifa bainifu za utenzi Ufahamu Soma utenzi ufuatao, kisha jibu maswali yanayofuata. Teknolojia ya kisasa 1. Kuwajuza natamani, 5. Matumiziye si tasa, Na ukweli ujueni, Tutumieni kisasa, Somo kuwapatieni, Ili tuishi kisasa, Faida yake mjue. Maisha tuyageue. 2. Somo talowapatia, 6. Hutumika kila siku, Lahusu teknolojia, Mchana hadi usiku, Mbinu twaihitajia, Giza tumeshalipiku, Maisha ituinue. Himahima twendelee. 3. Maisha itabadili, 7. Mfano takupatia, Ujuzi kila mahali, Wa mpya teknolojia, Ujinga kuukabili, Simu unayoitumia, Hali zetu tuinue. Ndiyo mfano ujue. 4. Hakika teknolojia, 8. Mawasiliano kweli, Upesi changamkia, Siku hizi ni aali, Ujuzi kujipatia, Ni mepesi kila hali, Muda wetu tuokoe. Ni sawia yatimie. 14 KISWAHILI_STD VII.indd 14 7/23/21 3:28 PM

P:22

FOR ONLINE USE ONLY 9. Pia za pesa hudumDaO, NOT DUP1L3I.C ATeTkEinolojia hizi, Si kama zama za zama, Faidaze kwa vizazi, Sasa pesa twazituma, Ubunifu ugunduzi, Kwa simu tusishangae. Himahima twendelee. 10. Biashara meboresha, 14. Palipo mwanya wa rushwa, Malipo kufanikisha, TEHAMA huteremshwa, Malengo kukamilisha, Kodi nyingi huzalishwa, Ndiyo kubwa faidae. Mapato yasipotee. 11. Dunia kama kijiji,FOR ONLINE15. Makini yahitajika, Ni TEHAMA usihoji,USE ONLY TEHAMA ikitumika, Marekani Msumbiji, Uzembe kuuepuka, Ni mafupi masafae. Madhara yasitokee. 12. Utandawazi hakika, 16. Utenzi mwisho mefika, Dunia kuunganika, Chini kalamu naweka, Kotekote kwafikika, Somo limekamilika, Hili ulizingatie. Tijaye mzingatie. Zoezi la kwanza: Ufahamu 1. Katika ubeti wa kwanza, mwandishi analenga kuwapa somo gani wasomaji? 2. Wakati gani teknolojia ya kisasa hutumika? 3. Teknolojia ya kisasa ina faida gani? 4. Maendeleo gani yameletwa na teknolojia ya kisasa? 5. Teknolojia ya kisasa imeleta mabadiliko yapi? 6. Mtunzi ana maana gani anaposema, “Giza tumeshalipiku”? 7. Katika ubeti wa 11, kifungu cha maneno “dunia kama kijiji” kina maana gani? 8. Teknolojia ya kisasa inasaidiaje katika kukusanya kodi? 9. Kwa nini “makini yahitajika” katika kutumia teknolojia ya kisasa katika jamii yako? 10. Umejifunza nini kutokana na utenzi huu? 15 KISWAHILI_STD VII.indd 15 7/23/21 3:28 PM

P:23

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY DO NOT DUPLICATE Zoezi la pili: Msamiati Tumia maneno uliyopewa kutunga sentensi moja kwa kila neno. Mfano: Ufaulu wa somo la Kiswahili katika mtihani wa Darasa la Saba umeongezeka. 1. somo 2. geua 3. aali 4. epesi 5. sawia 6. boresha 7. masafa 8. utandawazi 9. ubunifu 10. tija Zoezi la 3: Vitendawili Tegua vitendawili vifuatavyo kwa kuandika jibu lake kwenye mabano. Mfano: Nina mdomo lakini sina mikono wala miguu. (nyoka) Nyumba yangu ni kubwa lakini mlango mdogo. (chupa) 1. Chumba changu kikubwa lakini nalala peke yangu. 2. Akamatwapo mkiani, hutii amri. 3. Nina mwanangu, ukimkata hakatiki. 4. Tunda langu la ajabu, juu nyama, katikati ngozi na ndani mchanga. 5. Ukimkata shingo leo, kesho anayo nyingine. 6. Mama hana miguu lakini mtoto anayo. 7. Bunduki yangu ikilia, sauti husikika dunia nzima. 8. Hubeba mishale kila aendako. 9. Baba akipiga mbizi, huibuka na ndevu nyeupe. 10. Ukimgusa mwanangu, mimi hucheka. 16 KISWAHILI_STD VII.indd 16 7/23/21 3:28 PM

P:24

FOR ONLINE USE ONLY Zoezi la 4: Mazoezi yDaOlugNhOaT DUPLICATE A. Andika umoja au wingi wa maneno yafuatayo: Na. Umoja Wingi Mfano chungu vyungu mzimu mizimu (i) gego ____________ (ii) ____________ wajasiriamali (iii) chote ____________ FOR ONLINE(iv) ____________ beti USE ONLY (v) mshumaa ____________ (vi) ____________ wadokozi (vii) mzabibu ______________ (viii) ____________ vitovu (ix) kichaa ____________ (x) ukope ____________ B. Andika sentensi zifuatazo katika wakati uliopita. Mfano: Baba amejenga kituo cha kulelea watoto yatima. Baba alijenga kituo cha kulelea watoto yatima. (i) Serikali itatoa mikopo ya fedha kwa wajasiriamali wadogo. (ii) Mjomba anatunga utenzi kuhusu maadili ya jamii. (iii) Mwandishi ataikosoa jamii kwa kuendekeza imani potofu. (iv) Mwalimu hatungi mtihani wa muhula wa pili. (v) Dereva ataendesha gari kwa umakini mkubwa. (vi) Kiranja hasimamii usafi wa mazingira ya shule. (vii) Wanakijiji watachagua viongozi wa kijiji chao. (viii) Wanafunzi wanachimba shimo la takataka shuleni. (ix) Wanachuo watasafiri kuelekea mbuga ya wanyama. (x) Kwaya ya shule yetu itatumbuiza kwenye Sherehe za Muungano. 17 KISWAHILI_STD VII.indd 17 7/23/21 3:28 PM

P:25

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYC. Andika kinyume chaDkOilaNnOenToDkUwPa LmIaCnAeTnoEyafuatayo: Mfano: gumu - laini/rahisi/epesi kimiminika - yabisi (i) dhurika __________ (ii) nuna __________ (iii) karibisha __________ (iv) mkarimu __________ (v) taifisha __________ (vi) werevu __________ (vii) imara __________ (viii) afiki __________ (ix) ghali __________ (x) patikana __________ D. Jaza neno moja sahihi katika sehemu iliyoachwa wazi kutoka kwenye mabano. Mfano: Akida ni mwanafunzi ________tabia njema. (mwenye, mwenyewe, enyewe) Akida ni mwanafunzi mwenye tabia njema. Shangazi _________ simumtelezo kesho. (atanunua, alinunua, amenunua, akinunua) Shangazi atanunua simumtelezo kesho. (i) Mti huu ____________ matunda mazuri sana. (amezaa, umezaa, yamezaa, imezaa) (ii) Wajasiriamali ____________ ni wabunifu wamepewa mtaji wa biashara. (ambaye, ambayo, ambao, ndiye) (iii) Huyu____________mwanafunzi bora kitaifa katika mtihani wa Darasa la Saba. (ndio, ndiyo, ndiye, ndiwe) (iv) Ukulima wa kisasa ____________ budi kutiliwa mkazo ili kuinua uchumi wa nchi yetu. (una, ni, si, hauna) (v) Angalikuwa mwizi____________ na wenzake. (angakamatwa, angelikamatwa, angalikamatwa, angekamatwa) (vi) Wachezaji walichelewa kuingia uwanjani ____________ walielekezwa wafike mapema. (ama, ingawa, kwa sababu, kwa kuwa) (vii) Tabia mbaya____________katika jamii. (haufai, zinapendwa, zinapaswa, hazifai) 18 KISWAHILI_STD VII.indd 18 7/23/21 3:28 PM

P:26

FOR ONLINE USE ONLY (viii) Wanafunzi_D_O__N__O__T__D_U_sPhLaImCbAaTlaEshule sasa hivi. (anapalilia, walipalilia, atapalilia, wanapalilia. (ix) Miche____________ ya mikahawa imepandwa shambani. (wazuri, mzuri, mizuri, kizuri) (x) Mwaka jana, Bahati____________ Darasa la Sita. (alikuwa, atakuwa, amekuwa, anakuwa) E. Badili sentensi zifuatazo kuwa katika kauli halisi. Mfano: Dada aliuliza kuwa unapenda mchezo gani. “Unapenda mchezo gani?” Dada aliuliza. FOR ONLINE USE ONLY Polisi alisema kwamba tunatakiwa kutii sheria bila shuruti. “Mnatakiwa kutii sheria bila shuruti,” polisi alisema. (i) Mwalimu amesema kwamba twende upesi. (ii) Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilisema kwamba tunasajili laini za simu zetu ili kuzuia uhalifu. (iii) Bwana Afya aliuliza kuwa kuna umuhimu gani wa kuchemsha maji ya kunywa. (iv) Mwanafunzi mwenzangu alisema kwamba kalamu yangu inaandika vizuri sana. (v) Mgeni aliuliza kuwa mimi ni nani. (vi) Waziri alisema kwamba ajira huchochea ukuaji wa uchumi. (vii) Mwalimu alisema kwamba nidhamu ni msingi wa maendeleo ya taaluma shuleni. (viii) Mtabiri wa hali ya hewa alisema kwamba mwaka ujao kutakuwa na mvua nyingi. (ix) Kiranja alisema kwamba kila mwanafunzi atatakiwa kuja na ufagio kwa ajili ya usafi. (x) Daktari alimwambia mgonjwa kuwa anaumwa ugonjwa wa malaria. Zoezi la 5: Kazi ya kufanya Tembelea maktaba ya shule yako au shule jirani. Soma tenzi mbalimbali kisha teua utenzi mmojawapo na eleza ujumbe uliomo katika utenzi huo. Zoezi la 6: Utungaji Tunga utenzi wa beti kumi kuhusu mmomonyoko wa maadili katika jamii. 19 KISWAHILI_STD VII.indd 19 7/23/21 3:28 PM

P:27

FOR ONLINE USE ONLY DOSNuOraTyDaUTPaLtIuCATE Ngonjera Utangulizi Katika sura hii, utajifunza kutafsiri lugha ya picha katika ngonjera, kutamba ngonjera na kueleza ujumbe uliomo. Vilevile, utasoma ngonjera na kujibu maswali ya ufahamu na kufanya mazoezi mbalimbali ya lugha. FOR ONLINE USE ONLY Fikiri Tofauti kati ya ngonjera na shairi Ufahamu Soma ngonjera ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata. Kuku Hekima: Nakuja kwa hoihoi, Naja kuwapeni rai, Kuku asotaga yai, Si vizuri kumchinja. Majivuno: Kuku asotaga yai, Kwenye kiota hafai, Ufurahi yuko hai, Ni vizuri kumchinja. Hekima: Nikimwona ni furaha, Yeye ndo hunipa raha, Na haifai kuhaha, Si vizuri kumchinja. Majivuno: Nakuonea huruma, Wajifanyia hujuma, Hakuna alokutuma, Ni vizuri kumchinja. 20 KISWAHILI_STD VII.indd 20 7/23/21 3:28 PM

P:28

Hekima: FOR ONLINE USE ONLY Kwangu nDdiOyeNmOaaTluDmUuP, LICATE Ninanena kwa kalamu, Kuku wangu ni muhimu, Si vizuri kumchinja. Majivuno: Ukiwa kwako nyumbani, Mayai unatamani, Unakosa umakini, Ni vizuri kumchinja. FOR ONLINEHekima: Majivuno sikuwezi, USE ONLY Umejaa ubazazi, Usemayo upuuzi, Yafaa nikukimbie. Majivuno: Upuuzi uko wapi? Vifaranga wako wapi? Kukuyo atoe wapi? Ni vizuri kumchinja. Hekima: Atataga ipo siku, Mchana au usiku, Na uzao takupiku, Si vizuri kumchinja. Majivuno: Siku hiyo siku gani, Kuku atoke uani, Na vifaranga mbawani? Ni vizuri kumchinja. Hatakuja kutotoa, Utabaki kujutia, Wewe ndiwe wazembea, Ni vizuri kumchinja. Hekima: Kejeli nimezoea, Wala siwezi potea, Msingi mejiwekea, Si vizuri kumchinja. 21 KISWAHILI_STD VII.indd 21 7/23/21 3:28 PM

P:29

Majivuno: FOR ONLINE USE ONLY Usemacho mDeOeleNwOa,T DUPLICATE Kwa hoja unazotowa, Si vizuri kutugawa, Mapungufu tulonayo. Hekima: Asante umen’elewa, Kwa hoja nilizotowa, Utata mezongolewa, Kuku wangu hatachinjwa. FOR ONLINEZoezi la kwanza: Ufahamu USE ONLY 1. Taja wahusika wa ngonjera uliyoisoma. 2. Kuku gani si vizuri kumchinja? 3. Kiota katika ngonjera kinaweza kufananishwa na nini katika jamii yako? 4. Nani anayestahili kukaa kwenye kiota? 5. Kwa nini Majivuno anamwonea huruma Hekima? 6. Je, kuku anaweza kufananishwa na nani katika jamii yako? Kwa nini? 7. Ungepewa nafasi ya Hekima, ungemweleza nini Majivuno? 8. Je, ni vema kumchinja kuku asiyetaga? Kwa nini? 9. Kwa nini Majivuno alimwelewa Hekima? 10. Eleza kwa ufupi namna anavyojisikia kuku asiyetaga. Zoezi la pili: Msamiati Tumia jedwali lifuatalo kuunda maneno sahihi utakayoyatumia kujaza nafasi zilizoachwa wazi na kutunga sentensi moja kwa kila neno. P I KUKUV NJ I WA AH F TOTOAU CH I T A N O J MA A L UMU MAGUGUM BE AT AS A 22 KISWAHILI_STD VII.indd 22 7/23/21 3:28 PM

P:30

FOR ONLINE USE ONLY 1. Nyumba ya ndegeDiliOyoNtenOgTenDezUwPaLkIwCaAnTyEasi, udongo, manyoya au njiti ____________ 2. Ndege maarufu anayefugwa ____________ 3. Neno lenye maana sawa na angua ____________ 4. Tendo la kuharibu au kuvuruga mali au maendeleo ya mwingine ____________ 5. Enye sifa au nafasi ya pekee miongoni mwa vitu vingine ____________ 6. Zidi mtu au kitu kingine kwa ukubwa, umaridadi au kwa kigezo chochote kilichowekwa ____________ 7. Toa yai ____________ FOR ONLINE USE ONLYZoezi la 3: Mazoezi ya lugha A. Andika sentensi zifuatazo katika umoja. Mfano: Bibi zetu wanapenda kulima. Bibi yangu anapenda kulima. (i) Ngonjera ni mashairi ya kujibizana yenye kufuata kanuni za vina na mizani. (ii) Wahusika ni sifa muhimu za ngonjera. (iii) Kazi za fasihi zinaeleza matatizo yaliyopo katika jamii. (iv) Wahusika wanatamba ngonjera. (v) Timu za shule zetu zinafungwa na timu za shule za jirani. (vi) Wanafunzi wanatunga ngonjera kwa kushirikiana na walimu. (vii) Wafanyakazi wanakwenda kuwatembelea wagonjwa hospitalini. (viii) Kaka zangu wamepata ushindi katika mashindano ya kurusha mikuki. (ix) Babu zangu ni mashuhuri kwa kuwa ni wakwezi wazuri. (x) Washindi watapewa medali za dhahabu. B. Tumia irabu kujaza nafasi zilizoachwa wazi kuunda maneno sahihi ya Kiswahili. (i) sh__mr__sh__mr__ (vi) f__n__n__ (ii) v__g__l__g__l__ (vii) h__dh__r__ (iii) m__l__mb__n__ (viii) ng__nj__r__ (iv) __t__nz__ (ix) m__ndh__r__ (v) m__j__g__mb__ (x) b__p___ 23 KISWAHILI_STD VII.indd 23 7/23/21 3:28 PM

P:31

FOR ONLINE USE ONLY C. Kamilisha chemshaDbOonNgoOTifuDatUaPyoLIkCwAaTkEuzingatia maelezo ya herufi. a b c d FOR ONLINE ab – Enda huku na kule huku ukijigamba au kuzungumza maneno ya USE ONLYkujisifu. ac – Kidonge ambacho ni dawa ya maradhi fulani cd – Toa taarifa kuhusu jambo fulani. ad – Kifaa kinachotengenezwa kwa karatasi chenye umbo la pembenne cb – Kuwa katika hali ya kulalia, kuegemea au kupumzika juu ya kilichosimama. bd – Kiashirio kama vile kituo kikuu, mkato au mabano D. Jaza nafasi zilizoachwa wazi. Mfano: Pingu ni kwa mhalifu. Kilemba ni kwa kichwa. (i) Kughani ni kwa _______. Kutamba ni kwa _______. (ii) _______ ni ya muda. Taa ni ya _______. (iii) _______ ni ya macho. Mkufu ni wa _______. (iv) _______ ni ya kuona. Pua ni ya _______. (v) _______ ni ya kidole. Viatu ni vya _______. (vi) _______ ni cha ndege. Mzinga ni wa _______. (vii) _______ ni ya mawasiliano. Kamera ni ya _______. (viii) _______ ni ya kunywa. Chakula ni cha _______. (ix) _______ ni wa shule. Mgonjwa ni wa _______. (x) _______ ni la dirisha. Shuka ni la ________. E. Badili sentensi zifuatazo kuwa katika hali timilifu. Mfano: Sote tulishiriki kutamba ngonjera. Sote tumeshiriki kutamba ngonjera. (i) Wahitimu wote walimaliza kufanya mitihani yao. (ii) Sote tulipatiwa namba zetu za kufanyia mtihani. (iii) Kila mtahiniwa alibandika namba yake ya mtihani kwenye dawati lake. 24 KISWAHILI_STD VII.indd 24 7/23/21 3:28 PM

P:32

FOR ONLINE USE ONLY (iv) Wanafunzi wDalOipeNwaOkTadDi UzaPmLwICaAlikToEwa mahafali ya Darasa la Saba. (v) Walimu wote walihudhuria mahafali yetu. (vi) Ukumbi ulipambwa kwa mawaridi ya kila rangi. (vii) Ngoma ya kimasai ilitumbuiza waalikwa wote. (viii) Wavulana walivaa mashati meupe na suruali nyeusi. (ix) Wazazi na walezi waliandaa mashada ya kutuvisha. (x) Wageni walionesha kadi za mwaliko mlangoni kabla ya kuingia ukumbini. Zoezi la 4: Kazi ya kufanya Tamba na wenzako ngonjera ifuatayo: Maisha mazuri ni ya mjini au kijijini? Jeni: Uledi nimetembea, mijini na vijijini, Ndipo nilipogundua, maisha mema mijini, Nakupa zangu hisia, na mawazo akilini, Miji ina starehe, vijijini sizioni. FOR ONLINE USE ONLY Vijijini ni sulubu, kazi bila maakuli, Duka halipo karibu, kilimo na jua kali, Maishaye ni adhabu, wakazi hawana hali, Miji ina starehe, vijijini sizioni. Uledi: Pole kwa safari yako, mijini na vijijini, Nami nilikuwa huko, nimechunguza makini, Mijini mahangaiko, vikumbo na urubuni, Vijijini kuna shibe, twalima kwa maksai. Kule ardhi ni tele, tunajenga kwa nafasi, Tunajijengea shule, wakazi sisi kwa sisi, Mambo yanasonga mbele, kwa mipango si matusi, Vijijini kuna shibe, twalima kwa maksai. Jeni: Mijini njia za lami, vijijini vumbivumbi, Mabasi ni kwa makumi, vijijini hawatambi, Mijini mimi sihami, hapa nimejenga kambi, Miji ina starehe, vijijini sizioni. 25 KISWAHILI_STD VII.indd 25 7/23/21 3:28 PM

P:33

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Na madansi kabakaba, disko kwa wingi sana, Kwenu umeme ni haba, mijini shida hatuna, Mijini pia twashiba, japo mashamba hatuna, Miji ina starehe, vijijini sizioni. Uledi: Ngoja nikuhabarishe, we waongea ya kale, Sisi huku mishemishe, kote nuru teletele, Wewe wataka ubishe, hata uhubiri yale, Mijini na vijijini, ni kuzuri na kubaya. FOR ONLINE USE ONLY Rafiki mimi naona, manufaa kotekote, Kote kwasaidiana, kote twapata mkate, Si vizuri kuvutana, ili nikuzidi kete, Mijini na vijijini, ni kuzuri na kubaya. Jeni tusifanye shari, sote tutembeleane, Miji na vijiji shwari, bidhaa tuuziane, Mwishowe Jeni kwa heri, na mwakani tuonane, Mijini na vijijini, ni kuzuri na kubaya. Jeni: Uledi ninakusifu, kwa mawazoyo bayana, Wewe na mimi ni kufu, sasa twakubaliana, Haifai kukashifu, kashifa si uungwana, Miji na vijiji ndugu, ni kuzuri na kubaya. Zoezi la 5: Utungaji Tunga ngonjera yenye beti tano kuhusu mada yoyote unayoipenda. 26 KISWAHILI_STD VII.indd 26 7/23/21 3:28 PM

P:34

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY DO NSOuTraDUyaPLNICnAeTE Vitendawili Utangulizi Ulipokuwa Darasa la Sita, ulijifunza kutega na kutegua vitendawili. Katika sura hii, utajifunza kutafsiri lugha ya picha katika vitendawili. Pia, utajijengea ujuzi wa kuwa mbunifu na mdadisi. Fikiri Lugha inayotumika katika vitendawili Ufahamu Soma hadithi hii, kisha jibu maswali yanayofuata. Hapo zamani za kale, alikuwapo kijana mmoja aliyeitwa Ranginyingi. Alikuwa anaishi na babu yake kwa sababu wazazi wake wote walikwisha aga dunia. Ranginyingi alikuwa na uwezo wa kipekee wa kujibadilisha rangi. Aliweza kujigeuza hadi akafanana na mandhari ya mahali alipokuwa kwa wakati huo. Aliweza kugeuka na kuwa mweupe pee! Au mweusi tii! Wakati mwingine, mwenye madoadoa. Mara nyingi, usiku ndipo aliweza kuwa katika umbo la kawaida. Kutokana na uwezo huo, hakuna adui aliyeweza kumsogelea, na alikuwa na uwezo wa kujihami bila silaha. Mwanzoni, alipoanza kubalehe, Ranginyingi alikuwa kijana mnyenyekevu, na alitii maelekezo ya babu yake. Hata hivyo, alianza kuwa mtukutu alipofikia miaka ya mwishomwisho ya ujalunga, yaani kipindi kati ya mwanzo wa balehe na utu uzima. Alianza kutumia vibaya uwezo wake wa kujibadili rangi kwa kudokoa vyakula vya majirani na kula bila kutambulika. Majirani wakaanza kumchukia. Wakajaribu kumtafuta ili wamkamate na kumwadibu. Hawakumpata. Mara chache walimzingira, lakini hawakumweza. Mbali na kuwa mdokozi, Ranginyingi alikuwa mdanganyifu kwa watoto pale kijijini. Aliwaibia watu kwa kujifanya mwema kupindukia na kuwahadaa watoto ili wamwamini. 27 KISWAHILI_STD VII.indd 27 7/23/21 3:28 PM

P:35

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYHali hii iliendelea kwa mudDaOmrNefOu.TRaDnUgiPnyLinICgiAaTlieEndelea kuishi kwa ujanja na hadaa. Watu kijijini walijitahidi kumkamata ili wamwadhibu bila mafanikio. Hali hii iliwakatisha tamaa watu wengi. Babu yake Ranginyingi akawa analaumiwa sana kwa kushindwa kumdhibiti mjukuu wake. Hatimaye, kiongozi wa kijiji ikabidi aandae mkutano kujadili tatizo hili. Mkutano ulihudhuriwa na wanakijiji wote, isipokuwa wachache wasiojiweza. Watu wote walionekana kuwa na shauku ya kupata ufumbuzi wa tatizo lile. Kiongozi wa kijiji alianza mara moja kwa kusema: “Ndugu wanakijiji, leo tumekutana ili tujadili tatizo linalomhusu Ranginyingi. Wengi tunamfahamu kijana huyu. Ana uwezo wa kujibadilibadili rangi lakini tatizo si uwezo wake huo. Tatizo ni kuwa anautumia uwezo huo vibaya. Anautumia kuwaibia watu. Sasa, ninakaribisha mapendekezo juu ya namna ya kutatua tatizo hili.” Bi. Kizee mmoja akasimama na kuomba ruhusa aseme. Kiongozi akamruhusu. Bi. Kizee akanena: “Ninashukuru kwa kunipa ruhusa niseme. Mimi hukaa mwishoni kabisa mwa kijiji, lakini tatizo hili nimeshalisikia. Kusema kweli, sijaathirika na tatizo hili. Hata hivyo, ninatambua umuhimu wa kulitatua kabisa tatizo hili. Ndiyo maana leo nimekuja hapa. Hili tatizo mniachie mimi nitalitatua. Nitaanza kesho.” Wanakijiji walifurahi sana na kumshangilia. Kesho yake, Bi. Kizee aliamka mapema na kuanza kumtafuta Ranginyingi. Ranginyingi aliposikia kuwa anatafutwa na Bi. Kizee, aliamua kuhama kijijini na kuelekea msituni. Alikwenda kwa mwendo wake wa kunyata huku akitumia gari lisilotumia mafuta ya mwarabu. Ndani ya msitu, alisikia sauti ya wanyama wakitega na kutegua vitendawili. Aliamua kusogea karibu, akawaona Sungura, Mbweha, Nyani, Kima na Kobe. Nungunungu naye alikuwapo. Wanyama hao walikaa kwenye duara huku Sungura na Mbweha wakiwa katikati wamekalia vigoda. Upande ulioshindwa kutegua kitendawili, uliambiwa kutoa mji mashuhuri ili upatiwe jibu. 28 KISWAHILI_STD VII.indd 28 7/23/21 3:28 PM

P:36

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY Ranginyingi alisikia sauti kutoka mbali ikisema, “Kitendawili! Jini mnywa damu, haangazi bila damu. Jibu au nipe mji kama umeshindwa.” Aliipuuza sauti hiyo na kuendelea na safari yake. Baada ya kutembea masafa marefu, alifika eneo lenye miavuli ya mwituni yenye nguzo moja moja. Alipumzika pale kwa muda; mara usingizi ukamchukua. Alipozinduka kutoka usingizini, alijikuta amekamatwa mikono yote miwili na Bi. Kizee aliyekuwa amemkazia macho kwa utulivu. Alipigwa na bumbuwazi na kubaki mdomo wazi. Bi. Kizee akanena, “Mjukuu wangu, usihofu. Sitakudhuru. Natamka kuwa kuanzia leo, nakuondolea uwezo wako wa kujibadili rangi mbalimbali kwa kuwa umeutumia kutenda maovu. Rudi kijijini ili uishi vizuri na majirani zako.” Baada ya kuondolewa uwezo wa kujibadilibadili rangi, Ranginyingi alirudi kijijini. Wanakijiji walimshukuru Bi. Kizee kwa kazi aliyofanya. Ranginyingi alikaribishwa na babu yake na majirani, na kuanza kuishi maisha ya kawaida kama watu wengine kijijini. 29 KISWAHILI_STD VII.indd 29 7/23/21 3:28 PM

P:37

FOR ONLINE USE ONLY Zoezi la kwanza: UfahDamOuNOT DUPLICATE 1. Ranginyingi ni nani? 2. Mwanzoni Ranginyingi alikuwa kijana wa namna gani? 3. Ranginyingi alibadilika tabia lini? 4. Ranginyingi aliwaibia kina nani? 5. Unafikiri ni kwa nini wanakijiji walimchukia Ranginyingi? 6. Semi zifuatazo ni za aina gani? Zina maana gani? (a) Anajihami bila silaha. (b) Wanamzingira lakini hawamwezi. (c) Gari lisilotumia mafuta ya mwarabu. 7. Taja wanyama ambao walitega na kutegua vitendawili. 8. Kifungu cha maneno “usingizi ukamchukua” kina maana gani? 9. Pendekeza kichwa kinachoweza kufaa kwa hadithi hii. 10. Umejifunza nini kutokana na hadithi uliyoisoma? FOR ONLINE USE ONLYZoezi la pili: Msamiati Tumia maneno yafuatayo kutunga sentensi mbili kwa kila neno. 1. ujalunga 6. nena 2. zingira 7. nyata 3. mdokozi 8. kigoda 4. pindukia 9. masafa 5. ufumbuzi 10. maovu Zoezi la 3: Vitendawili A. Tegua vitendawili vifuatavyo: Mfano: Gari lisilotumia mafuta ya mwarabu. Miguu Tatutatu mpaka Ulaya. Mafiga (i) Hakuna adui anayeweza kumsogelea. ___________ (ii) Jini mnywa damu, haangazi bila damu. _____________ (iii) Napigwa faini kosa silijui. ____________ (iv) Mwavuli wa mwitu una nguzo moja. ____________ (v) Fumole hufuma huku na huko. ____________ (vi) Amefika kabla mjumbe hajarudi. ____________ 30 KISWAHILI_STD VII.indd 30 7/23/21 3:28 PM

P:38

FOR ONLINE USE ONLY (vii) Mtoto wanguDhOataNmObuTlikDi uUkPimLkIuCtaAnTaEwenzake. ____________ (viii) Kabla hajanitazama nimeshampiga. ____________ (ix) Kifa kifanana. ____________ (x) Liwali amekonda sana lakini hana dawa. ____________ (xi) Natumia nne, mbili, tatu. ____________ B. Tega vitendawili viwili kwa kila jibu. (i) kinyonga (ii) moto (iii) kifo (iv) maji FOR ONLINE USE ONLYC. Tega vitendawili viwili kwa kila picha. (i) (ii) (iii) (iv) 31 KISWAHILI_STD VII.indd 31 7/23/21 3:28 PM

P:39

FOR ONLINE USE ONLY D. Fumbua fumbo lifuaDtaOloNkOwaTkDuUtuPmLiaICmAaTelEekezo ya kwenda kulia na chini. Tumia herufi kubwa. 12 3 4 5 6 7 FOR ONLINE USE ONLYKwenda kulia 1. Wamanga wanapigana kwa panga. (herufi 4) 4. Kuku wangu katagia mibani. (herufi 6) 5. Nimezaliwa mlimani nikafunikwa kwa majani jua likanipa joto daima nakwenda mbele siwezi kurudi nyuma. (herufi 4) 6. Nimelala ila nachungulia sinema. (herufi 5) 7. Nyumba yangu haina mlango. (herufi 3) Kwenda chini 1. Amesuka mkeka wake lakini bado analala chini. (herufi 4) 2. Liwali amekonda sana lakini hana dawa. (herufi 7) 3. Bwana afya wa porini. (herufi 4) 5. Saa yangu haijawahi kusimama tangu itiwe ufunguo. (herufi 4) 6. Ukumbuu wa babu ni mrefu. (herufi 4) Zoezi la 4: Mazoezi ya lugha A. Andika wingi wa maneno yafuatayo: Mfano: joho - majoho mkanda - mikanda (i) televisheni ____________ (ii) mkarimu ____________ (iii) nanasi ____________ (iv) ukatili ____________ (v) chupa ____________ (vi) giza ____________ 32 KISWAHILI_STD VII.indd 32 7/23/21 3:28 PM

P:40

FOR ONLINE USE ONLY (vii) mbarika DO_N__O_T__D__U_P__L_ICATE (viii) uzio ____________ (ix) moto ____________ (x) mwanamwali ____________ B. Kanusha sentensi zifuatazo: Mfano: Mariamu alikwenda kupumzika kwa mjomba wake. Mariamu hakwenda kupumzika kwa mjomba wake. (i) Mwanafunzi amekwenda kucheza mpira. FOR ONLINE USE ONLY(ii) Liboli ni kijana mvivu. (iii) Jembe humtupa mkulima. (iv) Mwanajeshi amekwenda vitani. (v) Msafiri aliisahau bahasha juu ya meza. (vi) Mwalimu anamwadhibu mwanafunzi. (vii) Kinyume cha msichana ni kigori. (viii) Mbuzi ametoroka zizini. (ix) Bibi aligombea ubunge wa viti maalumu. (x) Chakula hiki kina chumvi nyingi sana. C. Andika wingi wa sentensi zifuatazo: Mfano: Mtumishi wangu ametoroka nyumbani. Watumishi wetu wametoroka nyumbani. Mkulima anapalilia shamba lake. Wakulima wanapalilia mashamba yao. (i) Mtoto wa Maria alichelewa shuleni. (ii) Kuku wangu ameangua kifaranga. (iii) Mzazi amemlipia mtoto wake ada ya shule. (iv) Mwanafunzi anachezea gololi. (v) Kalamu ya baba haiandiki kabisa. (vi) Mwandishi amesoma gazeti. (vii) Mtaa huu una mti mkubwa sana. (viii) Chakula kilichopikwa na mama ni kitamu. (ix) Mpira wake unadunda sana. (x) Mwanafunzi amempigia simu mzazi wake. 33 KISWAHILI_STD VII.indd 33 7/23/21 3:28 PM

P:41

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYD. Andika neno ambalDo Oni tNoOfauTtiDnUa PmLeInCgAinTeE. Mfano: chura, kaa, mamba, samaki, ndege - ndege asubuhi, kesho, mchana, usiku, jioni - kesho (i) suruali, yai, shati, kaptura, soksi (ii) mjomba, binamu, shangazi, mbunge (iii) muwa, samaki, kangaroo, twiga, ngamia (iv) sufuria, sahani, mkeka, kikombe (v) masega, mizinga, asali, kichuguu (vi) upepo, sauti, chuma, kelele (vii) gurudumu, mkonga, usukani, gia (viii) mwalimu, mhasibu kitabu, hakimu (ix) kumbikumbi, panzi, twiga, kipepeo (x) maharage, njegere, kunde, mchungwa E. Andika sentensi zifuatazo katika mtiririko sahihi. (i) Huingia darasani saa moja na nusu. (ii) Husimama mstarini tayari kwa kwenda nyumbani. (iii) Mwajuma huamka asubuhi na mapema. (iv) Humsikiliza mwalimu kwa makini. (v) Hupanda kitandani kulala. (vi) Hujibu maswali kwa usahihi. (vii) Hupeleka madaftari ofisini kwa mwalimu wake. (viii) Hupata kifunguakinywa. (ix) Huingia nyumbani akionekana mwenye uchovu. (x) Hula chakula cha jioni. Zoezi la 5: Kazi ya kufanya Orodhesha vitendawili ulivyojifunza katika madarasa yaliyotangulia na vile vinavyotumika katika mazingira ya shuleni. Soma vitendawili hivyo darasani kwa sauti. Zoezi la 6: Utungaji Chagua kitendawili kimoja unachokipenda ukitungie hadithi fupi. 34 KISWAHILI_STD VII.indd 34 7/23/21 3:28 PM

P:42

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY DO NOT DUPLICATE Sura ya Tano Tutumie methali zetu Utangulizi Ulipokuwa Darasa la Sita, ulijifunza methali na kueleza mafunzo yake. Katika sura hii, utaendelea kujifunza na kueleza mafunzo yanayopatikana katika methali. Pia, utajifunza kutumia methali katika miktadha mbalimbali. Hii itakusaidia kuwa na uwezo wa kufikisha ujumbe mpana kwa kutumia maneno machache. Pia, itakusaidia katika kuelimisha, kukosoa na kuonya jamii yako. Methali zitakusaidia kukuza lugha ya mazungumzo na ya maandishi. Fikiri Kazi za methali katika jamii Ufahamu Soma habari ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata. Mchelea mwana kulia hulia yeye Bwana na Bibi Pondamali waliishi muda mrefu bila kupata mtoto. Hali hii iliwahuzunisha sana. Kila mara walipowaona watoto wa wenzao, waliumia. Walitamani na wao wapate mtoto. Mke wa Bwana Pondamali ndiye aliyekuwa na simanzi zaidi. Kila siku alijiuliza lini atapata mtoto. Siku moja, wakati mke wa Bwana Pondamali akiwa amejiinamia, mumewe alimshika bega na kumuuliza, “Mke wangu, mbona uko katika lindi la mawazo?” Mke wake hakumjibu. Aliendelea kujiinamia. Mumewe alimsihi kutokuwa na mawazo kila wakati. Bwana na Bibi Pondamali waliendelea kumwomba Mungu ili wapate mtoto kwani waliamini kuwa mwomba Mungu hachoki. Pia, subira yavuta heri. Hatimaye, wakati ulifika ambapo Bwana na Bibi Pondamali walipata mtoto wa kike ambaye walimpa jina la Subira. Subira alilelewa kwa mapenzi makubwa. Wazazi wake walimpatia kila alichohitaji. Pia, walimdekeza kupita kiasi. 35 KISWAHILI_STD VII.indd 35 7/23/21 3:28 PM

P:43

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYSubira alikua akawa msichDaOnaNmOkuTbDwaU. PKLutIoCkAanTaEna malezi aliyopewa na wazazi wake, Subira hakuwa na tabia nzuri. Tabia yake iliwakera wengi katika eneo waliloishi kwani ilikiuka maadili ya jamii kwa ujumla. Siku moja, jirani yao aitwaye Mzee Msemakweli aliwafuata Bwana na Bibi Pondamali nyumbani kwao. Alipofika, aliwaeleza kuhusu tabia isiyoridhisha ya binti yao. Mzee Msemakweli aliwaomba Bwana na Bibi Pondamali wamkanye binti yao kuhusu tabia yake mbaya. Kinyume na matarajio ya mzee Msemakweli, Bwana na Bibi Pondamali walimbeza na kumwambia kuwa yeye na watu wengine wanamwonea kijicho binti yao. Mzee Msemakweli hakutaka kubishana nao. Hivyo, aliamua kuondoka. Kabla hajafika mbali, aliwageukia Bwana na Bibi Pondamali na kuwaambia, “Kumbukeni kuwa mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo.” Subira alifanikiwa kumaliza elimu ya msingi na alichaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari. Alipokuwa huko, aliendelea kukengeuka katika mambo mengi. Mara nyingi, alivunja sheria za shule, ikiwa ni pamoja na kutohudhuria baadhi ya vipindi. Walimu na wanafunzi wenzake walikerwa sana na tabia yake. Kila mara, walimkumbusha kuwa wakati ukiupoteza haurudi, lakini Subira hakuwasikiliza. Hatimaye, wakati ulifika; Subira akamaliza kidato cha nne. Matokeo yalipotoka, Subira hakufanya vizuri. Wazazi wake walisikitika sana kwani hawakutarajia kama binti yao angefanya vibaya. Kutokana na matokeo ya binti yao, Bwana Pondamali aliyakumbuka maneno ya Mzee Msemakweli na alijisemea moyoni, “Kweli mchelea mwana kulia, hulia yeye.” Subira naye alisikitika namna alivyopoteza muda alipokuwa shuleni kwa mambo yasiyofaa. Alijisikia vibaya zaidi alipokumbuka namna wazazi wake walivyomlea kwa mapenzi makubwa na kumpa kila alichohitaji. Aliamua kuwaomba radhi wazazi wake na kuahidi kuwa binti mwema kuanzia wakati huo. Pia, aliwaomba wazazi wake wampe nafasi nyingine aweze kusoma ili arudie mitihani ya kidato cha nne. Wazazi wake walimsamehe na kukubali kumsaidia. Walikumbuka maneno ya Mzee Msemakweli aliyowaambia kuhusu tabia mbaya ya binti yao. Bwana Pondamali aliwaza kwamba laiti yeye na mkewe wangemsikiliza Mzee Msemakweli, yote hayo yasingetokea. Waliamua kwenda kwa Mzee Msemakweli ili kumwomba msamaha kwa kitendo chao cha kumbeza alipokuja kuwaambia kuhusiana na tabia mbaya ya binti yao. 36 KISWAHILI_STD VII.indd 36 7/23/21 3:28 PM

P:44

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Zoezi la kwanza: Ufahamu 1. Bwana na Bibi Pondamali walikaa muda gani bila kupata mtoto? 2. Bwana na Bibi Pondamali walipata mtoto gani? 3. Mtoto wa Bwana na Bibi Pondamali aliitwa nani? 4. Unafikiri ni kwa nini walimpa mtoto wao jina hilo? 5. Nani alikwenda kuongea na Bwana na Bibi Pondamali kuhusiana na tabia mbaya ya binti yao? 6. Kwa nini matokeo ya kidato cha nne ya binti Pondamali hayakuwa mazuri? 7. Je, Bwana na Bibi Pondamali waliyapokeaje matokeo ya mtoto wao? 8. Mtoto wa Mzee Pondamali aliamua kufanya nini baada ya matokeo yake kuwa mabaya? 9. Taja wahusika katika habari uliyoisoma. 10. Eleza maana ya methali zilizotumika katika habari uliyoisoma. 11. Utamsaidiaje mwenzako mwenye tabia zisizofaa shuleni na katika jamii? 12. Umejifunza nini kutokana na habari uliyoisoma? FOR ONLINE USE ONLYZoezi la pili: Msamiati Tunga sentensi kwa kutumia maneno yafuatayo: 1. simanzi 6. kanya 2. lindi 7. beza 3. sihi 8. kijicho 4. dekeza 9. kengeuka 5. kera 10. radhi Zoezi la 3: Methali A. Andika methali zenye maana sawa na hizi zifuatazo: Mfano: Usigombane na mkono ukushikao. Usitukane wakunga, na uzazi ungalipo. Nguzo moja haijengi nyumba. Kidole kimoja hakivunji chawa. (i) Mgonjwa haulizwi dawa. (ii) Akusukumaye hutaka uanguke. (iii) Mbio za sakafuni huishia ukingoni. 37 KISWAHILI_STD VII.indd 37 7/23/21 3:28 PM

P:45

FOR ONLINE USE ONLY (iv) Kidevu kamwamDbOia NndOevTuDkiUlaPaLpaICtaAyeThEuwa mwerevu. (v) Avumaye baharini papa kumbe wengine wapo. (vi) Nyongeza haigombi. (vii) Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba. (viii) Ngoma ikilia sana hupasuka. (ix) Tabibu hazuii ajali. (x) Mtumikie kafiri upate mradi wako. B. Malizia methali zifuatazo: Mfano: Aulizaye si mjinga, ………………… Aulizaye si mjinga, mjinga ni asiyeuliza. FOR ONLINE USE ONLY Pabaya pako …………………......... Pabaya pako si pema pa mwenzako. (i) Mwenda tezi na omo,…………….. (ii) Mgeni siku mbili, ….…………….. (iii) Mla kuku wa mwenzie,…………… (iv) Mbwa wa msasi mkali,…………… (v) Mpanda hila,……………………….. (vi) Usicheze na simba,………………. (vii) Utamu wa muwa,………………….. (viii) Nyama ya nundu,…………............. (ix) Karamu mbili,……………………….. (x) Athari ya kidole,…………………….. C. Oanisha methali kutoka fungu A na maana zake kutoka fungu B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi mbele ya methali. Mfano: Mafiga mawili hayaivishi chungu. - k Mjaliwa ni mmoja, kila mtu ana lake. - l Fungu A (i) Mazoea huleta dharau. ____ (ii) Mwindaji haogopi miba. ____ (iii) Mcheza na tope humrukia. ____ (iv) Mambo ni kangaja, huenda yakaja. ____ (v) Leo ni siku ya mwerevu, kesho ni siku ya mpumbavu. ____ (vi) Kiingiacho mdomoni si haramu. ____ (vii) Maagizo matupu, hayahimizi kazi. ____ (viii) Mvuvi ndiye ajuaye pweza alipo. ____ (ix) Ya malishoni, hayasimuliwi mjini. ____ (x) Jumbe ni watu si kilemba. ____ 38 KISWAHILI_STD VII.indd 38 7/23/21 3:28 PM

P:46

Fungu B FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE (a) Anayehusiana na mtu mbaya huishia kuambukizwa ubaya huo. (b) Mambo huweza kubadilika. Mtu aliyekuwa na neema humwondokea na aliyekuwa fukara huinukia. (c) Kutekeleza jambo kunahitaji vitendo. Tusiridhike na kutoa maelekezo tu. (d) Kuwa kiongozi ni kuwa na matendo mazuri na kuhusiana vizuri na watu. (e) Mtu humdharau mtu mwingine kutokana na mazoea kupita kiasi. FOR ONLINE USE ONLY(f) Ukitaka kufanikiwa katika jambo lolote, lazima uvumilie. (g) Jambo linaloweza kufanyika leo ni bora lifanyike lisingoje kesho. (h) Anayeweza kulielezea jambo vizuri ni yule anayelifahamu na anayehusiana nalo. (i) Ukiona mtu anafanya jambo fulani, lazima jambo lile lina faida kwake. (j) Si vema kuchanganya mambo. Inafaa tujue ni jambo lipi linafaa mahali fulani. (k) Tukitaka kufanikiwa, lazima tuwe na ushirikiano na wenzetu. (l) Hatupaswi kuwaonea wenzetu gere au wivu kutokana na majaliwa yao, kila mtu amejaliwa jaala au majaliwa yake. Zoezi la 4: Mazoezi ya lugha A. Oanisha maneno ya sehemu A na maana zake katika sehemu B na tunga sentensi moja kwa kila neno kutoka sehemu A. Mfano: matata - (c) mvurugiko wa mambo, hali ya vurugu, ugomvi, sokomoko Baada ya timu yao kufungwa, walileta matata uwanjani. kijiji - (g) mahali wanapoishi watu wengi pamoja ambapo si mji Rafiki yangu anaishi kijiji cha jirani. 39 KISWAHILI_STD VII.indd 39 7/23/21 3:28 PM

P:47

Sehemu A FOR ONLINE USE ONLY (i) mofa DO NOT DUSePhLeImCuABTE (ii) kiini (iii) saladi (a) chanzo, sababu au undani wa jambo, (iv) mafya kisa au tukio (v) mseto (vi) matata (b) mafiga (vii) kijiji (c) mvurugiko wa mambo, hali ya vurugu, ugomvi, sokomoko (d) mchanganyiko wa vitu au mambo mbalimbali (e) mkate uliotengenezwa kwa unga wa nafaka (f) mchanganyiko wa mboga au matunda unaoliwa bila kupikwa (g) mahali wanapoishi watu wengi pamoja ambapo si mji FOR ONLINE USE ONLY B. Chagua neno sahihi kutoka katika mabano ili kukamilisha sentensi. Mfano: Tulisafiri usiku kucha kuelekea nchi jirani. (kucha, kutwa) Alijawa na hofu aliposikia kuwa bibi yake ni mgonjwa. (haiba, hofu) (i) Mama ameninunulia nguo zilizotengenezwa kwa_______ (sufi, sufu) (ii) Mjomba wangu anapenda _______ (ufahari, ufaari) (iii) Kwa hakika maneno yako_______sana. (yanauzi, yanaudhi) (iv) Embe lilidondoka kutoka mtini_______ (poo!, puu!) (v) Kula _______nyingi ni kuishi miaka mingi. (chumvichumvi, chumvi) (vi) Baba aliniombea _______ili nikasome shule ya jirani. (likizo, uhamisho) (vii) Baada ya kukimbia mbio ndefu_______ kwa uchovu. (alitweta, alitweka) (viii) Shida za aina mbalimbali huleta_______wa mawazo. (msonge, msongo) (ix) Babu alitembea polepole akiwa na_______wake. (mkongojo, mkongoje) (x) Ndege_______kuelekea mtini. (alikimbia, alipaa) 40 KISWAHILI_STD VII.indd 40 7/23/21 3:28 PM

P:48

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYC. Chagua maana mDoOja NiliOyoTsDahUihPiLkIuCkAamTEilisha semi zifuatazo kwa kuandika herufi ya jibu sahihi kwenye nafasi iliyoachwa wazi. Mfano: Shika tama maana yake ni c (a) fika tamati (b) achia tabasamu (c) shika shavu kwa huzuni (d) shika mtama (i) Hohehahe ni mtu …………………. (a) tajiri mno (b) maskini sana (c) mzembe mno (d) asiyejua kitu (ii) Kudunduliza ni …………………. (a) kuweka kidogokidogo (b) kudundadunda (c) kukopesha (d) kuweka kwa wingi (iii) Kutokuwa na mbele wala nyuma maana yake ni …………………. (a) kutokuwa na tumbo wala mgongo (b) kutokuwa na uso wala kisogo (c) kuwa hohehahe (d) kutokuwa na msimamo (iv) Nyota ya jaha maana yake ni …………………. (a) jua la mchana (b) nyota ya asubuhi (c) bahati nzuri (d) bahati mbaya (v) Kula na kipofu ni …………………. (a) kujifanya mwema ili mtu asikuone mbaya (b) kula na mtu asiyeona (c) kuiba (d) kudanganya 41 KISWAHILI_STD VII.indd 41 7/23/21 3:28 PM

P:49

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY (vi) Kukata maji maDanOa yNaOkeTnDi …U…PL…IC…A…T…E…. (a) kuzama katikati ya maji (b) kutenganisha maji (c) kunywa pombe (d) kukimbilia majini (vii) Kula yamini ni …………………. (a) kushabikia jambo (b) kula chakula kinachoitwa yamini (c) kula sana (d) kuapa (viii) Kutokuwa na masikio ni …………………. (a) kukosa uwezo wa kusikia (b) kutofuata ushauri/maelekezo (c) kutokusikia kengele (d) kutokuwa na kichwa (ix) Shika mkono maana yake ni …………………. (a) toa msaada (b) weka mkono begani (c) kuwa mwizi (d) kushikana mikono (x) Kuwa na shingo ngumu ni …………………. (a) kuwa na shingo isiyogeuka (b) kuwa mkaidi (c) kuvumilia maumivu ya shingo (d) kubeba mizigo mizito D. Bainisha nomino katika sentensi zifuatazo kwa kuzipigia mstari. Mfano: Alipofika, alimkuta bibi amelala. Wachezaji wetu walicheza vizuri ingawa hawakupata ushindi. (i) Darasa letu lina madawati ya kutosha. (ii) Asante sana Mwanaisha. (iii) Shambani kuna mazao mengi. (iv) Watoto wanaimba wimbo mzuri sana. (v) Maendeleo ni muhimu katika jamii yoyote. 42 KISWAHILI_STD VII.indd 42 7/23/21 3:28 PM

P:50

FOR ONLINE USE ONLY (vi) Anakula waliDkiOla sNikOu.T DUPLICATE (vii) Yeye ni mfanyakazi. (viii) Amenunua viatu na soksi. (ix) Timu yao imepata tuzo. (x) Rafiki yake amekuja leo. E. Jaza nafasi wazi kwa kutumia maneno yaliyo katika kisanduku. au, bila, kwa sababu, kama, walau, hata hivyo, harakaharaka, ingawa, wasiwasi, mithili, lakini FOR ONLINE USE ONLY(i) Alilima shamba kubwa ……………….. hakupata mazao mengi. (ii) Alikwenda kazini ……………….. alikuwa mgonjwa. (iii) Alijiandaa …………………….. ili awahi stendi ya basi. (iv) Kunywa chai kidogo ………………. upate nguvu. (v) Nilimsihi sana asiondoke, …………………… hakunisikiliza. (vi) Alichelewa kuamka hivyo, alikuwa na …………… atachelewa shuleni. (vii) Sikuweza kuvuka mto …………………… una mamba wengi. (viii) ………………………… kuvaa miwani hasomi vizuri. (ix) Anatembea kwa maringo ………………… ya twiga. (x) Juma anataka viatu ………………… vya rafiki yake. F. Tumia kamusi, kueleza maana mbili kwa kila neno na tunga sentensi moja kwa kila maana ya neno hilo. Mfano: ndege - chombo cha usafiri wa anga Baba alisafiri kwa ndege kwenda Arusha. ndege - kiumbe chenye manyoya na mabawa na huweza kuruka angani Ndege wa porini walivamia shamba na kula mtama wote. (i) pepeta (vi) vunda (ii) vuguvugu (vii) reli (iii) staha (viii) ngazi (iv) vua (ix) nafasi (v) kitivo (x) marejeo 43 KISWAHILI_STD VII.indd 43 7/23/21 3:28 PM

P:51

FOR ONLINE USE ONLY G. Andika visawe vya mDaOneNnOo TyaDfuUatPaLyoIC: ATE Mfano: uzinduzi - ufunguzi/ufunguaji/uanzishaji randa - tembeatembea/zurura/tangatanga (i) jipu (vi) dhila (ii) adhama (vii) kiinimacho (iii) ombwe (viii) hatia (iv) shupavu (ix) paranganya (v) johari (x) uchunguzi H. Kwa kila sentensi, pigia mstari neno ambalo linaonesha kauli ya kutendeka. Mfano: Kulima si kazi ndogo, haifanyiki kirahisi. Maji yakimwagika hayazoleki. FOR ONLINE USE ONLY(i) Chakula hiki hakiliki maana hakijaiva vizuri. (ii) Andika mwandiko unaosomeka kwa urahisi. (iii) Kiti hiki kimevunjika. (iv) Chai hii hainyweki maana ni ya moto sana. (v) Nguo zako nyeupe hazifuliki, labda utumie dawa ya madoa. (vi) Kunguru hafugiki maana anapenda kuokota majalalani. (vii) Vitu vimejaa sana uwanjani hata havipangiki. (viii) Njia hii ni nzuri, inapitika mwaka mzima. (ix) Kitabu hiki hakisomeki kwani kimechanika vibaya. (x) Ukumbi umepambika kwa mapambo ya aina mbalimbali. Zoezi la 5: Utungaji Tunga habari yenye maneno 80 - 120 yenye methali ndani yake. Zingatia usahihi wa methali utakazotumia. 44 KISWAHILI_STD VII.indd 44 7/23/21 3:28 PM

P:52

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Sura ya Sita Matumizi ya nahau Utangulizi Katika sura hii, utajifunza maana za nahau. Pia, utajifunza kutumia nahau katika miktadha mbalimbali. Hii itakusaidia kupata ujuzi wa kutumia nahau katika lugha ya mazungumzo na ya maandishi. FOR ONLINE USE ONLY Fikiri Matumizi ya nahau katika jamii Ufahamu Soma habari ifuatayo, kisha jibu maswali. Kijiji cha Mwendokasi Busara ni mwanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Tumaini. Anaishi na bibi yake katika Kijiji cha Mwendokasi. Kijiji hicho kipo karibu na Hifadhi ya Wanyama ya Mkomazi. Siku moja Jumamosi, Busara na bibi yake walijihimu kuelekea shambani. Wakiwa wanakaribia kufika shambani, Busara aliwaona wanyama wawili kwa mbali wakitembea kuelekea upande walikokuwa wakielekea wao. Alimshika bibi yake mkono kwa woga, huku akisema, “Bibi! Bibi! Unawaona wale ng’ombe?” Bibi alinyanyua shingo ili awatazame vizuri. Alimjibu huku akiwa amepigwa na butwaa kuwa wale si ng’ombe bali ni tembo. Alimuuliza tena, “Umejuaje kuwa ni tembo?” Bibi alimjibu, “Nawaona kwa mbali ni wanyama wakubwa kuliko ng’ombe. Wana masikio makubwa na mikonga imetangulia mbele.” Waliamua kusimama ili waangalie wanakoelekea. Mara, waliwaona tembo wakiingia kwenye shamba la mahindi na alizeti. 45 KISWAHILI_STD VII.indd 45 7/23/21 3:28 PM

P:53

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY Busara aliogopa sana! Alipiga moyo konde huku akimwambia bibi yake watembee harakaharaka ili warudi kwenye nyumba ya Mzee Sabuni ambayo waliiacha huko nyuma walikotoka. Walipofika kwenye nyumba ya Mzee Sabuni, walimkuta akiwa ameketi barazani pamoja na mke wake. Wakaanza kuwasimulia. Wote walishtuka sana, kwani hawakutegemea kusikia jambo kama hilo. Mzee Sabuni aliondoka na kwenda kumtaarifu jirani yake aitwaye Mafwere. Alipofika, alimsimulia kuhusu kuonekana kwa tembo katika kijiji chao. Hivyo, walishauriana kwenda kwa mwenyekiti wa kijiji ili kutoa taarifa. Walipofika, mwenyekiti aliwaambia kuwa atapiga mbiu ili kuwaita wanakijiji wote. Mbiu ilipigwa, na wanakijiji walipoisikia, walitoka na kukusanyika katika kiwanja kilichopo ofisi za kijiji. Wote walionekana wakiwa na shauku ya kutaka kujua kilichotokea. Walitega masikio kwa makini kumsikiliza mwenyekiti wa kijiji. Mwenyekiti aliwaeleza wanakijiji kuhusu kuonekana kwa tembo wakitembea ndani ya mashamba kijijini kwao. Wote walitahamaki kusikia habari hiyo. Wengi walihofia kuharibiwa mazao yao kwani tembo hukanyaga mazao na kuyaangusha chini. Walimshauri mwenyekiti atoe taarifa kwa uongozi wa hifadhi ya wanyamapori iliyokuwa karibu yao. Baada ya kutoa taarifa hiyo, wanakijiji wote waliungana kwa pamoja wakiwa wamebeba mikuki, mapanga na magobore huku wakikaza mwendo kuwatafuta tembo hao. Wakiwa njiani katika harakati za kuwatafuta, askari wa wanyamapori 46 KISWAHILI_STD VII.indd 46 7/23/21 3:28 PM

P:54

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYnao walifika kwa ajili yaDkOusNaiOdiaTnaDnUaPwLaICnaAkiTjijEi katika kuwatafuta tembo. Walikaza moyo kwani hawakujua tembo walielekea upande gani ndani ya mashamba hayo. Walitembea bila kukata tamaa umbali wa kilomita tatu. Huku wengine wakiwa wamechoka, ghafla, Mafwere aliwaona tembo kwa mbali. Alimshtua mmoja wa askari wa wanyama pori aliyekuwa ameongozana naye. Askari huyo aliwaita wenzake ili wamfuate alipo. Wanakijiji walifurahi sana kusikia kelele za shangwe zikisema, ushindi! Ushindi! Ushindi! Askari waliwasihi sana wanakijiji wasiwarushie tembo mikuki kwani walitaka kuwarudisha katika hifadhi yao. Waliwapongeza sana wanakijiji kwa ushirikiano na juhudi walizozifanya. Kikosi cha askari kiliondoka na tembo wale kuelekea katika hifadhi yao. Wanakijiji walibaki na askari wawili kwa ajili ya kupata maelekezo zaidi. Hapo ndipo waliweza kupata nafasi ya kuuliza na kujibiwa maswali yao. Busara aliuliza, “Kwa nini tusiwatoe uhai? Hawa wanyama wameharibu sana mashamba yetu.” Askari mmoja alimjibu huku akitabasamu na kusema, “Tembo ni mnyama maarufu katika mbuga zetu za Tanzania. Watu wengi wamewaua tembo na kuchukua meno yao na kuyauza nchi za nje.’’ Aliendelea kueleza, “Wanyamapori ni nyara za serikali. Pia, sote tuna jukumu la kuwatunza na kuwalinda.” Mzee Sabuni naye aliuliza swali, “Je, ni kwa namna gani mtaweza kuwazuia tembo wasiingie kwenye mashamba yetu?” Askari mwingine wa wanyama pori alijibu kwa kusema, “Tunawashauri, kama itawezekana, kila mwanakijiji aoteshe pilipili kuzunguka mipaka yote ya shamba. Hiyo itawafanya tembo kushindwa kuendelea mbele kwani, wakati wakitafuta chakula na wakikutana na pilipili, hushindwa kula na kurudi walikotoka. Pia, tengenezeni mizinga ya nyuki kuzunguka mipaka yote ya shamba. Nyuki huingia ndani ya mkonga wake na kusababisha usumbufu. Kelele za nyuki huwasumbua tembo. Wakisikia kelele hizo, hurudi walikotoka.’’ Busara na wanakijiji walifurahishwa sana na majibu ya askari. Walijifunza mambo mengi wakiwa katika harakati za kuwatafuta tembo. Wanakijiji waliwashukuru sana askari hao. Wote waliondoka kurudi nyumbani kwao wakiwa na furaha na amani. 47 KISWAHILI_STD VII.indd 47 7/23/21 3:28 PM

P:55

FOR ONLINE USE ONLY Zoezi la kwanza: UfahDamOuNOT DUPLICATE 1. Kijiji cha Mwendokasi kipo karibu na hifadhi gani? 2. Busara na bibi yake walikwenda wapi siku ya Jumamosi? 3. Nani alikuwa wa kwanza kuwaona tembo? 4. Tembo ni mnyama wa namna gani? 5. Jirani yake Mzee Sabuni aliitwa nani? 6. Mwenyekiti wa kijiji aliwaambia nini wanakijiji? 7. Nani aliyewarudisha tembo katika hifadhi yao? 8. Askari wa wanyamapori aliwaambia wanakijiji wafanye nini ili kuzuia uvamizi wa tembo? 9. Hifadhi za wanyamapori zina umuhimu gani katika nchi yetu ya Tanzania? 10. Umejifunza nini kutokana na habari uliyoisoma? FOR ONLINE USE ONLYZoezi la pili: Msamiati Eleza maana ya maneno yafuatayo: 1. hifadhi 6. gobore 2. mkonga 7. harakati 3. barazani 8. maarufu 4. tahamaki 9. nyara 5. wanyamapori 10. mzinga Zoezi la 3: Nahau A. Eleza maana ya nahau zifuatazo: (i) shika kasi (ii) timba mali (iii) kaa macho (iv) changanya miguu (v) tia ndani (vi) legea moyo (vii) fyata mkia (viii) ng’oa nanga (ix) panda mori (x) kata maji 48 KISWAHILI_STD VII.indd 48 7/23/21 3:28 PM

P:56

FOR ONLINE USE ONLY B. Tunga sentensi kDwOa kNutOumTiDa UnPahLaIuCzAifTuEatazo: Mfano: tia fora - Juma alitia fora alipokuwa akiimba. tia nanga - Meli ilitia nanga ilipofika bandarini. (i) noa ulimi (ii) kuwa kasuku (iii) roho kwenda juu (iv) kaza kamba (v) fuja mipango (vi) tega sikio (vii) ota manyoya (viii) kalia kuti kavu (ix) ponda mali (x) ndimi kali FOR ONLINE USE ONLYZoezi la 4: Mazoezi ya lugha A. Kamilisha sentensi kwa kuchagua jibu sahihi kutoka kwenye kisanduku. sikukuu, wimbo, mazao, matofali, alama, miti, kufunguliwa, zawadi, barua, shule, magari, hufunguliwa, helmeti Mfano: Jana nilipewa zawadi ya usafi shuleni. Msururu wa magari ulionekana ukielekea uwanjani. (i) Mbwa wetu _____________wakati wa usiku. (ii) Tunavaa _____________ tukipanda pikipiki. (iii) Baba amepanda ___________ ya kivuli. (iv) Tumevuna _________________ mengi mwaka huu. (v) Kaka amejenga nyumba ya _____________ ya kuchoma. (vi) Barabarani kuna ______________ za milia. (vii) Tumefungua ________________ mwanzoni mwa mwezi wa Januari. (viii) Mwalimu alitufundisha kuandika ______________ katika kipindi cha Kiswahili. (ix) Juma ameuza mbuzi wengi wakati wa ___________ ya mwaka mpya. (x) Shuleni huwa tunaimba _____________ wa Taifa. 49 KISWAHILI_STD VII.indd 49 7/23/21 3:28 PM

P:57

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYB. Andika kwa usahihi mDaOneNnOo TyaDliyUokPoLsIeCwAaTkEatika sentensi zifuatazo: Mfano: Kaka amekura chakula chote. Kaka amekula chakula chote. Mjomba amenunua zabuni ya kufulia. Mjomba amenunua sabuni ya kufulia. (i) Paka amerara juu ya meza. (ii) Thamaki ni watamu sana kuliko maharage. (iii) Miti yote iliyokuwa pembezoni mwa barabara imesatwa. (iv) Ninakuja kwako jana. (v) Baba amempasha kaka bakora nyingi. (vi) Nitakula uji wangu kesho asubuhi. (vii) Shangazi amenunua gari la dhamani. (viii) Wanafunzi wameimba vizuri shaili lao. (ix) Leo nimenunua pipi kwa shilingi hamthini. (x) Kitabu yangu kina hadithi nzuri. C. Andika kinyume cha kila neno kwa maneno yafuatayo: Mfano: wahi - chelewa kubwa - dogo (i) mnene ____________ (ii) ghasia ____________ (iii) butu ____________ (iv) fukua ____________ (v) pungufu ____________ (vi) mlalo ____________ (vii) hiari ____________ (viii) fanana ____________ (ix) suka ____________ (x) kaka ____________ D. Badili sentensi zifuatazo kuwa katika kauli ya kutendwa. Mfano: Mama anamuogesha mtoto. Mtoto anaogeshwa na mama. Juma ameiba toroli. Toroli limeibwa na Juma. (i) Baraka anachota maji. (ii) Batuli amepika wali. 50 KISWAHILI_STD VII.indd 50 7/23/21 3:28 PM

P:58

FOR ONLINE USE ONLY (iii) Kaka anaoshDaOvyoNmObTo vDyUotPe.LICATE (iv) Wao wanalima shamba. (v) Watoto wanacheza mpira. (vi) Wavuvi wanavua samaki. (vii) Mjomba amevaa koti zuri. (viii) Bibi amelima mihogo mitamu. (ix) Kuku anataga mayai mengi. (x) Mazoea atafua nguo nyingi. E. Pigia mstari vitenzi katika sentensi zifuatazo: Mfano: Mwanamvua anakula ugali. Kiti kimevunjika. (i) Bibi anafua nguo na babu anapasua kuni. (ii) Mwavuli wangu umepotea leo asubuhi. (iii) Nanasi si tamu. (iv) Mjuni amemaliza masomo yake ya sekondari. (v) Mtoto aliogelea mtoni. (vi) Nahodha anaongoza meli vizuri. (vii) Mwalimu anafundisha vizuri darasani. (viii) Daraja limesombwa na maji. (ix) Shimo limejaa uchafu. (x) Paka amekunywa maziwa yote. F. Jaza fumbo lifuatalo kwa kuzingatia maelekezo. ad FOR ONLINE USE ONLY b c ab - weka tayari 7/23/21 3:28 PM bc - mwanzo ad - mwenendo mwema dc - tangazo ac - mvivu/goigoi/legelege/mzembe bd - ni sawa na ac 51 KISWAHILI_STD VII.indd 51

P:59

FOR ONLINE USE ONLY G. Badili sentensi zifuaDtaOzoNkOuwTaDkUatPikLaICukAaTnEushi. Mfano: Makoko anaogelea mtoni kila siku. Makoko haogelei mtoni kila siku. Yule ni baba yangu. Yule si baba yangu. (i) Babu amevuna mahindi mengi mwaka huu. (ii) Bundi ni ndege anayefugwa na binadamu. (iii) Matiku amepanda basi kuelekea mjini. (iv) Siku ya Jumamosi tunakwenda shuleni. (v) Baba anapika chakula jikoni. (vi) Nyumba yetu imebomoka. (vii) Kesho nitapika ugali na dagaa. (viii) Zakia anasuka nywele za aina mbalimbali. (ix) Bustani ya mboga imestawi vizuri. (x) Kaka amechafua shati la shule. FOR ONLINE USE ONLYH. Andika visawe vya maneno yafuatayo: Mfano: laghai - danganya/ghilibu kiitikio - kibwagizo/kipokeo/mkarara (i) kikao ___________ (ii) sumbwi ___________ (iii) buni ___________ (iv) bashasha ___________ (v) dokoa ___________ (vi) fujo ___________ (vii) ghala ___________ (viii) sauti ___________ (ix) gharama ___________ (x) goigoi ___________ Zoezi la 5: Utungaji Tunga hadithi fupi isiyozidi maneno themanini (80) ikiwa na nahau zisizopungua tano (5). 52 KISWAHILI_STD VII.indd 52 7/23/21 3:28 PM

P:60

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY DO NSOuTraDyUaPSLIaCbAaTE Aina za maneno Utangulizi Ulipokuwa Darasa la Sita, ulijifunza dhana ya aina za maneno na kubainisha aina hizo. Katika sura hii, utaendelea kujifunza aina za maneno, namna zilivyogawanyika na kutumia aina za maneno katika sentensi. Hii itakusaidia kufahamu na kuchambua aina za maneno mbalimbali katika lugha. Fikiri Aina za maneno zinazotumika katika mazungumzo ya kawaida Ufahamu Soma masimulizi yafuatayo, kisha jibu maswali. Familia ya Mzee Maneno Katika Kijiji cha Sarufi palikuwa na mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la Maneno. Mzee huyo alikuwa maarufu sana pale kijijini na hakuna ambacho kingefanyika bila yeye kuhusika. Watu wengi walimtumia katika shughuli zao kutokana na umaarufu wake. Siku moja, alikuja mtu mmoja akitokea nchi ya mbali. Mtu huyo aliitwa Shule. Shule alipata habari za Mzee Maneno kuwa ndiye pekee anayetegemewa pale kijijini kwao katika mawasiliano. Shule alivutiwa sana na historia pamoja na masimulizi mbalimbali yaliyomhusu Mzee Maneno. Aliamua kumtafuta ili ajifunze siri ya mafanikio yake. Alijiuliza, kwa nini mzee huyo na familia yake walikuwa maarufu sana hapo kijijini. Shule alipanga safari ya kwenda kujifunza kwa Mzee Maneno ili kuupata ukweli wa historia ya Sarufi. Aliondoka asubuhi baada ya kunywa chai na kwenda nyumbani kwa mzee huyo ili aweze kuijua siri ya kijiji hicho iliyojificha kwa miaka mingi. 53 KISWAHILI_STD VII.indd 53 7/23/21 3:28 PM

P:61

FOR ONLINE USE ONLY “Hodi! Hodi!” Alisikika ShulDe OakiNgoOngTaDmUlaPngLoICwAa TnyEumba ya Mzee Maneno. “Karibu!” Aliitikia mzee mwenye nyumba. Shule aliingia na kusalimia, kisha akaketi. Alijitambulisha kwa kutaja jina lake na kueleza kuwa yeye ndiye anayetegemewa katika kijiji chao kuwaelimisha watu kuhusu mambo kadha wa kadha yanayohusu kauli zao. Alieleza kuwa alikwenda kujifunza siri ya mafanikio ya Mzee Maneno. Mzee Maneno alimtazama, kisha akatabasamu kidogo na kuanza kueleza. Alianza kwa kufafanua kuwa yeye anaitwa Aina za Maneno japo watu wote wamezoea kumwita Mzee Maneno. Aliendelea kueleza kuwa anaishi na watoto wake wote wanane aliowazaa. Aliongeza kuwa hata wajukuu zake wote anakaa nao pale nyumbani. Mzee Maneno alifafanua kuwa siri kubwa ya mafanikio yake ni umoja katika familia yake. Bila kusita, aliwatambulisha watoto wake wote wanane, mmoja baada ya mwingine, kisha akawatambulisha wajukuu zake. Wakati wote huo, Shule alikaa kimya huku akimwona Mzee Maneno kama mtu anayejidai sana. Hii ilitokana na kwamba, hapo awali, Shule alisikia habari kuwa Mzee Maneno ana watoto saba tu. Hivyo, aliona kana kwamba habari hizi zilikuwa zinakinzana. Alimuuliza kwa kejeli kidogo, “Eti una watoto wanane?” Mzee Maneno alimjibu kwa madaha, “Acha pupa. Hebu tega sikio upate kumakinika, maana kila mmoja atajieleza hivi punde.” Aliwataja watoto wake ambao ni Nomino (N), Kiwakilishi (W), Kivumishi (V), Kitenzi (T), Kielezi (E), Kiunganishi (U), Kihusishi (H) na Kihisishi (Hs). Baada ya kuwataja, aliomba kila mmoja ajieleze na awaelezee watoto wake ambao ni wajukuu wa Mzee Maneno. FOR ONLINE USE ONLY 54 KISWAHILI_STD VII.indd 54 7/23/21 3:28 PM

P:62

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY Mtoto wa kwanza alijitambulisha kwa jina la Nomino. Alibainisha kazi zake ambazo ni kutaja majina ya watu, vitu, hali na mahali. Alieleza kuwa anao watoto wanne ambao ni Pekee, Kawaida, Dhahania na Jumla. Alifafanua kuwa Pekee ndiye anayetaja majina ya watu, kwa mfano: Mariamu, Juma na Petro; mahali, kwa mfano: Liwale, Dodoma, Unguja, Tanzania, Mikumi na Zambezi; Sifa yake kubwa ni kuanza kwa herufi kubwa popote atokeapo. Kawaida yeye hutaja viumbe au hali kama vile mvulana, mtu, mama na wilaya. Yeye hafafanui ni mvulana gani, mtu yupi au wilaya gani. Mara zote, huandikwa kwa herufi ndogo, isipokuwa akiwa mwanzoni mwa sentensi. Kawaida huweza kuwa katika umoja au wingi, kwa mfano, mvulana - wavulana, mtu - watu. Dhahania sifa yake ni kutaja dhana za kufikirika tu ambazo hazionekani wala kushikika kama vile upendo, upepo, furaha na joto. Jumla hutaja vitu ambavyo viko katika makundi licha ya kwamba hutajwa kwa umoja. Kama vile kikosi, timu, kwaya, kundi na chama. Mtoto wa pili ni Kiwakilishi. Yeye alisema hufanya kazi pale tu ambapo mkubwa wake Nomino hayupo. Kwa maana nyingine, husimama kama kibadala cha 55 KISWAHILI_STD VII.indd 55 7/23/21 3:28 PM

P:63

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYNomino. Naye aliwatambuDlisOhaNwOaTtotDo UwaPkLeICwaAtTanEo ambao ni Nafsi, Idadi, Viulizi, Vimilikishi na Vioneshi. Alifafanua kuwa Nafsi huwa katika umoja na wingi, kwa mfano, mimi - sisi, wewe - nyinyi na yeye - wao. Idadi huelezea jumla ya watu au vitu ambavyo havikutajwa, kwa mfano wawili, vitatu na matano. Viulizi hutumika kuuliza maswali, kwa mfano, yupi? Wapi? Ngapi? Vimilikishi huelezea umiliki kama vile yangu, chenu na vyao. Vioneshi hutaja maneno ya kuonesha kama vile hiki, kile, vile, hawa, wale na hapa. Kivumishi ni mtoto wa tatu wa Mzee Maneno. Yeye alijipambanua kuwa walipo ndugu zake Nomino au kiwakilishi na yeye yupo. Anatoa taarifa za nyongeza kumhusu Nomino au Kiwakilishi. Aliwatambulisha watoto wake wote watano ambao ni Sifa kama vile kubwa, mnene na mtundu; Idadi, kwa mfano, kimoja, wengi, machache; Kimilikishi, kwa mfano, yangu, chako, vyao; Kioneshi, kwa mfano, kile, pale, kule; Kiulizi, kwa mfano, kipi, yupi, mangapi; na Pekee, kwa mfano, yenyewe, mwenyewe, wenyewe. Mtoto wa nne ni Kitenzi. Huyu alijinadi kuwa pamoja na kuwaheshimu nduguze, anao uwezo mkubwa. Anaweza kusimama peke yake bila kutetereka katika kulielezea jambo ambalo mtu amelitenda. Aliwataja watoto wake watatu ambao ni Kikuu (T), Kisaidizi (Ts) na Kishirikishi (t). Alifafanua kuwa Kikuu ndiye kijana wake mkubwa ambaye pia anaweza kusimama peke yake na kujitosheleza; kwa mfano, Baba anakula chakula. Kisaidizi yeye huwapo kwa ajili ya kumsaidia Kikuu kufanya kazi, kwa mfano, Baba alikuwa anataka kula. Kishirikishi alieleza kuwa na sifa ya kuleta uhusiano na upatanisho, kwa mfano, Baba ni mwalimu, Mama si mlegevu. Kitenzi alionesha sifa zake nyingine ambazo ni uwezo wake wa kubeba viambishi katika mzizi. Kwa mfano, neno anacheza (ana-chez-a) aliweza kuligawa katika sehemu tatu ambazo ni viambishi awali, mzizi na viambishi tamati. Vilevile, aliweza kubadilisha uyakinishi na kuwa ukanushi. Kwa mfano, ninakula lilibadilika na kuwa sili. Kielezi ni mtoto wa tano wa Mzee Maneno. Yeye, katika kujieleza, alimrejelea Kivumishi kwa kusema, “Kama alivyo ndugu yangu kivumishi kuwa anatoa taarifa kuhusu Nomino na Kiwakilishi, basi mimi ninatoa taarifa zaidi kuhusu Kitenzi, Kivumishi au Kielezi mwenzangu.” Aliendelea kusema, “Ninao wanangu wanne ambao ni Mahali, Wakati, Namna na Idadi. Hawa wote hujibu maswali mbalimbali. Mahali hujibu ni wapi tendo linatendekea. Wakati yeye hujibu hoja za muda gani tendo lilitendeka. Namna kazi yake ni kufafanua ni jinsi gani tendo lilitendeka, na Idadi hutoa maelezo ni mara ngapi au kwa kiasi gani tendo hujirudia.” 56 KISWAHILI_STD VII.indd 56 7/23/21 3:28 PM

P:64

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYMtoto wa sita ni KiungaDniOshiNaOmTbaDyeUaPlisLeImCaA,TkEama lilivyo jina lake, ndivyo ilivyo kazi yake. Yeye huunganisha maneno au vifungu vya maneno. Kiunganishi anao watoto wawili tu ambao ni Huru na Tegemezi. Huru husimama peke yake bila kutetereka. Yeye huunganisha maneno yenye miundo sawa. Mfano wake ni na, au, wala, lakini. Tegemezi hawezi kusimama peke yake. Yeye huunganisha maneno yenye miundo tofauti na mfano wake ni kama vile kwa sababu, iwapo, ingawa, ijapokuwa na isipokuwa. Kihusishi ni mtoto wa saba wa Mzee Maneno. Yeye hana mtoto. Kazi yake ni kuhusisha maneno katika tungo. Mfano: Amepanda juu ya paa; Dada anakula kwa kijiko. Mtoto wa nane ni Kihisishi. Huyu ndiye mtoto wa mwisho kwa Mzee Maneno. Yeye pia hana mtoto. Kazi yake ni kuonesha hisia za watu kama vile mshangao, huzuni, huruma, hasira na furaha. Kwa kawaida, huishia na alama ya mshangao. Kwa mfano: Lo! Kumbe! Nini! Ebo! Aisee! Yeye analo jina jingine pia; huitwa Kiingizi. Baada ya utambulisho huo, Mzee Maneno aliongeza kuwa yeye, watoto wake pamoja na wajukuu zake hufanya kazi kwa kushirikiana. Shule alifurahishwa sana na utambulisho wa familia ya Mzee Maneno. Alimpongeza kwa kuwa na familia kubwa kisha alianza safari ya kurejea nyumbani kwake. Zoezi la kwanza: Ufahamu 1. Mzee Maneno aliishi katika kijiji gani? 2. Taja majina ya watoto wa Nomino. 3. Nani alikwenda kumtembelea Mzee Maneno? 4. Kifupisho Hs kinasimama badala ya aina gani ya neno? 5. Kwa mujibu wa habari hii, kitenzi ni nini? 6. Kutokana na habari uliyoisoma, kuna aina ngapi za vivumishi? 7. Kielezi kinachoelezea namna tendo linavyotendeka huitwaje? 8. Taja watoto nane wa Mzee Maneno. 9. Taja watoto wa Mzee Maneno wasio na watoto. 10. Umejifunza nini kutokana na masimulizi uliyosoma? 57 KISWAHILI_STD VII.indd 57 7/23/21 3:28 PM

P:65

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY Zoezi la pili: MsamiatiDO NOT DUPLICATE Tumia maneno uliyopewa kutunga sentensi mbili kwa kila neno. Mfano: jidai - Mzee Maneno alijidai kuwa na watoto na wajukuu lukuki. Wanyamapori hujidai wanapokuwa kwenye makazi yao. 1. jidai 2. kinzana 3. kejeli 4. pupa 5. makinika 6. tenda 7. viambishi 8. mzizi Zoezi la 3: Mazoezi ya lugha A. Pigia mstari nomino katika sentensi zifuatazo: Mfano: Baba amenunua kompyuta nzuri sana. Kulwa na Doto wamefaulu mtihani wao. (i) Mayai yamevunjika yote. (ii) Seremala anatengeneza madawati shuleni. (iii) Wanafunzi wanatazama mashindano uwanjani. (iv) Asha hufua nguo zake kila jioni. (v) Batamzinga anataga mayai bandani. (vi) Mjomba wangu ameuza gari lake. (vii) Hii ni kalamu yangu ya risasi. (viii) Kitabu hiki hakipo mtandaoni. (ix) Alikaribishwa na Mheshimiwa Diwani wa Kibakwe. (x) Mwalimu alitufundisha heshima na adabu. B. Badili kauli halisi kuwa kauli taarifa. (i) Bahati aliuliza, “Kwa nini magari hayapiti hapa siku hizi?” (ii) “Tutatii sheria za barabarani,” madereva walisema. (iii) “Lusinde, kwa nini leo umechelewa darasani?” Kiranja aliuliza. (iv) “Nilijifunza Kiswahili mwezi uliopita,” Nyambura alisema. (v) Mwanafunzi alisema, “Kitabu hiki ni changu.” (vi) “Lo! Hamwogopi kunyeshewa?” Rozata aliwauliza rafiki zake. (vii) Mwalimu aliniambia, “Kiweke kitabu chako mezani.” 58 KISWAHILI_STD VII.indd 58 7/23/21 3:28 PM

P:66

FOR ONLINE USE ONLY (viii) “Chakula hikiDnOi kiNtaOmTu,”DmUtoPtoLIaClisAeTmEa. (ix) “Unamochezea mna hatari,” mama alinionya. (x) Mwalimu aliwaambia wanafunzi, “Mtakwenda Kondoa Irangi kwenye ziara ya kimasomo.” C. Andika neno moja linalojumuisha kifungu cha maneno yafuatayo: Mfano: kunguru, bata, njiwa, kasuku - ndege mpapai, nyasi, mkorosho, mkunde - mimea (i) mkono, mguu, kichwa, macho _____________ (ii) bakuli, sahani, sufuria, ndoo ____________ (iii) gauni, sketi, suruali, kaptura _____________ (iv) kichanga, tifutifu, mfinyanzi _________________ (v) wanga, hamirojo, vitamini, mafuta _________ (vi) sharubati, maji, soda, togwa __________ (vii) mshale, panga, kisu, upinde ___________ (viii) umeme, gesi, mkaa, kuni _________ (ix) almasi, dhahabu, shaba, ulanga ____________ (x) Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda ________ FOR ONLINE USE ONLY D. Oanisha maneno ya fungu A na kinyume chake kutoka fungu B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi kwenye nafasi iliyoachwa wazi. Fungu A Fungu B (i) wajibika _________ (a) dharau (ii) mwaminifu _______ (b) dari (iii) huzuni _________ (c) halali (iv) ubinafsi _________ (d) uvumilivu (v) mvivu __________ (e) mbaya (vi) unyenyekevu _______ (f) ujeuri (vii) nzuri ______________ (g) zembea (viii) heshima __________ (h) mchapakazi (ix) sakafu__________ (i) huzuni (x) bandia__________ (j) laghai (k) wasiwasi (l) ukarimu (m) furaha 59 KISWAHILI_STD VII.indd 59 7/23/21 3:28 PM

P:67

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYE. Nakili sentensi zifuaDtaOzoN, kOisThaDbUaPinLisIChaATaiEna ya neno lililopigiwa mstari kwa kuandika kifupisho cha neno hilo chini yake. Mfano: Watu hawa ni wavivu sana. V Mwanafunzi ametengeneza toroli la miti. T (i) Mtoto wake amepotea. (ii) Tembo ana masikio makubwa. (iii) Wewe unajulikana kila mahali. (iv) Nimepokea taarifa muhimu kutoka kwa mkuu wa shule. (v) Kumbe! Basi tumejua kwa nini haukuja shuleni. (vi) Mwanafunzi yule ni mtiifu. (vii) Hekima ametembea hadi shuleni. (viii) Hakunipa chakula wala chai. (ix) Barua hii imeandikwa na mwanafunzi wa Darasa la Saba. (x) Shukuru alilala fofofo hata hakusikia kelele za kukamatwa kwa mwizi. F. Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kutumia fumbo hili. K I VUM I SH I P KM A V I K NOM I NO I N T J SWM A D I N I E A I D A A D L E CH F K L J B H W S G D CH G T E E I A J E I RUBAN I ZM A AUYOGAPH F I U (i) __________ anaendesha ndege. (ii) Hali ya kuwa na pesa au mali nyingi ___________ (iii) Mtaalamu wa elimu ya nyota _______________ (iv) Musa, mpira, shule, kalamu, viatu ___________ (v) Maskini, fukara, hohehahe, mwombaji _________ (vi) _______hutoa taarifa kuhusu jinsi tendo lilivyofanyika. (vii) Nyumba yangu ina nguzo moja___________ (viii) Chuma, shaba, dhahabu, almasi_____________ (ix) __________ni kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuongoza nchi au kikundi cha watu. (x) Neno linalofafanua nomino au kiwakilishi._________________ 60 KISWAHILI_STD VII.indd 60 7/23/21 3:28 PM

P:68

FOR ONLINE USE ONLY G. Pigia mstari viunDgaOnisNhOi kTatDikUaPseLnICteAnTsiEzifuatazo: Mfano: Mzee Chalunde anakwenda shambani ingawa mvua inanyesha. Alifua nguo zake, kisha akazianika kwenye kamba. (i) Chausiku akitoka shuleni, atapika chakula na kuchota maji. (ii) Baba, mama, watoto, babu, bibi na shangazi huunda familia. (iii) Mwanafunzi bora alizawadiwa madaftari pamoja na begi. (iv) Mwalimu alitoka darasani bila kusema chochote. (v) Vita dhidi ya umaskini, rushwa na ujinga vinaendelea. (vi) Masumbuko alijificha kwani hakutaka kuonekana. (vii) Musa anacheza mpira lakini mimi ninaimba. FOR ONLINE USE ONLY(viii) Mwalimu mkuu alihutubia, ijapokuwa mgeni rasmi alikuwapo. (ix) Muthoni alikwenda Marekani ili kusomea udaktari. (x) Kibongoto alikwenda nyumbani kwa kuwa hakutaka kuchelewa. H. Pigia mstari vielezi katika sentensi zifuatazo: Mfano: Mvuvi alipowasili nyumbani alifurahi sana. Mama alipika chakula upesi. (i) Mtoto huyo hajaonekana nyumbani tangu alipotoka shuleni. (ii) Wanafunzi wa Darasa la Saba watakutana kesho. (iii) Daktari alimwagiza mgonjwa yule anywe dawa mara tatu kwa siku. (iv) Kibuyu cha bibi kilianguka na kuharibika vibaya. (v) Fundi seremala alitengeneza kabati kubwa kwa mbao. (vi) Wahitimu wa Darasa la Saba waliingia ukumbini kwa madaha. (vii) Mwizi wa mbuzi alipigwa mara kadhaa kabla ya kuokolewa na polisi. (viii) Bibi kikongwe anatembea polepole. (ix) Wanafunzi wengi hufanya kazi zao harakaharaka. (x) Kiongozi yule huzungumza kiungwana. Zoezi la 4: Methali Malizia methali zifuatazo kwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi. Mifano: Chuma kukatika ...................... Chuma kukatika si kosa la mhunzi Njia mbili ...................... Njia mbili zilimshinda fisi 61 KISWAHILI_STD VII.indd 61 7/23/21 3:28 PM

P:69

FOR ONLINE USE ONLY 1. Akufanyiaye ubaya …D…O…N…O…T…D…U…PL…IC…A…TE 2. Hucheka kovu ………………………………. 3. Imara ya jembe ……………………………. 4. Jina jema …………………………………….. 5. Kivuli cha fimbo …………………………….. 6. Asiyekuwapo machoni ………………………….. 7. Mwenye kovu …………………………………. 8. Ngoma ikivuma sana …………………………………. 9. Nia njema tabibu ……………………………………… 10. Njia mbili………………………………………………… Zoezi la 5: Utungaji Tunga habari yenye maneno mia moja hamsini (150), kisha pigia mstari vitenzi vyote katika habari hiyo. FOR ONLINE USE ONLY 62 KISWAHILI_STD VII.indd 62 7/23/21 3:28 PM

P:70

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Sura ya Nane Hadithi Utangulizi Ulipokuwa Darasa la Sita, ulijfunza kusimulia hadithi. Katika sura hii, utajifunza kutunga hadithi fupi, kueleza mafunzo yaliyomo na kueleza tabia za wahusika katika hadithi. Maarifa utakayoyapata yatakusaidia kuandika hadithi. FOR ONLINE Fikiri USE ONLYKazi za anayebeba ujumbe katika hadithi Ufahamu Soma hadithi ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata. Kijiji cha Fikika Fikika ni kijiji kilichopo kando ya bahari. Watu wa Kijiji cha Fikika waliishi kwa upendo tangu zamani. Kijiji hicho kiliongozwa na Mzee Bawata tangu kuanzishwa kwake. Mzee Bawata alitokea katika familia duni iliyotingwa na ufukara licha ya kwamba babu wa babu yake alikuwa chifu miaka ya huko nyuma. Mzee Bawata aliishi karne moja. Enzi za utawala wake, aliwafanya watu waishi kwa amani na raha tele. Alifanya juu chini kuwaendeleza watu kimaisha. Aliwainua wanyonge na waliokata tamaa kwa kutumia lugha nzuri yenye ushawishi. Alichukia sana umasikini; hivyo, alihamasisha watu kufanya kazi bega kwa bega ili kuondokana na umaskini. Aliviona vitu vitatu kuwa ni maadui wa maendeleo: ujinga, maradhi na umaskini. Kwa kipindi hicho, vijana na wazee wote walikuwa sawa kutokana na udugu alioujenga. Mzee Bawata alikuwa mzalendo, mpambanaji mashuhuri, mpenda watu na aliyediriki kujinyima mwenyewe kwa manufaa ya wengine. Hakuishia hapo tu, bali aliwatunza waliokuwa na mahitaji maalumu na wale wote wasio na mahitaji maalumu. Watu wote walimwona kama nguzo ya maisha yao. 63 KISWAHILI_STD VII.indd 63 7/23/21 3:28 PM

P:71

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYMzee huyo alipenda maenDdeOleNo.OAlTijiwDeUkePaLmICalAenTgEo ya kazi zake kwa faida ya watu wote. Ajabu iliyoje! Hakuanzia kwenye familia yake katika kutoa huduma. Alikuwa anawashangaza watu. Chochote alichokipata kutokana na kujishughulisha kwake kilikuwa kwa minajili ya kuwaendeleza watu wote kijijini pale. Mzee Bawata alijishusha sana, japokuwa alikuwa mtu maarufu wilayani kwake. Alidiriki kuvaa nguo za kifukara, kula chakula walichokula wanyonge na kulala kwenye malazi ya kawaida, licha ya kuwa ndiye aliyekuwa kiongozi wa kijiji. Katika uongozi wake, aliushangaza ulimwengu kuona anatumia tochi kumulika mchana kweupe. Aliiweka katika kichuguu kirefu kuliko vyote pale kijijini na watu wote waliiheshimu tochi ile. Kuna wakati aliwaita wasaidizi wake na kuwakabidhi tochi ile ili wazunguke kijiji kizima kuwasaka wahalifu. Ilitumika pia kumulika sehemu zote zilizokuwa na giza la maendeleo. Licha ya vijiji vingine kuwa na maendeleo kuliko Kijiji cha Fikika, bado Fikika ilitambulika sana hata kwa wageni waliotoka mbali kutokana na umaarufu wa Mzee Bawata. Kijiji cha Fikika kilikuwa na utajiri mkubwa wa mali. Hata hivyo, wazawa wa Fikika hawakulitambua hilo, kwani kama ujuavyo, penye miti hapana wajenzi. Walikuwa wanakanyaga juu ya mali bila kutambua, sawa na kitendawili kisemacho anacho, lakini hakioni. Licha ya kuwa na kiongozi mwenye maono, baadhi ya Wanafikika hawakuwathamini wanakijiji wenzao. Walitoa msaada kwa watu wa vijiji vya mbali. Walijidanganya kwa kujiona kama wanafanya mambo makubwa, lakini jitihada zao zote ziliishia kwenye kuwapigia makofi wageni waliowakaribisha. Watu hawa wanaweza kufananishwa na baluni lililoishiwa upepo likiwa bado angani. Mzee Bawata alijitahidi sana kuendelea na juhudi zake, lakini ulifika wakati utawala wake ukataka kuangushwa na msaidizi wake. Mzee Bawata alitafakari mara mbilimbili lakini hakujua cha kufanya. Hatimaye, alijisemea moyoni, “Hakuna marefu yasiyo na ncha.” Wakati huo, alionekana mwenye kuishiwa nguvu kutokana na kuzidiwa na uvamizi wa vijiji vingine. Kwa hekima na busara, aliitisha mkutano wa hadhara. Katika mkutano ule, aliongea mambo mengi ya kuwaasa wanakijiji wake. Maneno yake yaliwachoma mioyo baadhi ya watu. Baada ya maneno yale, alitangaza uamuzi wake wa kupumzika uongozi wa kijiji na kubaki kuwa raia wa kawaida. Uamuzi huo ulipokelewa kwa hisia tofautitofauti. Watu wengi walisikitika sana lakini wapo walioshangilia. 64 KISWAHILI_STD VII.indd 64 7/23/21 3:28 PM

P:72

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYWalichaguliwa viongoziDwOenNgiOneTkDutoUkPaLkIaCtikAaTfEamilia nyingine kukiongoza kijiji kile. Viongozi wote waliochaguliwa hawakuweza kufuata nyayo za Mzee Bawata. Wakati huu, Mzee Bawata alikuwa akipumzika nyumbani kwake lakini hakuacha kushirikiana na majirani zake katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali. Wakati mwingine, walimwendea ili kupata ushauri. Naye, bila hiyana, aliwashauri kulingana na mahitaji. Utaratibu wa kurithishana uongozi wa kijiji kile uliendelea miaka kadhaa. Waliitwa watu mbalimbali na kukalishwa mahali pamoja, kisha walianza kuwajadili mpaka apatikane wa kurithishwa uongozi kwa kuwa ulikuwa utaratibu wa kupokezana kijiti. Wakati wote, walijaribu kumtafuta mwenye uelekeo wa kufuata nyayo za Mzee Bawata. Tangu Mzee Bawata aachie ngazi, walipita viongozi kadha wa kadha. Kuna kipindi Mzee Bawata alitumika kama mshauri. Kila kiongozi alikuja na mbinu zake za kiutawala. Hali ya kijiji ilibadilika kila utawala ulipobadilika. Msemo wa kwamba “Binadamu ni mavumbi,” ulidhihirika siku ile Mzee Bawata alipokata roho. Baadhi ya watu walikata tamaa baada ya kuondokewa na mzee wao na kubaki kuchanganyikiwa. Waliweza kuongea bila kufahamu kile walichoongea. Kwao, aliyekuwa akitaja namba kumi, alikuwa sahihi, tano sawa na hata yule wa sifuri alijikuta anapata. Siku moja, katika uchaguzi wa viongozi wa Kijiji cha Fikika, walijitokeza watu wengi kugombea nafasi hiyo. Majina kadhaa yalipendekezwa katika kinyang’anyiro hicho. Miongoni mwao, alikuwamo kijana mmoja kutoka familia duni. Jina lake aliitwa Masanjiro. Wengi hawakudhani kuwa angeweza kushika hatamu kama Mzee Bawata waliyemzoea huko nyuma. Fikira hii ilitokana na ukweli kwamba watu wengi hawakumfahamu, na yeye mwanzoni hakuonesha nia ya kugombea mapema. Hata hivyo, Masanjiro hakuwa mtu wa mchezo. Hakuwa na mzaha katika kazi. Alikuwa na msimamo mkali kuhusu jambo hili. Hakuwa na lugha ya kubembeleza hasa kuhusiana na kufanya kazi kwa juhudi. Alitamka waziwazi kuwa ikiwa angepewa fursa kuwa mrithi, angeweza kusimamia kijiji na kuhakikisha watu wanafanya kazi kama ilivyokuwa mwanzo, hususani enzi za Mzee Bawata. Ulikuwa ukweli usiopingika kuwa historia ya Mzee Bawata ilikuwapo na bado iliendelea kukumbukwa daima kutoka kwa mababu hadi kwa vitukuu. Mzee Bawata aliendelea kuishi, japokuwa alikuwa amekufa. Maneno yake yalizungumzwa kila mahali hapo kijijini na hata nje ya kijiji. 65 KISWAHILI_STD VII.indd 65 7/23/21 3:28 PM

P:73

FOR ONLINE USE ONLY Kama wasemavyo wahenDgaO, “NUmOdThaDnUiaPyeLInCdiAyeTEkumbe siye.” Kijiji kilikaa kimya baada ya wazee wa kijiji kumtangaza Masanjiro kuwa kiongozi wa kijiji. Baadhi ya watu walimwona kama mwendawazimu vile. Wengine walimwona kama malaika aliyeshushwa na Muumba kunusuru kijiji kile. Wengine walisikika wakisema upele umepata mkunaji. Kila mmoja alikuwa na lake la kusema. Jasiri haachi asili. Masanjiro, katika mkutano wake wa kwanza wa hadhara, alitangaza vita dhidi ya wavivu wote wasiopenda kufanya kazi. Alisema kuwa lazima arudishe heshima ya kijiji. Alisisitiza kupambana na maadui watatu aliowatangaza Mzee Bawata enzi za utawala wake. Hivyo, alihamasisha wanakijiji wote kupata elimu ili kuufuta ujinga. Alijenga vituo vya kutolea tiba ili kupambana na adui maradhi. Aliwataka watu wote kuacha kupiga uvivu ili kuondokana na umaskini kwa kuwa mgaagaa na upwa hali wali mkavu. FOR ONLINE USE ONLY Waswahili husema kuwa maji hufuata mkondo. Wanafikika wote, wakubwa kwa wadogo, wake kwa waume, wafanyakazi na wasiofanya kazi, walikuwa kama watu walioamshwa usingizini. Walifanya kazi kwa juhudi, na ndani ya muda mfupi, hali ya kijiji ilibadilika sana. Watu wa vijiji vya jirani na vijiji vya mbali walianza kukiheshimu tena Kijiji cha Fikika. Walianza kuingia kwa adabu kama enzi za Mzee Bawata. Jina la Masanjiro likavuma kama lilivyokuwa jina la Mzee Bawata. 66 KISWAHILI_STD VII.indd 66 7/23/21 3:28 PM

P:74

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYZoezi la kwanza: UfDahOamNuO T DUPLICATE 1. Wanakijiji wa Fikika waliishi maisha ya namna gani? 2. Mzee Bawata alikuwa kiongozi wa wapi? 3. Kwa mujibu wa habari uliyoisoma, nani ni adui wa maendeleo? 4. Viongozi wa Kijiji cha Fikika walipatikana kwa njia gani? 5. Tochi ilitumika kumulika sehemu gani za nchi? 6. Kulingana na hadithi hii, ni viongozi gani walikuwa na sifa zinazofanana? 7. Neno kinyang’anyiro lina maana gani? 8. Masanjiro alifanya nini kukiletea maendeleo kijiji chake? 9. Kwa nini Kijiji cha Fikika kiliheshimika? 10. Umejifunza nini kutokana na hadithi uliyoisoma? Zoezi la pili: Msamiati Tumia maneno haya kutunga sentensi mbili kwa kila neno. 1. karne 2. mzalendo 3. diriki 4. minajili 5. tochi 6. kichuguu 7. wazawa 8. baluni 9. changanyikiwa 10. kinyang’anyiro 11. mzaha 12. vitukuu 13. vuma 67 KISWAHILI_STD VII.indd 67 7/23/21 3:28 PM

P:75

FOR ONLINE USE ONLY Zoezi la 3: Nahau DO NOT DUPLICATE Eleza maana ya nahau zifuatazo: 1. agiza risasi 2. fanya juu chini 3. vunja ungo 4. ng’ata sikio 5. kumbwa na masaibu 6. ota ndoto ya mchana 7. vaa kisua 8. chimba mtu 9. kwenda na maji 10. kula mlungula FOR ONLINE USE ONLY Zoezi la 4: Mazoezi ya lugha A. Kanusha sentensi zifuatazo: Mfano: Mwajuma ni mwanafunzi katika shule yetu. Mwajuma si mwanafunzi katika shule yetu. (i) Mwalimu anafundisha vizuri. (ii) Mimi ninaelewa umuhimu wa kunawa mikono kabla na baada ya kula. (iii) Baraka anapenda kupitia njia ile. (iv) Baba hutumia mitishamba kutibu wagonjwa. (v) Binamu yangu ana suruali nzuri. (vi) Ng’ombe wa Juma anatoa maziwa mengi. (vii) Watoto wa jirani yangu wana tabia nzuri. (viii) Mgonjwa anaweza kunywa uji mwenyewe. (ix) Wanafunzi wengi hupenda mashindano. (x) Yule ni maarufu kwa mchezo wa ngumi. B. Andika maneno sahihi kutokana na silabi zilizochanganywa. Mfano: mbika - kambi (i) rampi ________ (ii) sasia ________ (iii) tomto ________ 68 KISWAHILI_STD VII.indd 68 7/23/21 3:28 PM

P:76

FOR ONLINE USE ONLY (iv) nafunzimwa D_O___N_O__T_ DUPLICATE (v) gokigo ________ (vi) limumwa ________ (vii) ngemwe ________ (viii) komfu ________ (ix) fukum ________ (x) lechem ________ C. Andika visawe vya maneno yafuatayo: Mfano: fahali - dume FOR ONLINE USE ONLY(i) kiitikio ________ (ii) mwalimu ________ (iii) kiinimacho ________ (iv) jaji ________ (v) haraka ________ (vi) fungu ________ (vii) kabeji ________ (viii) kanganya ________ (ix) chache ________ (x) kivumishi ________ D. Pigia mstari jibu sahihi katika maswali yafuatayo: Mfano: Mwalimu mkuu ni ……………. katika shule. (a) kiongozi wa juu (b) kiongozi wa kawaida (c) kiongozi wa wanafunzi tu (d) kiongozi wa chini (i) Mtu anayejenga majengo huitwa ………………... (a) mwashi (b) mkulima (c) boharia (d) msanii (ii) Akimchukua hamrudishi. (a) kifo (b) usingizi (c) furaha (d) huzuni (iii) Ashakumu …………………... (a) ni matusi (b) si matusi (c) ni starehe (d) hukumu 69 KISWAHILI_STD VII.indd 69 7/23/21 3:28 PM

P:77

FOR ONLINE USE ONLY (iv) Mtoto wa mjomDbaOhuNitOwaT_D__U_P__L_IC_ ATE (a) shangazi (b) mjomba (c) binamu (d) mkwe (v) Mara nyingi herufi za mwanzo katika kichwa na habari huandikwa kwa herufi: (a) ndogo (b) kubwa (c) huchanganyika (d) inategemea (vi) Tuzingatie kanuni za afya ili tuepuke ________ la ebola. (a) laana (b) bara (c) baa (d) ujumbe (vii) Kipi ni kitenzi katika maneno yafuatayo? (a) vita (b) upepo (c) bisha (d) vitabu (viii) Sifa moja ya vitendawili ni kutegwa na …… (a) kundi la watu (b) mtu mmoja (c) wasomi tu (d) wasiosoma tuu (ix) Nina chemchemi isiyokauka. Jibu la kitendawili hiki ni: (a) kisima (b) damu (c) maji (d) mate Zoezi la 5: Kazi ya kufanya Waombe wazazi au walezi wako wakusimulie hadithi ambayo utawasimulia wanafunzi wenzako darasani. Zoezi la 6: Utungaji Tunga hadithi unayoipenda yenye maneno yasiyopungua mia mbili (200), kisha eleza mafunzo yanayopatikana ndani ya hadithi hiyo. FOR ONLINE USE ONLY 70 KISWAHILI_STD VII.indd 70 7/23/21 3:28 PM

P:78

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Sura ya Tisa Risala Utangulizi Ulipokuwa Darasa la Sita, ulijifunza kuandika risala kwa kuzingatia muundo wake. Katika sura hii, utaandika risala kwa kuzingatia alama za uandishi na kueleza matumizi ya risala. Hii itakusaidia kuwa mwangalifu, kwani itakuwezesha kutumia lugha ya heshima, iliyo wazi na inayoeleweka. FOR ONLINE USE ONLY Fikiri Matukio muhimu katika hafla yoyote uliyoishuhudia Ufahamu Soma habari hii, kisha jibu maswali yanayofuata. Kutembelea Bunge Kapesa anasoma Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Kikombo. Aliwahi kusikia kuhusu mihimili ya dola. Mhimili mmojawapo aliousikia ni Bunge. Siku moja akiwa shuleni, alimwomba mwalimu wake amweleze zaidi kuhusu Bunge. Mwalimu alikubali na kumwahidi Kapesa kuwa atafanya hivyo darasani. Nia ya mwalimu ilikuwa kuwafundisha wanafunzi wote ili waelewe kuhusu Bunge na shughuli zake. Wakati wanasubiri muda wa kipindi ufike, Kapesa aliwaeleza wenzake juu ya namna anavyotamani kujua habari za Bunge na shughuli zake kwa ujumla. Wanafunzi wenzake walifurahi sana. Wote walimsubiri mwalimu kwa hamu kubwa. Muda ulipotimia, mwalimu aliingia darasani. Wanafunzi wote walikaa kimya, tayari kumsikiliza. Wanafunzi waliamini kuwa mwalimu wao atawapa maelezo ya kina kuhusu Bunge na shughuli zake. Kama walivyotarajia, mwalimu aliwaeleza kila kitu alichoona kuwa ni muhimu wakifahamu. Aliwaeleza kuwa kazi kuu ya Bunge ni kutunga sheria za nchi. Baada ya hapo, aliwapa nafasi 71 KISWAHILI_STD VII.indd 71 7/23/21 3:28 PM

P:79

FOR ONLINE USE ONLY ya kuuliza maswali. WanafDunOzi NwaOliuTlizDaUmPasLwICalAi mTeEngi na mwalimu aliyajibu ipasavyo. Kapesa alikuwa wa mwisho kunyoosha mkono. Mwalimu alimpa nafasi ili aulize swali lake. Kapesa alisema yeye hakuwa na swali, bali alitaka kupendekeza jambo. Mwalimu alimruhusu atoe pendekezo lake. Kapesa alipendekeza kuwa ingefaa zaidi kama wangekwenda kutembelea ofisi za Bunge ili wakajifunze namna shughuli za Bunge zinavyofanyika. Mwalimu na wanafunzi waliunga mkono wazo la Kapesa. Baada ya kipindi, mwalimu aliandika barua kwa Katibu wa Bunge kuomba kwenda kutembelea Bunge. Barua yao ilijibiwa na Katibu wa Bunge. Walipangiwa tarehe ya kwenda bungeni. Siku ilipofika, walikwenda bungeni huko Dodoma. Walipofika, walipokelewa vizuri. Walielezwa kwa ufasaha shughuli zote za Bunge. Baada ya maelezo kutolewa, walikaribishwa kuhudhuria kikao kimoja cha Bunge. Katika kikao hicho, walisikia namna miswada na hoja mbalimbali zinavyojadiliwa na waheshimiwa wabunge. FOR ONLINE USE ONLY 72 KISWAHILI_STD VII.indd 72 7/23/21 3:29 PM

P:80

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYSiku iliyofuata, walianzaDsaOfaNri OyaTkuDruUdPi sLhIuCleAniT. WEalipofika shuleni, mwalimu aliandaa hafla fupi iliyohusisha wanafunzi wa Darasa la Saba na walimu wa Shule ya Msingi Kikombo. Mwalimu mkuu ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo. Wanafunzi waliandaa risala kwa mgeni rasmi ambayo ilisomwa na Kapesa. RISALA YA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA KWA MGENI RASMI, MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI KIKOMBO Ndugu Mgeni Rasmi, kwanza, tunatoa shukurani za dhati kwako na walimu wote kwa kukubali kuhudhuria hafla hii. Pia, tunashukuru kwa kuturuhusu kusafiri kwenda bungeni ili kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali za Bunge. Ndugu Mgeni Rasmi, tukiwa Dodoma, tulitembezwa katika ofisi za Bunge na kuelezwa shughuli zinazofanyika katika kila ofisi. Pia, tulitambulishwa kwa viongozi mbalimbali wa Bunge, yaani Spika, Naibu Spika na wenyeviti. Vilevile, tulielezwa kuhusu kazi za viongozi hao. Kwa mfano, kazi mojawapo ya Spika ni kuongoza vikao vya Bunge. Asipokuwapo, kazi hiyo hufanywa na Naibu Spika. Ikitokea Spika na Naibu wake hawapo, basi vikao vya Bunge huongozwa na mmoja wa wenyeviti. Pia, tulifahamishwa kwamba, kabla ya Bunge kuanza vikao vyake, hutanguliwa na sala ya kuliombea Bunge ambayo huongozwa na kiongozi anayesimamia kikao cha Bunge kwa muda huo. Ndugu Mgeni Rasmi, sisi wanafunzi wa Darasa la Saba tulifurahi sana kupata wasaa wa kutembelea ofisi za Bunge na kujifunza mambo mengi. Hivyo, tunatoa ombi kwako kwamba wanafunzi wawe wanapewa nafasi ya kutembelea sehemu mbalimbali kwa ajili ya kujifunza kazi zinazofanyika huko. Maeneo wanayoweza kutembelea ni pamoja na mahakama, viwanja vya ndege, makumbusho ya taifa na maktaba zetu. Ndugu Mgeni Rasmi, mwisho, kwa unyenyekevu mkubwa, tunawashukuru wewe na walimu wote kwa kutulea vyema tangu tulipoingia Darasa la Kwanza hapa shuleni. Mmetupatia maarifa mbalimbali ambayo tunaahidi kuyatumia katika maisha yetu ya kila siku. Shukurani za pekee zimwendee mwalimu wetu aliyeambatana nasi katika safari yetu na kuhakikisha tunakuwa salama wakati wote. 73 KISWAHILI_STD VII.indd 73 7/23/21 3:29 PM

P:81

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY DO NOT DUPLICATE Ndugu Mgeni Rasmi, tunapokaribia kumaliza Darasa la Saba, tunawatakia kila la heri, wewe na timu yako katika kuendelea kuwalea vyema na kuwapatia maarifa wadogo zetu wanaobaki hapa shuleni. Mungu ibariki Afrika. Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Shule ya Msingi Kikombo. Kapesa alipomaliza kusoma risala, alikwenda kumkabidhi Mgeni Rasmi nakala ya risala hiyo. Mgeni Rasmi alisimama na kuipokea. Walimu na wanafunzi wengine walisimama pia. Mgeni Rasmi aliwashukuru walimu na wanafunzi wa Darasa la Saba kwa kuandaa na kufanikisha ziara yao. Pia, alimpongeza Kapesa kwa kutoa wazo la kwenda kutembelea ofisi za Bunge. Vilevile, aliahidi kuwa kila itakapowezekana, wataandaa ziara kwa ajili ya wanafunzi kutembelea maeneo mbalimbali na kujifunza shughuli zinazofanyika huko. Zoezi la kwanza: Ufahamu 1. Kapesa aliwahi kusikia kuhusu nini? 2. Mhimili mmojawapo wa dola ambao Kapesa aliwahi kuusikia ni upi? 3. Kapesa anasoma shule gani? 4. Kazi kuu ya Bunge ni ipi? 5. Kapesa alitoa pendekezo gani? 6. Mwalimu aliandika barua ya maombi ya kutembelea Bunge kwa nani? 7. Nani alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla iliyoandaliwa na mwalimu wa Darasa la Saba baada ya kutoka bungeni? 8. Nani alisoma risala kwa Mgeni Rasmi? 9. Taja viongozi wa Bunge waliotajwa katika risala. 10. Viongozi hao wanafanya kazi gani bungeni? 11. Kabla ya kuanza vikao vya Bunge, kiongozi wa Bunge hufanya nini? 12. Umejifunza nini kutokana na habari uliyoisoma? 74 KISWAHILI_STD VII.indd 74 7/23/21 3:29 PM

P:82

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY Zoezi la pili: MsamiaDtiO NOT DUPLICATE Eleza maana ya maneno yafuatayo, kisha tunga sentensi moja kwa kila neno. Mfano: kina - undani; umakini Katibu wa Bunge alitoa maelezo ya kina kuhusu shughuli za Bunge. 1. mhimili 2. bunge 3. hamu 4. timia 5. kina 6. muswada 7. mheshimiwa 8. hafla 9. wasaa 10. ombi 11. ambatana Zoezi la 3: Miundo Tunga sentensi mbili kwa kila muundo. 1. Baada ya ………………. Mfano: Baada ya kumaliza elimu ya msingi, alichaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari. 2. …………….. aina ………… za ………… Mfano: Kuna aina mbalimbali za mboga za majani. 3. Pamoja na hayo ……………… Mfano: Pamoja na hayo, sitaweza kuhudhuria mkutano huo. 4. ……………. kwa ……… ili ……….. Mfano: Tueleze kwa ufasaha ili tuelewe vizuri. 75 KISWAHILI_STD VII.indd 75 7/23/21 3:29 PM

P:83

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY5. ………… moja kwa mDoOja …NO…T…D. UPLICATE Mfano: Aliondoka moja kwa moja; hakurudi tena. 6. …………… alipo__ …………… Mfano: Baba alipofika, tulimpa chakula. 7. La hasha! ................................ Mfano: La hasha! Amina hakupita kwetu leo. Zoezi la 4: Nahau Toa maana ya nahau zifuatazo, kisha tunga sentensi kwa kila nahau. Mfano: anua malago - hama Mkazi mmoja wa bondeni alianua malago baada ya nyumba yake kuingiliwa na mafuriko. kaza roho - stahimili, vumilia Kazi ile ilikuwa ngumu, lakini tulikaza roho hadi tukaimaliza. 1. chukua muda 2. tega sikio 3. kula jiwe 4. fungua macho 5. shika usukani 6. mwaga unga Zoezi la 5: Mazoezi ya lugha A. Panga sentensi zifuatazo ili kupata kifungu cha habari chenye maana. (i) Watoto hufurahi zaidi katika msimu huu. (ii) Pia, wanafunzi hujiandaa kurejea shuleni kwa ajili ya muhula mwingine wa masomo. (iii) Wengine husafiri pamoja na wazazi wao kwenda kuwaona ndugu, jamaa na marafiki. (iv) Msimu wa sikukuu, hasa za mwisho wa mwaka, huwa na shamrashamra za kila aina. 76 KISWAHILI_STD VII.indd 76 7/23/21 3:29 PM

P:84

FOR ONLINE USE ONLY (v) Ingawa vitu hDuOuzwNaOkTwaDbUePi yLaICjuAuT, kEila mtu hupenda kununua vitu vipya kwa ajili ya familia yake. (vi) Wakifika shuleni, kila mmoja husimulia namna alivyofurahia sikukuu za mwisho wa mwaka. (vii) Hufurahia kupata nguo mpya na kwenda kutembea. (viii) Msimu wa sikukuu ukiisha, waliosafiri hurejea makwao. (ix) Vyombo vya usafiri hupata abiria wengi wanaokwenda na kutoka sehemu mbalimbali. (x) Wafanyabiashara hufanya biashara zaidi kipindi hiki. B. Tumia maneno yaliyo katika kisanduku ili kukamilisha sentensi. amevaa miwani, tulipokelewa kwa mikono miwili, alikubali kwa ulimi, waliangua kicheko, ilitia fora, tulipiga pasi, alishika mkia, kata tamaa, imepiga marufuku, bega kwa bega (i) Sheria ya mazingira …………… kulima kandokando ya mto. (ii) Katika mbio za wanyama, kobe …………………… (iii) Babu alianguka kwenye tope kwa sababu alikuwa …………… (iv) Tulipotembelea shule ya jirani, ………………….... na wenyeji wetu. (v) Baada ya kubishana kwa muda mrefu, Swalehe …………… tu. (vi) Alipopita yule mlevi, watu wote ………………. (vii) Shule yao ……………… katika mashindano ya mbio ndefu. (viii) Wanakijiji walihimizwa kufanya kazi ……………. ili kupata mazao mengi. (ix) Kabla ya kuanza safari, …………….. nguo za kuvaa bungeni. FOR ONLINE USE ONLY 77 KISWAHILI_STD VII.indd 77 7/23/21 3:29 PM

P:85

FOR ONLINE USE ONLY C. Oanisha methali kuDtoOkaNfuOnTguDAUPnaLImCaAaTnEa zake kutoka fungu B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi kwenye nafasi uliyopewa. Fungu A Fungu B (i) Kikulacho ki nguoni (a) Watu hufanya wanavyotaka mwako. ______ kama kiongozi wao/mkubwa (ii) Halahala mti na macho. wao hayupo ______ (b) Turidhike na vitu tulivyonavyo, (iii) Furaha ya kima mbwa hata kama ni vibaya. asiwepo. ______ (c) Tujitegemee badala ya kuwategemea au kuwatarajia FOR ONLINE(iv) Kijiti kimoja hakisimamishi USE ONLY watu wengine watufanyie mambo jengo. ______ yanayotuhusu. (v) Maasi hufilisi heri za (d) Mtu anayeweza kukudhuru au mtu. ______ kukufanyia mambo mabaya ni (vi) Mkwamba hauzai zabibu. yule anayekufahamu vizuri. ______ (e) Wanapopigana wakubwa (vii) Baya lako si jema la wanaoumia ni wadogo. mwenzako. ______ (f) Tufanye mambo kwa uangalifu. (viii) Usichezee maji yaliyotuama. (g) Matendo mabaya ya mtu humletea sifa mbaya. ______ (h) Ili tuweze kufanikiwa katika (ix) Wapiganapo fahari mambo mbalimbali, tunapaswa wawili, ziumiazo nyasi. kushirikiana na watu wengine. ______ (i) Usitarajie jambo lisilowezekana (x) Mwenye lake usimngoje kutokea. na lako. ______ (j) Usimdharau mtu mwingine; ni vema kuchukua tahadhari kwa kila jambo. D. Jaza herufi zinazoendana na namba ili kupata maneno sahihi, kisha tunga sentensi moja kwa kila neno. A B CH D E F G H I J 1 3 5 7 9 11 13 15 17 19 K L MN OP R S T U 21 23 25 27 29 31 33 35 37 39 78 KISWAHILI_STD VII.indd 78 7/23/21 3:29 PM

P:86

FOR ONLINE USE ONLY V W DYO NOT ZDUPLICATE 41 43 45 47 Mfano: 3 39 27 13 9 B UNGE Bunge letu linafanya kazi ya kutunga sheria. (i) 21 FOR ONLINE 1 37 17 3 39 USE ONLY (ii) 33 17 1 35 15 9 (iii) 35 31 17 21 1 33 1 (iv) 47 17 1 (v) 1 11 23 1 15 1 33 1 21 1 (vi) 43 (vii) 1 11 1 33 17 35 79 KISWAHILI_STD VII.indd 79 7/23/21 3:29 PM

P:87

FOR ONLINE USE ONLY (viii) DO NOT DUPLICATE 15 29 19 1 (ix) 25 19 1 7 1 23 1 (x) 41 17 21 1 FOR ONLINE 29 USE ONLY E. Andika sentensi kwa kutumia kinyume cha neno lililokolezwa wino. Mfano: Mbuzi ameingia zizini. Mbuzi ametoka zizini. Samani zote zimenunuliwa kwa bei nafuu. Samani zote zimeuzwa kwa bei nafuu. (i) Wakulima walikwenda shambani wakati wa machweo. (ii) Acha kunifurahisha kwa kunivika kilemba cha ukoka. (iii) Yule aliyevaa kilemba ndiye aliyeshindwa. (iv) Ungalichelewa kidogo, ungalipanda basi. (v) Someni habari hii kimyakimya. (vi) Alianguka kwa kishindo alipokuwa akishuka kwenye mnazi. (vii) Gauni hili ni dogo sana kwa binti yangu. (viii) Nani amesema chumvi ni chungu? (ix) Mwanzo wa likizo yako umekaribia. (x) Wageni wamekatazwa kukaa hapa. F. Panga vizuri maneno yanayounda methali yaliyochanganywa ili kupata methali sahihi. (i) Kazi ya makosa haina Mungu (ii) Kwa upitao mbachao msala usiache (iii) Kisa ya mkasa baada 80 KISWAHILI_STD VII.indd 80 7/23/21 3:29 PM

P:88

FOR ONLINE USE ONLY (iv) Hakivunji kidDoleOcNhaOwTa kDimUoPjaLICATE (v) Cha hufa nduguye mtegemea maskini (vi) Huishia mbio za ukingoni sakafuni (vii) Ovyo hula mpanda ovyo (viii) Ndiye mla simba mwenda nyama pole (ix) Harabu ya nazi mbovu nzima (x) Huvuma mkuu mshindo mbali G. Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kuchagua jibu sahihi kutoka katika kisanduku. angeanza, kwa ajili ya, asingechelewa, ngoma, angekuja, kwa muda, wakati, alikuwa na, mnamo, mbali na, baada ya, inakupasa, ndipo, matanga, kabla ya (i) Mgeni wetu alifika nyumbani ……………. saa mbili usiku. (ii) Kama ……………. jana, angetukuta wote. (iii) Bahati …………… kuanza safari, angefika mapema. (iv) Tumekusanyika uwanjani ……………. kuangalia mechi ya mpira wa miguu. (v) Walipitiwa na usingizi ………………… kukaa macho kwa muda mrefu. (vi) Nyumbani kwao ni ……………………. stendi ya basi. (vii) Mgeni Rasmi alihutubia ………………… wa dakika arobaini na tano. (viii) Nilitembea umbali mrefu …………… kupanda gari. (ix) …………….. ufanye mazoezi ya kutosha ili upate ushindi. (x) Mtoto mkaidi mngoje siku ya …………….. FOR ONLINE USE ONLY 81 KISWAHILI_STD VII.indd 81 7/23/21 3:29 PM

P:89

FOR ONLINE USE ONLY H. Andika sentensi zifuDaOtazNoOkaTtiDkaUuPhLaIlCisAiaTwEake. Mfano: Rubani anatengeneza samani. Rubani anaendesha ndege. Jua huchomoza upande wa Magharibi. Jua huchomoza upande wa Mashariki. (i) Nahodha anatengeneza gari. (ii) Kazi ya seremala ni kutengeneza magari. (iii) Kulinda nchi ni jukumu la jeshi la wananchi. (iv) Kuongoza magari barabarani ni kazi ya wapita njia. (v) Wakati wa mafuriko, miundombinu kama vile barabara huimarika. (vi) Meli hutia nanga darajani. (vii) Njia ya garimoshi hutengenezwa kwa kiwango cha lami. (viii) Mpira wa miguu huchezwa na wanaume tu. (ix) Kujenga nyumba ni kazi ya kila mtu. (x) Baadhi ya watoto hawatakiwi kupata elimu. FOR ONLINE USE ONLY Zoezi la 6: Utungaji Andika risala kwa mgeni rasmi ambaye ni mwalimu wa darasa kumshukuru kwa namna alivyokuwa pamoja nanyi tangu mlipoingia Darasa la Saba. 82 KISWAHILI_STD VII.indd 82 7/23/21 3:29 PM

P:90

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY DO NSOurTaDyUaPKLIuCmATi E Kusoma magazeti Utangulizi Katika sura hii, utajifunza kueleza maana za maneno mapya, kuyatungia sentensi na kuchanganua mawazo muhimu katika matini za kisiasa, kiuchumi na kijamii kwenye magazeti. Fikiri Ujumbe muhimu unaoweza kuupata katika magazeti Ufahamu Soma habari ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata. Makini asoma makala kwenye gazeti Makini alikuwa anasoma Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Azimio. Alipenda kusoma magazeti. Siku moja alimwomba baba yake fedha ili aende kununua gazeti. Baba yake alikubali na kumpatia shilingi elfu moja. Makini aliondoka kuelekea kibanda cha magazeti akiwa na furaha. Alipofika kibandani, alinunua gazeti. Alipolifunua, aliona makala. Ilikuwa inahusu vyuo vya ufundi, sifa za kujiunga na vyuo hivyo na fani zinazotolewa na mchango wake katika soko la ajira kwa vijana. Makala hiyo ilimfurahisha sana Makini. Kesho yake, aliamua kwenda na gazeti lile shuleni ili akamwoneshe rafiki yake. Alipofika shuleni, alimwita rafiki yake Doto ili waisome makala hiyo. Makala yenyewe ilikuwa imeandikwa kama ifuatavyo: “Vyuo vya ufundi ni taasisi za elimu zinazotoa mafunzo ya ujuzi wa kazi katika fani mbalimbali kama uashi, uchongaji, ushonaji, ufundi bomba, ufundi chuma, ufinyanzi, ufundi umeme, useremala, umakanika, upambaji, ufumaji, upishi, na nyinginezo. Vijana wanaojiunga na vyuo vya ufundi ni wale waliohitimu Darasa la Saba na Kidato cha Nne. Katika vyuo hivi, vijana hujifunza fani mbalimbali ambazo huwasaidia kujiajiri. 83 KISWAHILI_STD VII.indd 83 7/23/21 3:29 PM

P:91

FOR ONLINE USE ONLY Vijana wanapojiunga naDvOyuNo OhiTvyDo UhuPjLifuICnzAaTmEasomo kwa nadharia na vitendo. Kwa hiyo, walimu huwafundisha wanachuo nadharia zote zinazohitajika. Wanachuo hutumia nadharia hizo wanapofanya kazi kwa vitendo, wakati wa mazoezi. Hivyo, nadharia na vitendo hufundishwa sanjari. Vijana wanaomaliza kozi na kufaulu, hupewa vyeti vinavyo o n e s h a f a n i walizofuzu na viwango vya madaraja waliyopata. Vijana wanapohitimu katika taaluma hizi, hujiajiri wenyewe. Watu mbalimbali wanahitaji vifaa kama meza, viti, makabati, mapambo na nyumba za kuishi. Vilevile, wanahitaji vifaa vingine kama majembe, magari, baiskeli na matoroli kwa maisha yao ya kila siku. Vijana wanapotengeneza vifaa hivyo hujipatia kipato. Hivyo, vyuo vya ufundi ni muhimu sana kwa jamii yetu.” Makini na Doto walivutiwa sana na makala ile baada ya kuisoma. Makini alitamani sana kuwa fundi magari na Doto alitamani sana kuwa seremala. Walitamani kujiunga na chuo cha ufundi kimojawapo. Wote walipenda masomo ya ufundi kwa sababu walitaka kujiajiri. FOR ONLINE USE ONLY 84 KISWAHILI_STD VII.indd 84 7/23/21 3:29 PM

P:92

FOR ONLINE USE ONLY Siku moja kabla ya kuhDitiOmuNDOaTrasDaUlaPSLIaCbaA,TmEwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Azimio alipata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi wa Darasa la Saba. Alisema, “Kesho mtaenda kufanya mitihani yenu ya kuhitimu Darasa la Saba. Mtaenda kuanza maisha mapya ya kuishi mtaani. Hivyo, mkatunze nidhamu zenu muishipo na jamii huku mkisubiri matokeo ya mitihani yenu. Kuna watakaofaulu na kuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari na kuna ambao hawatachaguliwa. Ninawashauri sana wale ambao hawatapata nafasi ya kujiunga na sekondari, muwaombe wazazi au walezi wenu wawapeleke katika vyuo vya ufundi. Huko mtajifunza fani mbalimbali ambazo zitawawezesha kumudu maisha yenu hapo baadaye.” Alipomaliza kusema hayo, aliwatakia mafanikio mema katika mitihani yao. Makini na Doto walitazamana huku wakitabasamu kwani walifurahi sana kusikia maneno hayo. Wanafunzi wote walifurahi sana na kumshukuru mwalimu mkuu kwa nasaha nzuri. Wote walitawanyika na kurudi nyumbani. Zoezi la kwanza: Ufahamu 1. Makini alipenda kufanya nini? 2. Makini alifanya nini kuona makala gazetini? 3. Makala iliyoandikwa gazetini ilihusu nini? 4. Vyuo vya ufundi ni nini? 5. Vijana wanaojiunga na vyuo vya ufundi hujifunza masomo kwa namna gani? 6. Vijana wanaofaulu kozi katika mafunzo kwenye vyuo vya ufundi hupewa nini? 7. Rafiki yake Makini alitamani kuwa nani? 8. Kwa nini Doto na Makini walipenda masomo ya ufundi? 9. Taja fani nyingine tano unazozifahamu zinazotolewa na vyuo vya ufundi. 10. Umejifunza nini kutokana na habari uliyoisoma? FOR ONLINE USE ONLY 85 KISWAHILI_STD VII.indd 85 7/23/21 3:29 PM

P:93

FOR ONLINE USE ONLY Zoezi la pili: MsamiatiDO NOT DUPLICATE Eleza maana za maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika habari, kisha yatungie sentensi. 1. makala 2. uchongaji 3. ufinyanzi 4. umakanika 5. ufumaji 6. hitimu 7. nadharia 8. kozi 9. nidhamu 10. shauri Zoezi la 3: Miundo Tunga sentensi mbili kwa kila muundo. 1. ………………… badala ya …..……………… Mfano: Nilinunua kalamu badala ya daftari. 2. ……………...…. kwa kuwa …….....………… Mfano: Juma alipotea njia kwa kuwa alikuwa mgeni kijijini. 3. ………………….. angali …………….....…… Mfano: Mtoto mkanye angali mdogo. 4. ………….....… kabla ya ……………………… Mfano: Kaka hunywa chai kabla ya kwenda shuleni. FOR ONLINE USE ONLY Zoezi la 4: Nahau na misemo Eleza maana za nahau na misemo ifuatayo: 1. tia akilini 6. piga msasa 2. tia nanga 7. kuonea gere 3. mguu kwa mguu 8. moyo mzito 4. pata kichwa 9. mkavu wa macho 5. teka akili 10. andika meza 86 KISWAHILI_STD VII.indd 86 7/23/21 3:29 PM

P:94

FOR ONLINE USE ONLY Zoezi la 5: MazoeziDyOa luNgOhaT DUPLICATE A. Andika umoja au wingi wa maneno yafuatayo: Umoja Wingi Mfano: mwanahewa wanahewa rubani marubani (i) mzigo _______________ (ii) _______________ watafiti FOR ONLINE(iii) _______________ abiria USE ONLY (iv) mwanamuziki _______________ (v) mshindi _______________ (vi) ________________ wapole (vii) _________________ mapera (viii) unywele ________________ (ix) _______________ mipira (x) mkoba _______________ B. Andika kinyume cha maneno yafuatayo: Neno Kinyume Mfano: mkubwa mdogo huzuni furaha (i) kufaulu ________________ (ii) kike ________________ (iii) mjomba ________________ (iv) mkakamavu ________________ (v) rejareja ________________ (vi) ficha _______________ (vii) sukuma ________________ (viii) sarafu _______________ (ix) nyeusi ________________ (x) Mashariki ________________ 87 KISWAHILI_STD VII.indd 87 7/23/21 3:29 PM

P:95

FOR ONLINE USE ONLY C. Badili sentensi zifuaDtaOzoNkOuwTaDkUatPikLaIChaAliTtEimilifu. Mfano: Watoto wanalilia baiskeli. Watoto wamelilia baiskeli. Bata wataogelea bwawani. Bata wameogelea bwawani. (i) Mama anapika chakula kingi. (ii) Wanafunzi wa Darasa la Saba waliotesha mahindi shambani. (iii) Ng’ombe atachinjwa leo jioni. (iv) Dada yangu alifaulu mitihani yake. (v) Mwalimu aliingia darasani kimyakimya. (vi) Mto unafurika wakati wa mvua. (vii) Bibi anapasua kuni. (viii) Busara alitoka kutibiwa hospitalini. (ix) Magoti atahudhuria kikao cha wazazi. (x) Shamba lote litapandwa vizuri. FOR ONLINE D. Kanusha sentensi zifuatazo:USE ONLY Mfano: Tunapenda kucheza mpira. Hatupendi kucheza mpira. Kaka amevaa kaptura ya shule. Kaka hajavaa kaptura ya shule. (i) Juma ameshinda mashindano ya riadha. (ii) Tunafundishwa somo la Kiingereza kila siku shuleni. (iii) Mariamu atanunua kitabu kizuri. (iv) Kaka yangu anavua samaki bwawani. (v) Nimewaona wanyama wengi mbugani. (vi) Mzava alifua shati lake. (vii) Shangazi anakula senene kwa wingi. (viii) Ameuza viatu vyake vya shule. (ix) Kizota anafuga kuku na mbuzi. (x) Meli imezama ziwani. 88 KISWAHILI_STD VII.indd 88 7/23/21 3:29 PM

P:96

FOR ONLINE USE ONLY E. Andika neno tofaDutOi nNa OmTenDgiUneP.LICATE Mfano: ndege, treni, basi, taa, pikipiki - taa bamia, biringanya, nyanyachungu, mkate, nyanya - mkate (i) dawati, kiti, meza, kigoda, stuli ____________ (ii) sahani, kijiko, kikombe, sufuria, bakuli ____________ (iii) gauni, suruali, kaptura, raba, shati ____________ (iv) wali, ugali, kande, nyama, ndizi ____________ (v) swala, tembo, kiboko, buibui, mbogo ____________ FOR ONLINE(vi) daftari, kalamu, penseli, mwanafunzi, karatasi ____________ USE ONLY (vii) matofali, bati, mchanga, sementi, kokoto ____________ (viii) mahindi, maharage, ngano, mchicha, mtama ____________ (ix) pua, masikio, macho, mikono, mdomo ____________ (x) rangi, chaki, penseli, karatasi, kalamu ____________ F. Panga herufi ili kupata maneno yenye maana. Mfano: raubo - ubora chemzo - mchezo (i) ekilezi ______________ (ii) shimpi ______________ (iii) guua ______________ (iv) mulimwa ______________ (v) atepo ______________ (vi) niuga ______________ (vii) gadaa ______________ (viii) liposi ______________ (ix) maliu ______________ (x) rihoda ______________ G. Nominisha vitenzi vifuatavyo: Mfano: lima – mlimaji/kilimo/mkulima/ukulima/ulimaji/mlimo panda – mpandaji/mpanzi/mpando/upandaji/upanzi (i) pamba ______________ (ii) cheza ______________ 89 KISWAHILI_STD VII.indd 89 7/23/21 3:29 PM

P:97

FOR ONLINE USE ONLY (iii) kata D_O__N__O_T__D__U_P__L_ICATE (iv) fua ______________ (v) pima ______________ (vi) uza ______________ (vii) imba ______________ (viii) chunga ______________ (ix) winda ______________ (x) vuta ______________ Zoezi la 6: Kazi ya kufanyaFOR ONLINE USE ONLY Chagua gazeti moja ulipendalo. Lisome, kisha baini maneno mapya. Eleza maana za maneno hayo na tunga sentensi kwa kila neno. Zoezi la 7: Utungaji Tunga hadithi fupi kutokana na gazeti ulilolisoma. Hadithi yako inaweza kuwa ya kiuchumi, kisiasa au kijamii. 90 KISWAHILI_STD VII.indd 90 7/23/21 3:29 PM

P:98

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Sura ya Kumi na Moja Barua ya kirafiki na rasmi Utangulizi Ulipokuwa Darasa la Sita, ulijifunza namna ya kujibu barua rasmi. Katika sura hii, utaendelea kuandika barua rasmi na za kirafiki kwa kufuata muundo wake pamoja na kueleza matumizi ya barua hizo. Vilevile, utajifunza namna ya kuzituma. Hii itakusaidia kuwa na ujuzi wa kuwasiliana kwa njia ya maandishi. FOR ONLINE USE ONLY Fikiri Sifa za barua za kirafiki na rasmi Ufahamu Soma habari hii, kisha jibu maswali yanayofuata. Kijiji cha Katale Mzee Mutayabwa alizaliwa kijijini Katale mkoani Kagera. Kwa miaka mingi, alikuwa anaishi mjini Tunduma mkoani Songwe. Mzee Mutayabwa alikuwa na watoto watatu, Kemilembe, Tumaini na Mulashani. Mulashani alikuwa anasoma Darasa la Sita. Mwaka jana, Mzee Mutayabwa pamoja na familia yake walirudi kuishi kijijini kwao. Alipofika, aliona mabadiliko mengi ya maendeleo kijijini. Hii ilitokana na wananchi kuhamasishana katika shughuli mbalimbali kama vile kilimo na uvuvi. Siku chache baada ya kuwasili kijijini, Mzee Mutayabwa aliuguliwa na mwanae Mulashani. Ilibidi ampeleke zahanati iliyoko kijiji cha jirani. Alitembea kilomita kumi hadi kufika ilipo zahanati hiyo. Alipata shida kubwa ya usafiri kutokana na barabara kuharibiwa na tetemeko la ardhi. Hali hiyo ilimfadhaisha sana. Baada ya Mulashani kupona, alimwandikia barua rafiki yake Lusajo kumweleza hali ya maisha ya kijijini kwao. Barua ilikuwa hivi: 91 KISWAHILI_STD VII.indd 91 7/23/21 3:29 PM

P:99

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Kijiji cha Katale, S.L.P. 210, Katale, Bukoba. 18/02/2017. FOR ONLINE Mpendwa rafiki yangu Lusajo, USE ONLY Ni matumaini yangu kuwa u mzima wa afya. Mimi pamoja na familia yangu hatujambo. Madhumuni ya barua hii ni kutaka kujua unavyoendelea na masomo yako na kukufahamisha ninavyoendelea hapa kijijini kwetu. Kwa sasa, sijambo ingawa niliugua hadi kupelekwa zahanati. Tulipata shida sana kufika zahanati kwa sababu ya ubovu wa barabara. Nimekukumbuka sana rafiki yangu. Dada yangu Kemilembe na kaka Tumaini wanakusalimu. Ninakutakia kila la heri katika masomo yako. Wasalimie wote wanaonifahamu. Rafiki yako, Mulashani Mutayabwa Baada ya kuandika barua hiyo, Mulashani aliikunja na kuiweka kwenye bahasha. Aliifunga na kuandika anwani juu ya bahasha hiyo, kisha akaibandika stempu na kuituma kwa njia ya posta. Familia ya Mzee Mutayabwa iliendelea kuishi kijijini na maisha yaliendelea kuwa magumu kutokana na changamoto ya miundombinu. Baada ya changamoto hiyo kudumu kwa muda mrefu, siku moja mwenyekiti wa kijiji aliitisha mkutano kijijini hapo na kuwataka wakazi wa kijiji hicho kueleza mambo yaliyowasibu. 92 KISWAHILI_STD VII.indd 92 7/23/21 3:29 PM

P:100

FOR ONLINE USE ONLY Wanakijiji walimiminika kaDmOa sNiaOfuTkuDhuUdPhuLrIiaCmAkTuEtano. Kila mkazi wa kijiji hicho alifika ili kujua hatima ya kero za muda mrefu zilizowakabili. Mwenyekiti alimruhusu kila mwanakijiji aeleze kero zake. Katika mkutano huo, Mzee Binamungu alisimama na kueleza kero walizozipata kutokana na tetemeko la ardhi kijijini hapo. Alieleza kuwa changamoto ya miundombinu waliyo nayo ni pamoja na barabara inavyohatarisha usalama wa wananchi na hata kusababisha vifo. Baada ya hapo, Mzee Mutayabwa naye alipata nafasi ya kuchangia mawazo. Alisisitiza kuwa wanakijiji washirikiane na kufanya juhudi katika kujenga barabara. Aliwakumbusha jinsi wenzao walivyopoteza maisha kwa kucheleweshwa kufikishwa zahanati. Wanakijiji waliunga mkono hoja hiyo. Baada ya kero zote kuwasilishwa, mwenyekiti aliwaeleza wanakijiji wake kwamba hayo yote yalikuwa yakiwapata kutokana na umaskini, ukosefu wa elimu na wataalamu mbalimbali. Mkutano uliendelea na mwafaka ulipatikana. Azimio la mkutano lilikuwa ni kujenga barabara. Wanakijiji waliunga mkono hoja ya mjumbe na walikubaliana kuchangia ujenzi wa barabara hizo. Wanakijiji waliwapendekeza vijana wawili hodari ambao watashirikiana bega kwa bega na kamati ya ujenzi kusimamia na kuhamasisha ujenzi wa barabara hizo. Vijana hao waliwaahidi wanakijiji kuwa watafanya juu chini kuhakikisha ujenzi wa barabara unakamilika. Mwenyekiti aliendelea kusisitiza kuwa kila kaya ishiriki ili kufanikisha zoezi hilo. Mwishoni mwa wiki, baada ya mkutano wa kijiji, Mzee Mutayabwa alipata nafasi ya kuwa ofisa mtendaji wa kijiji. Alimwandikia barua mwenyekiti wa kijiji kumtaarifu kwamba yuko tayari kushirikiana na wanakijiji katika ujenzi wa barabara. Barua ilisomeka hivi: FOR ONLINE USE ONLY 93 KISWAHILI_STD VII.indd 93 7/23/21 3:29 PM

P:101

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY DO NOT DUPLICATEKijiji cha Katale, S.L.P. 210, Bukoba. 20/04/2017. Kumb. Na. BUEND/KIT/05 Mwenyekiti wa Kijiji cha Katale, Kata ya Buendangabo, S.L.P. 30, Bukoba. Ndugu, YAH: KUSHIRIKI KATIKA UJENZI WA BARABARA Tafadhali husika na somo lililotajwa hapo juu. Kutokana na maazimio ya mkutano mkuu wa kijiji ya kujenga barabara, mimi Fidelis Mutayabwa, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Katale, ninakubali kushirikiana na wanakijiji wenzangu katika ujenzi wa barabara hadi kufanikisha zoezi hilo. Ninashukuru kwa ushirikiano. Wako katika maendeleo ya kijiji chetu, Fidelis Mutayabwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji Baada ya kuandika barua hiyo, Mzee Mutayabwa aliikunja na kuiweka kwenye bahasha, akaifunga na kuandika anwani juu yake. Aliipeleka kwa mkono kwa mwenyekiti. Mwenyekiti aliipokea na kuisoma barua hiyo. Aliwajulisha viongozi wenzake na kamati ya ujenzi juu ya barua ya Mzee Mutayabwa. Wote kwa pamoja walikubaliana na kuitisha mkutano wa dharura, ambapo waliwajulisha wanakijiji kushirikiana nao katika ujenzi wa barabara yao. Wanakijiji walifurahishwa sana na taarifa hizo na kuungana katika kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo. Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa barabara, mwenyekiti aliwashukuru wanakijiji wake. Alihimiza ushirikiano katika shughuli za maendeleo kijijini hapo uendelee. 94 KISWAHILI_STD VII.indd 94 7/23/21 3:29 PM

P:102

FOR ONLINE USE ONLY Zoezi la kwanza: UfDahOamNuOT DUPLICATE 1. Kijiji cha Katale kiko mkoa gani? 2. Mulashani alikuwa anasoma darasa la ngapi? 3. Wananchi wa kijiji hicho hujishughulisha na nini? 4. Kwa nini mwenyekiti alisisitiza wananchi waeleze kero zao? 5. Wananchi waliazimia nini kutokana na mkutano mkuu? 6. Wananchi walishiriki vipi katika ujenzi wa barabara? 7. Nini kilisababisha changamoto za miundombinu katika Kijiji cha Katale? 8. Kwa nini Mzee Mutayabwa alimwandikia mwenyekiti barua? 9. Wanakijiji wa Katale walifurahishwa na nini? 10. Umejifunza nini kutokana na habari uliyoisoma? FOR ONLINE USE ONLYZoezi la pili: Msamiati Tunga sentensi kwa kutumia maneno yafuatayo: 1. tetemeko 6. miundombinu 2. barua 7. hatima 3. bahasha 8. changia 4. stempu 9. kaya 5. posta 10. kamilika Zoezi la 3: Mazoezi ya lugha A. Chagua neno sahihi kutoka kwenye mabano ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi. Mfano: Wanafunzi _________ wamechelewa shuleni leo kwenye kipindi cha kwanza. (nane, wanane, tunane) Wanafunzi wanane wamechelewa shuleni leo kwenye kipindi cha kwanza. (i) Shamba la kijiji cha ushirika __________. (limeungua, liriungua, ririungua) (ii) Wanakijiji waliamua kujenga barabara ili ___________ usafiri. (kurahisisha, kulahisisha, kurahithisha) (iii) Barabara ilijengwa kwa muda mfupi kwa sababu wanakijiji _________. (walishilikiana, wanashilikiana, walishirikiana) (iv) Zamoyoni___________ hospitalini kwa uchunguzi zaidi. (amelazwa, amerazwa, atarazwa) 95 KISWAHILI_STD VII.indd 95 7/23/21 3:29 PM

P:103

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY (v) Tetemeko la ardDhiOlilisNaObaTbiDshUa P__L_I_C_A__T_E______ makubwa kijijini. (madhara, madhala, mazala) (vi) __________ ni kikwazo katika maendeleo ya jamii. (ukwasi,umaskini, utajiri) (vii) Adili ni mwalimu wa kilimo _________alipata taaluma hii kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine. (ambaye, ambae, ambayo) (viii) Mazao ___________ yamestawi vizuri. (yao, yawo, yayo) (ix) Mvua kubwa iliponyesha, ilisababisha ukuta ___________ kubomoka. (ule, wule, hule) (x) Maneno __________ yalitusisimua sana. (aliyoyasema, alioyasema, aliyesema) B. Andika KWELI kwa sentensi ya kweli na SI KWELI kwa sentensi isiyo ya kweli katika nafasi uliyopewa. (i) Barua rasmi ina anwani nne. ____________ (ii) Barua ya kirafiki ni lazima iwe na anwani ya mwandikiwa. ____________ (iii) Lazima kuweka kichwa cha barua kwenye barua rasmi. ____________ (iv) Barua rasmi kwa jina lingine huitwa barua za kiofisi. ____________ (v) Barua ya kirafiki hutumia lugha rasmi. ____________ (vi) Muundo wa uandishi wa barua ya kirafiki na barua rasmi ni tofauti. ____________ (vii) Barua rasmi huandikwa kwa marafiki na ndugu. ____________ (viii) Katika uandishi wa barua rasmi, anwani ya mwandikiwa ni lazima iwe upande wa kushoto. ____________ (ix) Barua rasmi huanza na salamu. ____________ (x) Kabla ya kuituma barua kwa njia ya posta, ni lazima kuiweka kwenye bahasha na kuibandika stempu. ____________ C. Andika sentensi zifuatazo katika wingi: (i) Shule yangu imefungwa; hivyo, sitakwenda shuleni. (ii) Kitabu changu kimechanika; nimeshindwa kufanya kazi yangu ya nyumbani. (iii) Mwanafunzi wa Darasa la Saba amefaulu mtihani wake vizuri. (iv) Ninajifunza lugha yangu ili niwe mahiri katika mawasiliano. (v) Kijana anajua kusoma na kuandika vizuri. (vi) Mtoto mtiifu na mwenye adabu hupendwa na mzazi wake. 96 KISWAHILI_STD VII.indd 96 7/23/21 3:29 PM

P:104

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY (vii) Yanipasa kusDoOmaNkOwaTbDidUii Pili LkuICfaAulTuEmtihani wangu. (viii) Mwanakijiji huyo alikuwa mkulima na mfugaji. (ix) Bwanashamba alimweleza mwanafunzi jinsi ya kulima mbogamboga. (x) Mwanafunzi aliyetoa hoja darasani alipongezwa kwa kupewa zawadi. D. Panga herufi zilizochanganywa ili kuunda neno sahihi. Mfano: bututhu - thubutu mawek - kamwe (i) milafia _____________ (ii) maheki _____________ (iii) bituka _____________ (iv) ndakela _____________ (v) njiakag _____________ (vi) uzugumi ____________ (vii) mamnya _____________ (viii) adasam _____________ (ix) uraba _____________ (x) adhiba _____________ E. Badili sentensi zifuatazo kutoka wakati uliopo kwenda wakati ujao. Mfano: Kinoge anathamini sana kazi. Kinoge atathamini sana kazi. (i) Vyakula aina ya wanga vinasaidia kujenga mwili. (ii) Mwalimu Mkumbukwa anatufundisha habari za mashujaa. (iii) Serikali inachukua hatua katika kulinda rasilimali za taifa. (iv) Gari linalopita kijijini kwao linakwenda Kilwa. (v) Wanafunzi wanakwenda kumwona mwenzao. (vi) Fikiri anasifiwa sana kwa hekima na juhudi katika mafunzo ya shuleni na nyumbani. (vii) Tunakumbuka Sikukuu ya Mashujaa. (viii) Lusato anazungumza lugha ya Kiswahili kwa ufasaha. (ix) Chivuma anasimama chini ya mchungwa akiwasubiri wenzake. (x) Mtoto analifunga dirisha linaloingiza hewa. 97 KISWAHILI_STD VII.indd 97 7/23/21 3:29 PM

P:105

FOR ONLINE USE ONLY F. Kanusha sentensi zDifuOatNazOoT: DUPLICATE Mfano: Sote tulisaidiana kufyeka nyasi kwenye kiwanja cha mpira wa pete. Sote hatukusaidiana kufyeka nyasi kwenye kiwanja cha mpira wa pete. (i) Mzee Mbagala na jamaa yake wana dhiki ya chakula. (ii) Mashine yetu inasaga magunia themanini ya mahindi kwa siku. (iii) Mtangazaji anatangaza kwa kipazasauti. (iv) Mwenyekiti alifafanua bajeti ya kijiji. (v) Ndizi zile zingekuwa mbivu, zingedondoka zenyewe. (vi) Mashindano ya nyimbo yalifanyika ndani ya jumba la makumbusho. (vii) Sadiki alikuwa mwanafunzi mwenye bidii darasani. (viii) Maziwa ya mtoto yamemwagika. (ix) Nitanunua viatu bei ikishuka. (x) Shangazi amepika chakula cha wageni. FOR ONLINE USE ONLYG. Andika visawe na vinyume vya maneno yafuatayo: Neno Kisawe Kinyume Mfano kiburi ujeuri/ukaidi unyenyekevu mwanga (i) zorota nuru/mwangaza giza (ii) kwanza (iii) lingana (iv) adimu (v) ugumu (vi) uwanda (vii) legevu (viii) amani (ix) adabu (x) omboleza H. Pigia mstari neno ambalo ni tofauti na mengine. Mfano: utulivu, upole, amani, vurugu, ukimya kamba, farasi, ugwe, ngamia, uzi (i) sifu, tukuza, heshimu, faharisha, kashifu (ii) penda, kubali, tamani, chukia, taka (iii) mchwa, panzi, kipepeo, jongoo (iv) kiongozi, mkuu, nahodha, mfuasi, mnyapara 98 KISWAHILI_STD VII.indd 98 7/23/21 3:29 PM

P:106

FOR ONLINE USE ONLY (v) ongea, zunguDmOzaN, nOyTamDaUzaP, LseICmAa,TloEnga (vi) lia, cheka, furahi, tabasamu, changamka (vii) uvivu, bidii, jitihada, juhudi, kasi (viii) nuna, kasirika, ghadhibika, chukia, tabasamu (ix) kata, pasua, tatua, unga, chana (x) nasa, kamata, nata, gwia, ng’atuka Zoezi la 4: Utungaji A. Kamilisha barua ifuatayo kwa kutumia maneno yaliyopo kwenye kisanduku. FOR ONLINE USE ONLYKikombo, kujifunza shughuli mbalimbali, Mpwapwa, Dodoma, Spika, Kikombo, Husika na somo lililotajwa hapo juu, Wanafunzi wa Darasa la Saba, 12/02/2020 (1) Shule ya Msingi ___________, S.L.P. 53, (2) ___________. (3) _________________. Kumb. Na. SM/KIKOM/MPW/013 Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, S.L.P. 941, (4) ____________. Ndugu, YAH: SHUKURANI YA ZIARA YA WANAFUNZI BUNGENI (5) _________________________. Wanafunzi wa shule ya msingi (6) ______________ tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa (7) _____ wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukubali ombi letu la kutembelea Bunge ili (8)______________. Tulijifunza mambo mengi na tulipata uelewa wa kutosha kuhusu shughuli za Bunge. Mwisho, tunawashukuru waheshimiwa wabunge wote kwa ushirikiano waliotuonesha wakati wote tulipokuwa huko. Wenu watiifu, (9)____________ Shule ya Msingi Kikombo 99 KISWAHILI_STD VII.indd 99 7/23/21 3:29 PM

P:107

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE B. Andika barua kwa shangazi yako kumjulisha kuwa utakwenda kumtembelea wakati wa likizo ya mwezi Juni. Zoezi la 5: Kazi ya kufanya Andika barua ya kikazi na barua ya kirafiki, kisha tengeneza bahasha. Andika anwani juu ya bahasha ili ziweze kutumwa kwa njia ya posta. Peleka barua zako posta iliyo karibu. FOR ONLINE USE ONLY 100 KISWAHILI_STD VII.indd 100 7/23/21 3:29 PM

P:108

FOR ONLINE USE ONLY SDuOraNyOaTKDuUmPLi InCaATMEbili Kadi za mialiko Utangulizi Katika sura hii, utajifunza maana na muundo wa kadi za mialiko. Pia, utajifunza mambo ya kuzingatia wakati wa kuandaa kadi za mialiko na matumizi yake. Hii itakusaidia kuwa mwandaaji mzuri wa kadi hizi na kutoa mafunzo ya uandaaji wa kadi za mwaliko kwa watu wengine. FOR ONLINE USE ONLY Fikiri Namna ulivyopata taarifa ya kuhudhuria sherehe yoyote Ufahamu Soma hadithi ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata. Marula yaleta furaha Ilikuwa siku ya Jumamosi yenye mawingu kiasi. Siku hiyo, kulikuwa na pilikapilika nyingi katika kijiji chetu cha Darini. Katika kijiji hiki, wanakijiji wote waliishi kwa furaha, amani na upendo. Wanakijiji wa Darini walikuwa na shauku ya sherehe ya mwaka. Shauku hii ilichochewa na maandalizi kabambe yaliyofanywa na kamati thabiti ya maandalizi ya sherehe hiyo. Kila mwanakijiji alipewa jukumu la kufanya ili kufanikisha maandalizi ya sherehe. Panya alipewa kazi ya kuhakikisha mazingira yote yanakuwa safi, tayari kwa sherehe. Alifagia, alifuta vumbi na kudeki ukumbi wote. Kiongozi wetu mkuu aitwaye Bundi alimteua Paka kuwa mkuu wa kamati ya vinywaji. Paka alihakikisha kila aina ya kinywaji inapatikana wakati wa sherehe. Aliandaa majokofu mengi kwa ajili ya kuhifadhia na kupozea vinywaji. 101 KISWAHILI_STD VII.indd 101 7/23/21 3:29 PM

P:109

FOR ONLINE USE ONLY Vilevile, Bundi alimteua MjuDsiOkuNwOa mTwDaUndPaLajIiCmAkuTuEwa vyakula vya sherehe. Mjusi alifurahia uteuzi wake na kumshukuru Bundi. Mjusi alishiriki kikamilifu kuandaa vyakula vitamu. Pamoja na kuandaa vyakula vitamu na vinono, Mjusi pia aliandaa matunda ya kila aina, akayapanga kwa ustadi mkubwa. Miongoni mwa matunda yaliyoandaliwa, yalikuwemo matunda yanayopendwa sana hapa kijijini kwetu yaitwayo marula. Kamati ya mapambo iliyokuwa chini ya uongozi wa Kipepeo iliupamba ukumbi kwa maua, nakshi na vito mbalimbali. Ukumbi ulipendeza na kuvutia mno. Ili kuhakikisha ulinzi, Bundi alimteua Siafu kuulinda ukumbi. Sisimizi naye, chini ya uongozi wa Popo, alipewa kazi ya kukaribisha wageni na kugawa chakula na vinywaji. Wanakamati wote walichapa kazi kwa ushirikiano mkubwa. Ilipotimu saa 1:00 usiku, wageni waalikwa walianza kumiminika ukumbini mithili ya siafu. Miongoni mwa wageni hao walikuwa Mbayuwayu, Njiwa na Nyoka. Bundi alisema, “Wageni wetu wamefika ukumbini kwa wakati.” Popo alisisitiza, “Kumbuka tuliandaa na kutoa kadi za mwaliko ambazo zilieleza kila kitu.” Popo aliendelea kusema kuwa alikaa akajadiliana na wanakamati wenzake, kisha wakaandaa kadi nzuri za mwaliko kwa ustadi mkubwa. Kadi hizo ziliandikwa kwa kuzingatia mambo muhimu katika uandishi wake. Mambo yaliyozingatiwa ni: jina la mwandishi na anwani yake, wadhifa wa mwalikwa, tarehe ya sherehe, lengo la sherehe, mahali sherehe inapofanyika, muda wa kuanza na kumalizika kwa sherehe na mawasiliano. “Karibu … karibu … karibu … Profesa Mbayuwayu!” Ilisikika sauti ya mwanakamati mmojawapo akimkaribisha mgeni ambaye aliwaonesha wanakamati hao kadi yake. Waliifungua kadi hiyo na kuisoma. FOR ONLINE USE ONLY 102 KISWAHILI_STD VII.indd 102 7/23/21 3:29 PM

P:110

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY Baada ya kuisoma na kujiridhisha na jina la mwalikwa kwenye kadi na kwenye orodha ya wageni, walimwonesha Profesa Mbayuwayu sehemu ya kuketi ukumbini. Kila aliyekuwapo ukumbini, aligawiwa vinywaji avipendavyo na kupatiwa chakula akitakacho. Cha ajabu waalikwa wote hawakupata furaha waliyoitazamia. Mjusi aliinua kichwa chake na kuwatazama wageni kwa huruma, kisha akatikisa kichwa chake juu chini. Akajisemea moyoni, “Marula yataleta furaha timilifu.” Aliwaamuru sisimizi wagawe matunda ya marula kwa kila mtu ukumbini. Kila mmoja wetu aliyafurahia sana matunda yale. Tuliyala kwa pupa. Ghafla, kila mmoja alijitupa ukumbini na kuanza kucheza kwa madaha. Washiriki wote tulitimua vumbi kwa mitindo mbalimbali ya uchezaji tukiwa tumechangamka sana. 103 KISWAHILI_STD VII.indd 103 7/23/21 3:29 PM

P:111

FOR ONLINE USE ONLY Ama kwa hakika, siku hiyoDOilikuNwOaTyaDkUukPuLmICbuAkTwEa daima. Mpaka leo, kila mmoja wetu katika Kijiji cha Darini huikumbuka siku hiyo. Hujivunia kuwa mjumbe wa kamati iliyofanikisha sherehe hiyo ya mwaka. Zoezi la kwanza: Ufahamu 1. Nani alikuwa kiongozi mkuu wa sherehe? 2. Paka alipewa jukumu gani katika sherehe hiyo? 3. Nani alishiriki kuandaa vyakula? 4. Ungekuwa mwalikwa wa sherehe hii, ungependelea kula nini? Kwa nini? 5. Unafikiri ni kwa nini Panya alipewa kazi ya kusimamia usafi? 6. Mbayuwayu alionesha nini mlangoni? 7. Unafikiri ni kwa nini wageni walifika ukumbini kwa wakati? 8. Popo aliandaa kadi za mwaliko kwa kuzingatia mambo gani? 9. Unafikiri ni wanyama gani wengine walipaswa kuhudhuria sherehe hii? Kwa nini? 10. Tunajifunza nini kutokana na hadithi hii? FOR ONLINE USE ONLYZoezi la pili: Msamiati Eleza maana za maneno yafuatayo, kisha tunga sentensi mbili kwa kila neno. 1. chochea 6. marula 2. kabambe 7. kadi 3. kamati 8. mwaliko 4. bundi 9. wadhifa 5. nono 10. timilifu Zoezi la 3: Mazoezi ya lugha A. Andika umoja wa sentensi zifuatazo: Mfano: Wageni walioalikwa walifika kwa wakati. Mgeni aliyealikwa alifika kwa wakati. (i) Wanyama walihudhuria sherehe ya kumaliza mwaka. (ii) Wanakamati walifanya kazi kwa bidii. (iii) Popo hawaoni vizuri mchana. (iv) Sisi tulipokea kadi za mialiko ya mahafali. (v) Waalikwa walifurahishwa na maandalizi ya sherehe. 104 KISWAHILI_STD VII.indd 104 7/23/21 3:29 PM

P:112

FOR ONLINE USE ONLY (vi) Walilipuka kwDaOfurNaOhaTbaDaUdaPyLaICkuAlaTEmatunda ya marula. (vii) Wanafunzi wanasoma kwa bidii ili wafanye vizuri katika mitihani yao. (viii) Kadi za mialiko ndizo zinazowapa watu idhini ya kuhudhuria kwenye sherehe. (ix) Vinywaji viliwatosha wageni. (x) Popo waliandaa kadi kwa rangi za kuvutia.   B. Andika KWELI au SI KWELI kwenye sentensi zifuatazo: (i) Kadi ya mwaliko huandikwa ili kumpa taarifa muhimu mwalikwa kuhusu sherehe.____________ (ii) Anwani ya mwandishi ni kitu muhimu katika kadi ya mwaliko. ____________ (iii) Tarehe ya shughuli ni kitu muhimu kwenye kadi ya mwaliko. __________ (iv) Si muhimu kuandika mawasiliano kwenye kadi za mialiko. __________ (v) Kadi za mialiko zinasaidia kujua idadi ya waalikwa.__________ (vi) Lengo la sherehe lazima lionekane kwenye kadi ya mwaliko. _________ (vii) Kadi za mialiko hutolewa kwa watu wote._________ (viii) Anwani ya mwandikiwa ni kitu cha msingi katika mawasiliano kwa waalikwa.________ (ix) Barua na kadi ya mwaliko zinafanana kwa kila kitu.__________ (x) Kadi ya mwaliko inakusaidia kufahamu muda wa kuanza na kumalizika kwa sherehe.___________ FOR ONLINE USE ONLY C. Andika visawe vya maneno yafuatayo: (i) darizi __________ (ii) mwaliko __________ (iii) sherehe __________ (iv) kinywaji __________ (v) chakula __________ (vi) kamili __________ (vii) changamka __________ (viii) kanuni __________   105 KISWAHILI_STD VII.indd 105 7/23/21 3:29 PM

P:113

FOR ONLINE USE ONLY D. Kamilisha fumbo lifDuaOtaNloOkTwaDkUuPtuLmICiaAmTaEelezo ya kwenda kulia na kwenda chini. 12 3 4 56 FOR ONLINE USE ONLY 7 Kwenda chini 1. Mtu aliyetembelea mahali fulani kwa mara ya kwanza (Herufi 5) 2. Karibisha watu kwenye tafrija (Herufi 5) 3. Kadi rasmi yenye picha na taarifa mbalimbali za mtu binafsi zinazombainisha na kumthibitisha yeye miongoni mwa watu wengine (Herufi 12) 6. Amrisho la kukwambia ugharimie kitu kwa kutoa fedha au mali (Herufi 5) Kwenda kulia 1. Taarifa anayopewa mtu kumtaka ahudhurie hafla fulani (Herufi 7) 4. Karatasi ngumu ambayo humtambulisha mtu aliyealikwa (Herufi 4) 5. Jumla ya vitendo vinavyomfanya mtu asitulie bila ya kazi (Herufi 8) 7. Tafrija inayoambatana na shamrashamra inayofanywa ili kuadhimisha tukio fulani la furaha (Herufi 7) 106 KISWAHILI_STD VII.indd 106 7/23/21 3:29 PM

P:114

FOR ONLINE USE ONLY E. Kamilisha jedwaliDlifOuaNtalOoTkwDaUkuPbLaIiCniAshTaEidadi ya silabi, konsonanti na irabu katika maneno yafuatayo: Na. Neno Silabi Konsonanti Irabu Mfano kofia 3 2 3 (i) themanini (ii) zambarau (iii) nta FOR ONLINE (iv) waliotukimbilia USE ONLY (v) chuchumaa (vi) aghalabu (vii) sisimizi (viii) konsonanti (ix) mzalendo (x) blanketi Zoezi la 4: Kazi ya kufanya Kusanya kadi za mialiko za hafla mbalimbali na mzijadili darasani. Zoezi la 5: Utungaji Shule yenu inatarajia kufanya sherehe ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la Saba. Andaa kadi ya mwaliko kwa wageni watakaoalikwa katika sherehe hiyo. 107 KISWAHILI_STD VII.indd 107 7/23/21 3:29 PM

P:115

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY SuDraOyNaOKTuDmUiPnLIaCTAaTtEu Insha Utangulizi Katika sura hii, utajifunza kuandika insha kuhusu uharibifu wa mazingira kwa kuzingatia mantiki na alama za uandishi. Utajijengea ujuzi wa kuandika insha kwa kufuata kanuni na taratibu za uandishi na kukufanya uwe mwandishi mzuri wa kazi mbalimbali. Fikiri Sifa za insha unazozifahamu Ufahamu Soma habari ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata. Uharibifu wa mazingira Matata ni mwalimu anayefundisha katika Shule ya Msingi Maendeleo iliyoko Wilaya ya Mjimkongwe. Anakaa katika Kitongoji cha Usafi kilicho umbali wa kilomita tano kutoka shuleni. Siku moja, Mwalimu Matata alikuwa anakwenda shuleni kwa kutumia pikipiki. Alipokuwa anapita pembezoni mwa msitu wa kijiji, aliwaona vijana watatu. Vijana hao walikuwa wakikata miti kwa kutumia mapanga na mashoka na kuirundika pembeni. Aliwatambua vijana hao kuwa ni Sadiki, Sikiri na Karumekenge. Mwalimu Matata alisikitika sana. Alisimamisha pikipiki yake haraka na kwenda katika eneo lile. Alianza kuwafokea vijana wale kwa kukata miti mingi kiasi kile. Vijana wale walimshangaa. Mwalimu Matata aliwahoji akitaka kujua sababu ya kukata miti. Karumekenge alimwambia kuwa wanakata ili wapate miti ya kuchongea vinyago. Mwalimu Matata aliwashangaa sana na aliwasihi waache kukata miti, kwani kufanya hivyo ni kuharibu mazingira. Aliwaelimisha kuhusu athari za uharibifu wa mazingira. Aliwaambia kuwa uharibifu wa mazingira husababisha athari nyingi kama vile ukosefu wa mvua na kuongezeka kwa joto duniani. Baada 108 KISWAHILI_STD VII.indd 108 7/23/21 3:29 PM

P:116

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYya elimu hiyo, vijana waleDwOalimNwOahTidDi kUutPokLaItCa mAiTti Eovyo. Walisema, “Hatutakata tena miti ovyo. Tutakuwa mabalozi wa mazingira kijijini kwetu.” Baada ya kusema maneno hayo, vijana hao walichukua mapanga na mashoka yao na kurejea nyumbani kwao. Mwalimu Matata aliondoka kuelekea shuleni ingawa alikuwa amechelewa kazini. Alipofika shuleni, alikwenda moja kwa moja hadi kwenye ofisi ya mwalimu mkuu. Alimkuta ofisini akiwa anasaini kwenye kitabu cha mahudhurio. Alimweleza sababu iliyomchelewesha kazini. Mwalimu Mkuu alimpongeza sana kwa kile alichokifanya. Mwalimu Matata aliingia darasani kufundisha uandishi wa insha kuhusu uharibifu wa mazingira. Wanafunzi walikuwa na shauku juu ya mada hiyo. Aliwauliza wanafunzi mambo muhimu ya kuzingatia katika uandishi wa insha yoyote ile. Wanafunzi walijibu kuwa insha yoyote huwa na vipengele vinne ambavyo ni kichwa cha insha, utangulizi, kiini na hitimisho. Mwalimu Matata alifurahishwa sana na majibu ya wanafunzi, kisha aliwaongoza kuandika insha kuhusu uharibifu wa mazingira. Insha iliyoandikwa ilisomeka hivi: UHARIBIFU WA MAZINGIRA Mazingira ni jumla ya mambo yote yanayomzunguka kiumbe katika maisha yake. Vitu hivyo vinaweza kuwa vyenye uhai kama vile wanyama, wadudu na mimea au visivyo na uhai kama vile milima, maziwa, mabonde, mito na bahari. Uharibifu wa mazingira ni uzoroteshaji wa mazingira kwa njia ya kupunguza rasilimali kama vile hewa, maji, mimea, udongo na hata kupotea kwa wanyamapori. Mara nyingi, uharibifu wa mazingira husababishwa na vitendo vya binadamu kuangamiza viumbe vinavyomzunguka. Vitendo hivyo ni kama vile kukata miti ovyo, kulima kandokando ya vyanzo vya maji, kutupa taka ovyo na kutiririsha maji machafu kwenye vyanzo vya maji. Uharibifu wa mazingira hutokana na shughuli mbalimbali za binadamu kama vile kilimo. Binadamu hupanua mashamba kwa ajili ya shughuli za kilimo kwa kukata miti ovyo na kuchoma misitu. Ukataji wa miti ovyo na uchomaji wa misitu husababisha vifo vya viumbe hai vinavyoishi katika miti hiyo kama vile nyani, tumbili na sokwe. 109 KISWAHILI_STD VII.indd 109 7/23/21 3:29 PM

P:117

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY Utupaji wa taka huwezaDkOuhNarOibTu DmUazPinLgIiCraA. TTEaka hizo hutoa harufu mbaya na kuvutia wadudu kama vile nzi. Wadudu hao husababisha magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindupindu. Viwanda kutiririsha maji machafu kwenye vyanzo vya maji ni sababu nyingine ya uharibifu wa mazingira. Maji yanayotiririshwa huchafua maji yanayotumiwa na binadamu kutoka kwenye mito na maziwa hivyo, kusababisha magonjwa kwa binadamu kama vile kansa. Viwanda pia hutoa moshi ambao huchafua hewa. Watu wanapovuta hewa chafu, huathirika. Ongezeko la joto duniani ni mojawapo ya matokeo ya uharibifu wa mazingira. Ongezeko hilo husababisha ukame. Ukame nao husababisha kukauka kwa mazao ya chakula. Hali hii husababisha njaa. Milipuko ya magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindupindu na yasiyo ya kuambukiza kama vile kansa ni athari nyingine ya uharibifu wa mazingira. Magonjwa hayo yanaweza kusababishwa na maji machafu ya viwandani ambayo hutiririshwa kwenye vyanzo vya maji kama vile mito na maziwa. Kwa hiyo, hatuna budi kutunza mazingira ili nayo yatutunze. Jamii inatakiwa kuelimishwa kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira. Serikali na jamii kwa ujumla tunatakiwa kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya waharibifu wa mazingira ili kunusuru vizazi vilivyopo na vijavyo. Baada ya kuandika insha hiyo, Mwalimu Matata aliwaongoza wanafunzi kuisoma kwa sauti, kisha akawauliza, “Insha ina vipengele gani?” Mwanafunzi aitwaye Mashauri alijibu kwa kutaja vipengele vinavyounda insha. Alisema kuwa insha yoyote huwa na kichwa, utangulizi, kiini na hitimisho. Alifafanua, “Kichwa cha insha iliyosomwa ni Uharibifu wa mazingira, utangulizi ni maana ya mazingira na kiini ni sababu na athari za uharibifu wa mazingira. Hitimisho ni hatua za kuchukua ili kuepusha uharibifu wa mazingira.” Mwalimu Matata alimpongeza Mashauri kwa kujibu swali vizuri. Mwishowe, Mwalimu Matata aliwapa wanafunzi kazi ya kuandika insha kuhusu utupaji wa taka ovyo. Wanafunzi waliandika insha nzuri sana. Mwalimu alisahihisha insha hizo. Insha nzuri zaidi zilisomwa darasani. Wanafunzi walimshukuru mwalimu wao kwa kuwapa elimu ya utunzaji wa mazingira. 110 KISWAHILI_STD VII.indd 110 7/23/21 3:29 PM

P:118

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Zoezi la kwanza: Ufahamu 1. Matata ni mwalimu wa shule gani? 2. Mwalimu Matata alikuwa anakwenda shuleni kwa kutumia usafiri gani? 3. Mwalimu Matata aliona nini alipokuwa anapita pembezoni mwa msitu wa kijiji? 4. Sadiki, Sikiri na Karumekenge walikuwa wanafanya nini msituni? 5. Ukataji wa miti ovyo husababisha nini? 6. Kwa nini tunashauriwa kutokata miti ovyo? 7. Je, uandishi wa insha unazingatia vipengele gani? 8. Taja shughuli zinazosababisha uharibifu wa mazingira. 9. Je, ukikuta watu wanaharibu mazingira utafanya nini? 10. Umejifunza nini kutokana na habari uliyoisoma? Zoezi la pili: Msamiati FOR ONLINE USE ONLY Tumia maneno uliyopewa, kutunga sentensi mbili kwa kila neno. Mfano: rundika Baba alirundika uchafu sehemu moja ili auchome. Wanafunzi wamerundika viti ndani ya darasa. 1. rundika 6. tiririsha 2. kinyago 7. harufu 3. athari 8. kansa 4. uharibifu 9. ambukiza 5. taka 10. nusuru Zoezi la 3: Miundo Tunga sentensi mbili kwa kila muundo. 1. …………… sababu ya ………… Mfano: Mwalimu alitaka kujua sababu ya wanafunzi kuchelewa shuleni. 2. ……………... __enda ………………… Mfano: Unaruhusiwa kwenda kumwona mgonjwa wako. 3. …………... hivyo ………………… Mfano: Vinanda hivyo vilipigwa kwa ustadi mkubwa. 111 KISWAHILI_STD VII.indd 111 7/23/21 3:29 PM

P:119

FOR ONLINE USE ONLY 4. …………... kuwa ……D…O…N…O..T. DUPLICATE Mfano: Wanafunzi walisema kuwa watakuwa kidato cha kwanza mwaka kesho. 5. …………... alipofika …………… Mfano: Mwalimu alipofika, wanafunzi walianza kujisomea. Zoezi la 4: Mazoezi ya lugha A. Andika sentensi zifuatazo katika wingi. Mfano: Babu yangu anafanya biashara. Babu zetu wanafanya biashara. FOR ONLINE USE ONLY(i) Mkulima anapalilia bustani ya nyanya. (ii) Mbunge ametembelea mgodi wa mwekezaji. (iii) Mkono mtupu haulambwi. (iv) Mwanafunzi anafagia ofisi ya mwalimu mkuu. (v) Mtoto wa shangazi yangu hapendi kiazi. (vi) Mjasiriamali hufanya kazi kwa bidii. (vii) Garimoshi linasafirisha kontena la chakula. (viii) Mzazi amemnunulia mtoto wake kitabu kipya. (ix) Mfadhili amejenga choo cha shule kwa gharama nafuu. (x) Mwanafunzi ametunga shairi la kisasa. B. Andika KWELI au SI KWELI katika sentensi zifuatazo: (i) Muundo wa insha hufanana na muundo wa barua rasmi. ____________ (ii) Insha huandikwa kwa kuzingatia alama za uandishi. ____________ (iii) Uandishi wa insha humfikirisha mwandishi. ____________ (iv) Katika utangulizi, mwandishi wa insha huandika kwa kirefu kile anachotaka kukielezea. ____________ (v) Insha zilizoandikwa vizuri huchukiza wasomaji. ____________ (vi) Insha huandikwa kwa kufuata au bila kufuata mpangilio wa mawazo. ____________ (vii) Mawazo katika insha huandikwa katika aya. ____________ (viii) Kichwa cha insha huandikwa kwa maneno mengi. ____________ (ix) Katika kiini, mwandishi wa insha huelezea kwa undani jambo analoliandikia. ___________ (x) Uandishi wa insha haumpi mwandishi uhuru wa kujieleza kwa maandishi. ____________ 112 KISWAHILI_STD VII.indd 112 7/23/21 3:29 PM

P:120

FOR ONLINE USE ONLY C. Badili sentensi ziDfuOataNzOo kTuDwUa kPaLtiIkCaAkTaEuli taarifa. Mfano: “Dada yangu ni mrefu,” mtoto alisema. Mtoto alisema kwamba dada yake ni mrefu. Alisema, “Tutakuwa wachezaji bora wa dunia.” Alisema kwamba watakuwa wachezaji bora wa dunia. (i) “Simu zetu zimevunjika vioo,” wazazi walisema. (ii) “Nitakuwa safarini kesho kuelekea Mwanza,” abiria mmoja alisema. (iii) Mbunge alisema, “Uchumi wa viwanda huchochea ukuaji wa pato la taifa.” (iv) “Kwa nini hamna utamaduni wa kujisomea vitabu?” Mwalimu FOR ONLINE USE ONLY aliuliza. (v) “Nitasoma kwa bidii ili nifaulu mitihani yangu,” mtoto alimwambia mzazi wake. (vi) “Dereva aliendesha gari bila uangalifu ndiyo maana tumepata ajali,” abiria aliwaambia askari. (vii) “Mnakimbia kwenda wapi?” Kiranja aliwauliza wanafunzi wenzake. (viii) “Saratani ni ugonjwa hatari sana,” daktari aliwaambia wananchi. (ix) “Ni bora kuraruka nguo kuliko kuraruka akili,” mwalimu aliwaeleza wanafunzi. (x) Muuzaji aliwaambia wanunuzi, “Redio hizi zinauzwa kwa bei ghali sana.” D. Andika sentensi zifuatazo katika wakati ujao. Mfano: Baba alikata tawi la mti kwa kutumia panga. Baba atakata tawi la mti kwa kutumia panga. Bahati alinunua gazeti lenye makala ya biashara na uchumi. Bahati atanunua gazeti lenye makala ya biashara na uchumi. (i) Mwanafunzi amekunywa maji safi. (ii) Shangazi alisafiri kwa basi kuelekea Ruvuma. (iii) Wawekezaji wanajenga hoteli ya kisasa. (iv) Wanamuziki wameburudisha wananchi kwenye sherehe za uhuru. (v) Mwalimu alitunga kisamafunzo kizuri sana. (vi) Wanafunzi wameigiza mbele ya wanafunzi wenzao darasani. (vii) Wanakijiji walichangia ujenzi wa soko la kijiji. (viii) Vijana walikwenda kurina asali mwituni. (ix) Mimi nimetunga mashairi ya kimapokeo na ya kisasa. (x) Wanajeshi walijenga daraja ili kupitisha vifaa vya kijeshi. 113 KISWAHILI_STD VII.indd 113 7/23/21 3:29 PM

P:121

FOR ONLINE USE ONLY E. Kanusha sentensi zDifuOatNazOoT: DUPLICATE Mfano: Yeye alifinyanga mitungi ya kuuza. Yeye hakufinyanga mitungi ya kuuza. Bahati amekokotoa mlinganyo vizuri. Bahati hajakokotoa mlinganyo vizuri. (i) Shule yetu imenunua kompyuta mpya. (ii) Seremala atatengeneza samani za shule. (iii) Mafuriko yameleta maafa kijijini kwetu. (iv) Swali hili linajibika kwa urahisi. (v) Mjomba ananunua cherehani dukani. (vi) Wanajeshi walilipua ndege ikiwa angani. (vii) Wakulima wanapata hasara. (viii) Fundi ametengeneza gari la shule kwa ustadi mkubwa. (ix) Mwenyekiti wa kijiji anakubalika kwa wanakijiji wenzake. (x) Babu ameuza mahindi sokoni leo. FOR ONLINE USE ONLY F. Jaza chemshabongo ifuatayo kwa kuandika herufi moja tu kwa kila kisanduku. Zingatia maelekezo ya kwenda chini na kulia. 1 2P W 3E 4 5K 6E 7 8 114 KISWAHILI_STD VII.indd 114 7/23/21 3:29 PM

P:122

FOR ONLINE USE ONLY Kwenda chini DO NOT DUPLICATE Mfano: 2. Kuwa pekee bila ya mwingine. (herufi 5) - PWEKE 1. Kipindi cha mabadiliko ambacho mtu au jamii hutoka kuingia kwenye kipindi cha utaratibu tofauti. (herufi 5) 4. Kitendo cha kuweka mbegu au mche katika ardhi ili ukue. (herufi 5) 7. Makundi mbalimbali ya vitu au jambo fulani. (herufi 4) Kwenda kulia 2. Mahali penye miti mingi, vichaka na nyasi. (herufi 4) 3. Neno lenye maana ya kuepuka pigo au jambo la hatari. (herufi 3) 5. Kitendo cha mtu kuwa na hamu au haja ya kupata kitu fulani. (herufi 4) 6. Kitendo cha kusambaa au kuwa kila mahali. (herufi 4) 8. Mahali pa kutupia taka. (herufi 3) Zoezi la 5: Utungaji Andika insha yenye maneno yasiyopungua mia moja na hamsini (150) na yasiyozidi mia mbili (200) kuhusu uharibifu wa mazingira. FOR ONLINE USE ONLY 115 KISWAHILI_STD VII.indd 115 7/23/21 3:29 PM

P:123

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY SuDraOyNaOKTuDmUPi nLIaCANTnEe Hotuba Utangulizi Katika sura hii, utajifunza kusikiliza na kusoma hotuba pamoja na kufafanua maudhui yaliyomo. Maarifa utakayoyapata yatakusaidia kukuza uwezo wa kujieleza kwa kujiamini na kujenga hoja kwa kuzingatia miktadha mbalimbali. Fikiri Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa hotuba Ufahamu Soma habari ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata. Mkuu wa wilaya ahutubia wanakijiji Kijiji cha Majengo kipo katika Wilaya ya Mapambano. Kijiji hicho kilikuwa nyuma kimaendeleo kutokana na mwamko mdogo wa wanakijiji kushiriki katika shughuli za maendeleo. Licha ya kuwa na wakazi wengi, kijiji hicho hakikuwa na maji wala umeme. Shughuli nyingi za kijamii zilisuasua, kwa hiyo wanakijiji walikosa huduma nyingi. Katika harakati za kukikwamua kijiji katika hali ile, Mkuu wa Wilaya ya Mapambano aliamua kumwandikia barua Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Majengo akimwagiza kuitisha mkutano wa wanakijiji wote. Lengo lake lilikuwa kuhamasisha wanakijiji kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo kama vile uchimbaji wa visima. Alipanga mkutano huo ufanyike siku ya Jumanne ya wiki iliyofuata. Pia, alimwagiza Mtendaji wa Kijiji kumwalika Mheshimiwa Diwani, Ofisa Mtendaji wa Kata, Mwenyekiti wa Kijiji, wenyeviti wa vitongoji pamoja na Meneja wa Shirika la Umeme na Mhandisi wa Maji wa Wilaya. Mtendaji wa Kijiji alifanya kama alivyoagizwa na Mkuu wa Wilaya. 116 KISWAHILI_STD VII.indd 116 7/23/21 3:29 PM

P:124

FOR ONLINE USE ONLY Mkuu wa Wilaya aliandaDaOhoNtuObaTkDwUa aPjiLliIyCaAkuTwEahutubia wanakijiji. Siku ya mkutano ilipofika, Mkuu wa Wilaya alianza safari kuelekea Kijiji cha Majengo. Aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya, Meneja wa Shirika la Umeme na Mhandisi wa Maji wa Wilaya. Walipofika eneo la mkutano, walikuta umati mkubwa wa wanakijiji ukiwa unawasubiri. Mkuu wa Wilaya alifurahishwa na kitendo cha wanakijiji kuitikia wito. Walipokelewa na viongozi wa kijiji pamoja na Mheshimiwa Diwani. Mkuu wa Wilaya aliwasalimu wanakijiji na viongozi wao kwa bashasha. Alioneshwa mahali pa kuketi. Aliketi huku akiwa na hamu kubwa ya kuwahutubia wanakijiji. Baada ya muda mfupi, viongozi walitambulishwa kwa kuzingatia itifaki. Mtendaji wa Kijiji aliwatambulisha wenyeviti wa vitongoji na Mwenyekiti wa Kijiji. Baadaye, alimkaribisha Mtendaji wa Kata ambaye alijitambulisha na akamtambulisha Mheshimiwa Diwani. Hatimaye, Mheshimiwa Diwani alimkaribisha Mkurugenzi wa Wilaya ili awatambulishe viongozi walioambatana na Mkuu wa Wilaya katika msafara wake. FOR ONLINE USE ONLY 117 KISWAHILI_STD VII.indd 117 7/23/21 3:29 PM

P:125

FOR ONLINE USE ONLY Baada ya utambulisho, MkDuOu wNaOWTilaDyUa PalLisIiCmAamTaEkuwahutubia wanakijiji. Hotuba yake ilikuwa hivi: HOTUBA YA MKUU WA WILAYA YA MAPAMBANO KWA WANAKIJIJI Majengo oyeee! WA MAJENGO Ndugu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya, Mhandisi wa Maji, Meneja wa Shirika la Umeme, Mheshimiwa Diwani, Ofisa Mtendaji wa Kata, Mwenyekiti wa Kijiji, Ofisa Mtendaji wa Kijiji, wenyeviti wa vitongoji, ndugu wananchi, FOR ONLINE USE ONLYmabibi na mabwana, habari zenu? Ndugu wananchi, ninapenda kutumia fursa hii kuwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huu siku ya leo. Asanteni sana! Ndugu wananchi, sote tunajua kuwa maji na umeme ni vitu muhimu sana katika maisha ya binadamu. Pia, ni kitovu cha maendeleo katika jamii yoyote ile kwa sababu husaidia katika shughuli mbalimbali. Ili kupata maendeleo, tunahitaji kuwa na huduma zote za msingi, zikiwamo za maji na umeme. Tunatambua kuwa kijiji chetu hakina huduma hizi. Kwa kulitambua hilo, nimeona nije na wataalamu ambao wanaweza kutushauri namna ya kufanya ili tuweze kupata huduma hizi kijijini kwetu. Ndugu wananchi, miongoni mwa matatizo yanayotukabili katika wilaya yetu ni suala la upatikanaji wa maji. Maji ambayo watu wengi wanayatumia si safi wala salama. Lengo letu ni kuhakikisha watu wote wanapata maji safi na salama. Hili ni lengo la muda mrefu. Lengo la muda mfupi ni kuhakikisha kuwa watu wanapata maji ya kutumia. Hapa ndipo ninawaomba mshiriki katika kuchimba visima. Mhandisi wa Maji atawaelekeza utaratibu utavyokuwa. Ninaomba nisisitize jambo moja, maji ya visima ni lazima myachemshe kabla ya kuyatumia kwa kunywa. Kwa namna hii, hamtakuwa mnaweka afya zenu hatarini. Visima vitasaidia kupunguza umbali tunaotembea kutafuta maji. Ndugu wananchi, nimekuja pia na Meneja wa Shirika la Umeme ambaye amenihakikishia kwamba tayari kuna mkakati wa kuleta umeme wa wakala wa nishati vijijini. Ninadhani mmeshaona nguzo zilizofikishwa tayari kijijini 118 KISWAHILI_STD VII.indd 118 7/23/21 3:29 PM

P:126

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY hapa. Ninawaomba tujDitaOhidNi kOuTchDanUgPiaLilIiCtuAwTezEe kuunganishiwa umeme. Hii itatusaidia kuondokana na matumizi ya vibatari. Umeme pia utasaidia kuharakisha maendeleo. Ndugu wananchi, baada ya kuzungumza haya, kwa mara nyingine, ninawashukuru sana kwa mahudhurio yenu mazuri katika mkutano huu. Pia, niwatakie afya njema na kila la heri katika kutekeleza majukumu yenu ya kila siku. Majengo oyeee! Asanteni kwa kunisikiliza. Baada ya hotuba, wanakijiji walipewa fursa ya kuuliza maswali. Waliuliza maswali mbalimbali pamoja na kutoa hoja zao walizokuwa nazo. Pia, walimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwatembelea na kuwahamasisha kushiriki shughuli za maendeleo ya kijiji chao. Waliahidi kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa. Mkuu wa Wilaya aliwaaga wanakijiji pamoja na viongozi wa kijiji na kuondoka. Alirejea ofisini kwake kuendelea na majukumu mengine. Baadaye, Diwani aliongoza kikao kifupi kati ya viongozi wa kijiji na wanakijiji kujadili hotuba ya Mkuu wa Wilaya. Katika mjadala huo, walichambua na kufafanua maudhui yake. Walikubaliana kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo. Waliweka mkakati wa kuchimba visima. Walianza kuchangia fedha na nguvukazi. Baada ya miezi sita, walifanikiwa kukamilisha uchimbaji na ujenzi wa visima vitano vya maji kijijini. Ama kweli, hotuba ya Mkuu wa Wilaya iliwazindua wanakijiji. Sasa, wanapata maji safi na salama. Pia, wana umeme ambao wanautumia katika shughuli mbalimbali za kiuchumi. Zoezi la kwanza: Ufahamu 1. Kijiji cha Majengo kipo katika wilaya gani? 2. Kwa nini Kijiji cha Majengo kilikuwa nyuma kimaendeleo? 3. Nani alimwandikia barua Mtendaji wa Kijiji akimwagiza kuitisha mkutano wa wanakijiji? 4. Lengo la Mkuu wa Wilaya kuitisha mkutano wa wanakijiji lilikuwa nini? 5. Hotuba aliyoiandika Mkuu wa Wilaya ilikuwa na vipengele vingapi? Taja vipengele hivyo. 6. Mkuu wa Wilaya aliambatana na viongozi gani? 7. Nani alimtambulisha Mkuu wa Wilaya kwa wanakijiji? 8. Diwani alifanya nini baada ya Mkuu wa Wilaya kuondoka? 9. Mkakati gani wa utekelezaji uliwekwa na wanakijiji? 10. Umejifunza nini kutokana na habari uliyoisoma? 119 KISWAHILI_STD VII.indd 119 7/23/21 3:29 PM

P:127

FOR ONLINE USE ONLY Zoezi la pili: MsamiatiDO NOT DUPLICATE Tumia maneno uliyopewa kutunga sentensi moja kwa kila neno. Mfano: Kijiji chetu kina mwamko mkubwa katika shughuli za maendeleo. 1. mwamko 7. hatarini 2. suasua 8. mkakati 3. lengo 9. jukumu 4. hotuba 10. chambua 5. bashasha 11. maudhui FOR ONLINE6. itifaki 12. zindua USE ONLY Zoezi la 3: Methali Kamilisha methali zifuatazo: Mfano: Mwenda bure si mkaa bure, …………… Mwenda bure si mkaa bure, huenda akaokota. …………… imo miguuni mwake. Riziki ya mwanadamu imo miguuni mwake. 1. Kitanda usichokilalia …………………………………………… 2. …………………………………………… hakisimamishi jengo. 3. …………………………………………… kwa msala upitao. 4. Mtumikie kafiri ...…………………………………………… 5. …………………………………………… na uzazi ungalipo. 6. Mwamba ngoma …………………………………………… 7. …………………………………………… mauti humuumbua. 8. …………………………………………… ila mzaliwa nawe. 9. …………………………………………… hutanda na kuyeyuka. 10. Ng’ombe haelemewi …………………………………………… Zoezi la 4: Mazoezi ya lugha A. Tunga sentensi tano (5) zilizo sahihi kutokana na jedwali lifuatalo: Anapenda kucheza mpira wa miguu na mpira wa wavu Babu ni mfupi lakini mama ni mrefu Hakuandika ingawa alikuwa na kalamu Tunapenda kusoma kimya kwa sauti Kiswahili Kiingereza ni masomo ya lugha 120 KISWAHILI_STD VII.indd 120 7/23/21 3:29 PM

P:128

FOR ONLINE USE ONLY B. Andika KWELI auDSOI KNWOETLIDkUatPikLaIsCeAntTeEnsi zifuatazo: (i) Hotuba huandikwa kwa lugha rahisi ili kumfanya msomaji asielewe kilichomo. ____________ (ii) Kichwa cha hotuba mara nyingi huandikwa kwa herufi kubwa. ____________ (iii) Uchambuzi wa maudhui ya hotuba hudumaza akili za msomaji. ____________ (iv) Mwandishi wa hotuba hana budi kuwapuuza wasomaji wake. ____________ (v) Maudhui ya hotuba ni yale mawazo yaliyomo katika hotuba. ____________ (vi) Uandishi wa hotuba huzingatia vipengele vitatu. ____________ (vii) Mawazo katika hotuba huandikwa kwa mpangilio. ____________ (viii) Hotuba inapaswa kuandikwa kwa kuzingatia alama za uandishi kwa kiasi fulani. ____________ (ix) Vipengele vya muundo wa hotuba ni sawa na vya muundo wa risala. ____________ (x) Hotuba hutolewa na mtu maalumu. ____________ FOR ONLINE USE ONLY C. Unda vitenzi kutokana na nomino zifuatazo: Mfano: upishi - pika ucheshi - cheka (i) ziara (ii) dhuluma (iii) uchafu (iv) kashifa (v) usafi (vi) hotuba (vii) wizi (viii) utangulizi (ix) amri (x) mchemsho 121 KISWAHILI_STD VII.indd 121 7/23/21 3:29 PM

P:129

FOR ONLINE USE ONLY K R D. Zungushia herufi iliDkOuunNdOaTmDanUePnoLIsCaAhiThEi. I I S S HO T UB A A A ON I BAK E S MGM I A I P I AEAADB U B CH Z M D H A A O AAUNP I W G MB I L I J E A BUREKO T E UZ I OAH AD LM J O D U ABMA FOR ONLINE USE ONLYE. Badili vitenzi vifuatavyo kuwa katika kauli ya kutendeka. Mfano: lima - limika osha - osheka (i) fundisha (vi) shona (ii) soma (vii) kubali (iii) lipa (viii) endesha (iv) pika (ix) tosha (v) danganya (x) nunua Zoezi la 5: Utungaji Fikiria wewe ni mwanafunzi uliyechaguliwa kuwa kiranja mkuu shuleni kwenu. Andika hotuba ya kuwashukuru wanafunzi wenzako kwa kukuchagua. 122 KISWAHILI_STD VII.indd 122 7/23/21 3:29 PM

P:130

FOR ONLINE USE ONLY SDuOraNyOaTKDuUmPLi InCaATTEano Ufupisho Utangulizi Ulipokuwa Darasa la Sita, ulijifunza kufupisha hadithi bila kupotosha maana. Katika sura hii, utasoma habari na kuifupisha. Pia, utafafanua mafunzo yatokanayo na habari uliyoisoma. FOR ONLINE USE ONLY Fikiri Mambo utakayozingatia wakati unaandika ufupisho Ufahamu Soma habari hii, kisha jibu maswali yanayofuata. Viatu vya Babu Lukoma, Mkomi na Bashiku wanaishi Kijiji cha Mkombozi. Vijana hawa waliamua kufanya kazi kwa ushirikiano, japo walitoka familia tofauti. Ulikuwa msimu wa mvua, watu wote kijijini hawakubweteka. Kila mmoja alishiriki katika shughuli za kilimo. Vijana hawa walifanya kazi za shamba kwa umoja. Siku moja alfajiri, waliondoka nyumbani kuelekea shambani. Kila mmoja alibeba aina kadhaa za mbegu kwa ajili ya kupanda. Njiani, walikutana na watu wakienda kwenye mashamba yao. Watu hao walikuwa wamebeba majembe na mapanga. Mnamo majira ya saa kumi na moja alfajiri, vijana hawa waliwasili shambani. Baada ya muda mfupi, wasaidizi wao waliwasili shambani hapo. Shughuli ya upanzi ilianza. Baadhi ya wasaidizi waliweka mbolea kila shimo. Wengine walikagua uwapo wa mbegu kwa kila shimo. Walipanda maharage ekari moja. Sehemu nyingine walipanda karanga. Ilipofika saa tano na nusu asubuhi, waliahirisha shughuli za upanzi na kurejea nyumbani. 123 KISWAHILI_STD VII.indd 123 7/23/21 3:29 PM

P:131

FOR ONLINE USE ONLY Wakiwa njiani kurudi nyumDbOanNi, OwTaliwDaUoPnaLIwCaAtuTwEakiwa wanaendelea na shughuli za shamba. Walipita karibu na shamba moja ambapo Lukoma aliona viatu vikuukuu vikiwa chini ya mti na kuwaambia wenzake. Walipotazama, kwa mbele, walimwona Babu akipanda mtama. Walisemezana taratibu kumcheza shere. Wakati wakifikiria, Bashiku aliwaza na kusema, “Kuna haja gani ya kumtaabisha Babu?” Badala ya kumfichia viatu, kwa nini tusimtendee tendo la huruma na ukarimu?” Wote walimwona Babu alivyoonekana kwa mbali akiwa amevaa nguo chafu na kuukuu. Walisikiliza ushauri wa Bashiku kwa makini. Waliafikiana kuchanga kiasi cha fedha ili wampe yule Babu. Baada ya kuchanga fedha, Bashiku alizichukua na kuziweka ndani ya viatu vya Babu. Ndani ya kila kiatu, aliweka kiasi fulani cha fedha. Bila mtu yeyote kuwaona, waliondoka kwa haraka kutoka eneo hilo na kujificha kwa mbali. Walitaka wajiridhishe kama Babu amechukua fedha zile kama walivyokusudia. Hawakutaka wafahamike kwa Babu. Baada ya muda mfupi, Babu alisitisha shughuli ya upanzi, akaenda kuvaa viatu ili arejee nyumbani. Alitembea taratibu hadi mahali alipoweka viatu. Alipochukua kiatu cha kwanza, alistaajabu kukutana na fedha. Alitoa machozi ya furaha huku akimshukuru Mungu. Moyoni alijisemea, “Nani mtu mwema huyu aliyejua shida yangu na kuniletea pesa?” Alijaribu kuangaza macho lakini hakuona mtu. Wakati akitafakari tukio hilo, alishika kiatu cha pili, akakutana tena na fedha. Babu hakuamini alichokiona. Alihisi kwamba anaota ndoto za mchana. Siku hiyo ilikuwa njema na iliyogubikwa na bahati kubwa. Babu hakuhisi tena uchovu. Alijisemea taratibu, “Mke wangu ni mgonjwa wa siku nyingi. Leo nimeona muujiza na maajabu makubwa. Fedha hii itatumika kumpeleka mke wangu hospitalini kwa tatizo lake la mgongo. Nyingine itatumika kununulia chakula.” FOR ONLINE USE ONLY 124 KISWAHILI_STD VII.indd 124 7/23/21 3:29 PM

P:132

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY Wale vijana walichapuka kuelekea nyumbani kwao baada ya tukio hilo. Walimshukuru Bashiku kwa ushauri mzuri. Kama wangelificha viatu, wangelimtesa Babu na kumwongezea machungu ya maisha. Ama kweli, “Dhamira safi ni tandiko laini.” Ushauri wa Bashiku ulileta manufaa na matumaini. Mkomi naye akakumbuka maneno aliyoyasikia kutoka kwa mama yake kwamba, “Siku zote wema hushinda ubaya.” Waliahidi kuwa watu wema na kuwajali wahitaji badala ya kuwacheka na kuwahangaisha. Babu alirejea nyumbani akiwa mwenye furaha na kumsimulia mkewe yaliyomtokea. Mkewe hakuamini. Siku iliyofuata, asubuhi na mapema, Babu aliandaa chai ya mkono mmoja, kisha wakanywa. Walipomaliza kunywa chai, waliandaa nguo za kuvaa, kisha wakapanda gari kuelekea hospitalini. Walipofika hospitalini, walipokelewa na muuguzi wa zamu. Muuguzi aliwaandikisha, kisha akawapeleka chumba cha tabibu. Baada ya maelezo waliyotoa kwa tabibu, walielekezwa kwenda chumba cha maabara ambapo vipimo vilichukuliwa kwa ajili ya uchunguzi. Majibu ya vipimo yalitoka, kisha matibabu yakaanza. Baada ya miezi miwili, mke wa Babu alipona kabisa, wakaruhusiwa kurejea nyumbani. Alianza kufanya shughuli za kifamilia kama kawaida. Majirani na ndugu zao walifurahi kumwona mke wa Babu amepona. 125 KISWAHILI_STD VII.indd 125 7/23/21 3:29 PM

P:133

FOR ONLINE USE ONLY Zoezi la kwanza: UfahDamOuNOT DUPLICATE 1. Taja vijana watatu wanaozungumziwa kwenye habari hii. 2. Katika Kijiji cha Mkombozi, watu walijishughulisha na nini? 3. Babu alipanda nini shambani? 4. Nani aliyewashauri vijana kumtendea Babu tendo la huruma na ukarimu? 5. Kwa nini wale vijana watatu waliamua kujificha kwenye kichaka? 6. Eleza kwa kifupi kilichotokea baada ya Babu kukuta pesa kwenye viatu vyake? 7. Babu alitumiaje fedha alizozipata? 8. Je, kwa mujibu wa habari, unafikiri Babu anamjali mkewe? Fafanua. 9. Unajifunza nini kutokana na hadithi hii? 10. Fupisha kwa aya mbili habari uliyoisoma. FOR ONLINE USE ONLYZoezi la pili: Msamiati Tunga sentensi mbili kwa kila neno. Mfano: Panya alichapuka na kuingia shimoni baada ya kumwona paka. Wanafunzi walichapuka kuelekea shuleni baada ya kumwona mwalimu wao. 1. msimu 6. mtama 2. mbegu 7. ukarimu 3. upanzi 8. sitisha 4. ahirisha 9. staajabu 5. kuukuu 10. chapuka Zoezi la 3: Nahau Tunga sentensi mbili kwa kila nahau. Mfano: Mzee Nangu aliona tahayuri baada ya adui yake kumnunulia suti. 1. ona tahayuri 2. cheza shere 3. weka mtu roho juu 4. vaa koti la mtu 5. inika kichwa 126 KISWAHILI_STD VII.indd 126 7/23/21 3:29 PM

P:134

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Zoezi la 4: Misemo Oanisha misemo ya kifungu A na maana zake katika kifungu B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi kwenye nafasi iliyoachwa wazi. Mfano: tunu na tamasha - l Na. Kifungu A Kifungu B (i) ukali wa maisha (a) arusi kubwa (b) sambamba (ii) ugomvi wa patashika nguo kuchanika FOR ONLINE USE ONLY(iii) ubavu kwa ubavu(c) baridi kali (iv) mpaka liamba (d) kushuka na kupanda kwa kiasi cha maji baharini (v) maisha ya utusitusi (e) shida, dhiki na taabu za maisha (vi) kupwa na kujaa (f) kitu kinachotegemewa sana (vii) baridi yenye mzizimo (g) ugomvi mkali (viii) hiba na atia (h) neema na zawadi kubwa (ix) arusi ya ndovu kumla mwanawe (i) umati mkubwa (x) halaiki ya watu (j) mpaka asubuhi (xi) uti wa mgongo (k) maisha yasiyokuwa na matumaini (l) zawadi na sherehe Zoezi la 5: Miundo Tunga sentensi mbili kwa kila muundo ufuatao: 1. …………… kati ya ……………. Mfano: Askari alisimama kati ya watu waliokuwa wakigombana. 2. …………..... mbele ya ……….. Mfano: Amina alitoa ushahidi mbele ya mahakama bila kusita. 3. Zamani za ………… Mfano: Zamani za kale hili eneo halikuwa na nyumba hata moja. 4. …………. ukingoni mwa ……………… Mfano: Paka aliyekuwa ukingoni mwa mto, alikamatwa na mamba. 127 KISWAHILI_STD VII.indd 127 7/23/21 3:29 PM

P:135

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYZoezi la 6: Mazoezi yaDluOghNaOT DUPLICATE A. Pigia mstari neno ambalo ni tofauti na mengine katika orodha hii. Mfano: kikombe, sahani, jagi, kitabu ndevu, mboni, kope, nyusi (i) rushwa, ufisadi, hongo, huruma (ii) hadithi, shairi, kisa, simulizi (iii) baba, shangazi, mama, watoto (iv) kicheko, furaha, huzuni, burudani (v) kihusishi, kielezi, kivumishi, utenzi (vi) chui, simba, twiga, ng’ombe (vii) kabati, kitanda, meza, pikipiki (viii) giza, mwanya, upenyo, nafasi (ix) ingawa, cheza, pika, osha (x) jezi, mechi, mchuano, pambano B. Andika wingi wa sentensi zifuatazo: Mfano: Paka amemkamata panya. Paka wamewakamata panya. Mwanafunzi amegawiwa kitabu kipya. Wanafunzi wamegawiwa vitabu vipya. (i) Mimi nimejiunga na kikundi cha uimbaji. (ii) Mwanafunzi amefunga goli la kichwa. (iii) Kijana ni fundi wa nguo ya kiume. (iv) Kitabu kimesahaulika jikoni. (v) Njiwa ni ndege mpole. (vi) Mbona simwoni mtoto? (vii) Kiongozi anapaswa kuwa mfano wa kuigwa. (viii) Ukiona kinachong’aa, ujue kimeng’arishwa. (ix) Shangazi yangu yuko dukani. (x) Paka amemkamata panya. 128 KISWAHILI_STD VII.indd 128 7/23/21 3:29 PM

P:136

FOR ONLINE USE ONLY C. Oanisha manenoDyOa fNunOgTu DAUnPa LfuICngAuTBE kwa kuandika herufi ya jibu sahihi kutoka fungu B katika nafasi iliyoachwa wazi. Mfano: benki - h Na. Fungu A Fungu B (i) moyo mweupe ..... (a) tia makali (ii) kata tamaa …… (b) kazi ya ushairi yenye beti nyingi na mistari mifupi yenye vina vya mwisho pekee, ambayo huelezea matukio ya kihistoria na ya kishujaa FOR ONLINE USE ONLY(iii) ona haya ……… (c) hali ya kutokuwa na kinyongo (iv) chukuzana ……… (d) hali ya kuwa na wasiwasi (v) kunja sura ……… (e) kosa matumaini (vi) piga tupa ….… (f) msichana mrembo (vii) kibyongo ……. (g) kasirika (viii) utendi ………….. (h) sehemu rasmi ambayo watu huweka na kutoa pesa (ix) kipusa ……….. (i) mtu aliyepinda mgongo/sehemu ya mgongo wa mtu iliyovimba na kutokeza (x) kiwewe …….. (j) fuatana (k) sikia aibu D. Tunga sentensi ishirini kwa kutumia jedwali hili. Mfano: Wanafunzi wasikivu wanawasalimia wakubwa. Watoto wema huwatii wazazi wao. Wanafunzi wema huwapokea wageni. Watoto wasikivu huwatii wazazi wao. wanawasalimia wakubwa. hawagombani njiani. watafaulu mtihani. E. Kanusha sentensi zifuatazo: Mfano: Jua liliwaka sana mchana kutwa. Jua halikuwaka sana mchana kutwa. (i) Mtima anaimba taarabu. (ii) Kuku anatembea kwa maringo. (iii) Sisi sote ni watani. 129 KISWAHILI_STD VII.indd 129 7/23/21 3:29 PM

P:137

FOR ONLINE USE ONLY (iv) Leo nimekunywDa OchaNi OkwTaDviUtaPfuLnIwCaA. TE (v) Kunguru waliruka na kupaa kama tai. (vi) Eneo letu limevamiwa na siafu. (vii) Mto umefurika tangu asubuhi. (viii) Kijana anapenda kuvaa vizuri. (ix) Nyumbani kwetu kuna aina mbalimbali za matunda. (x) Nitanunua gari la thamani kubwa. F. Andika sentensi zifuatazo katika wakati ujao. Mfano: Shangazi amefuma kitambaa maridadi. FOR ONLINE Shangazi atafuma kitambaa maridadi. USE ONLY (i) Mama anakunywa uji wa ulezi. (ii) Dada anachemsha chai ya maziwa. (iii) Mgonjwa ameruhusiwa kutoka hospitalini. (iv) Chamando hula ugali kwa mboga za majani. (v) Kilimo cha ndizi kimeinua kipato cha wananchi. (vi) Nkindi anachimba viazi vya kuchoma. (vii) Samaki ameoza kabla ya kupikwa. (viii) Wanamichezo walirudi nyumbani jioni sana. (ix) Kima walishambulia shamba la Babu Kigugu. (x) Njama ya kudhuru mifugo ya Mzee Mombe iligonga mwamba. (xi) Bomba la jikoni linavuja maji. Zoezi la 7: Utungaji Tunga habari yenye maneno yasiyozidi mia mbili (200), kisha uifupishe kwa maneno sitini hadi sabini (60 - 70). 130 KISWAHILI_STD VII.indd 130 7/23/21 3:29 PM

P:138

FOR ONLINE USE ONLY SDuOraNOyaT DKUuPmLiICnAaTSEita Uwasilishaji wa hoja Utangulizi Ulipokuwa Darasa la Sita, ulijifunza namna ya kubaini na kuchambua hoja kuu zilizotolewa katika majadiliano. Katika sura hii, utajifunza kujenga hoja, kueleza hoja na kuziwasilisha katika miktadha mbalimbali kwa kuzingatia mpangilio sahihi wa mawazo kimantiki. Baada ya kusoma sura hii, utapata ujuzi wa namna ya kuwasilisha hoja kwa mpangilio sahihi katika miktadha mbalimbali. FOR ONLINE USE ONLY Fikiri Mambo ya msingi ya kuzingatia katika ujengaji wa hoja Ufahamu Soma hadithi ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata. Mdahalo wa wanyama Katika Kijiji cha Hewani waliishi wanyama mbalimbali wa msituni. Wanyama hao waliishi maisha ya uvivu. Hawakufanya kazi. Walikuwa wanapiga domo tu. Maendeleo ya kijiji chao yalikuwa duni sana. Hali hiyo ilitokana na kukosekana kwa uongozi thabiti, kwani uongozi uliokuwapo haukuhamasisha wanyama kufanya kazi kwa bidii. Mfalme wa wanyama aliitisha mkutano kujadili hali hiyo. Katika mkutano huo, Sokwe alisema, “Tatizo la kijiji chetu kuwa na maendeleo duni linajulikana. Kwa hiyo, naomba Mfalme aitishe uchaguzi, ili tumpate Mwenyekiti ambaye tutashirikiana naye kuleta maendeleo ya kijiji.” Wanyama wote waliafiki wazo la Sokwe. 131 KISWAHILI_STD VII.indd 131 7/23/21 3:29 PM

P:139

FOR ONLINE USE ONLY Baada ya wiki moja, MfalmDeOaliNanOdaTa DshUuPghLuIlCi yAaTuEchaguzi. Aliteua Tume ya Uchaguzi ya Hewani ambayo mwenyekiti wake alikuwa Tembo na katibu wake Chui. Tume ilitangaza tarehe ya kuchukua fomu. Faru, Fisi, na Nyati walijitokeza kuchukua fomu na kuzijaza, kisha walizirejesha. Tume ya Uchaguzi ilipitia fomu zote za wagombea na kubaini kuwa wote walikuwa na sifa. Hivyo, iliwapitisha wote kugombea nafasi ya mwenyekiti wa kijiji. Tume ya Uchaguzi ilitangaza siku ya uchaguzi na ratiba ya kampeni. Wagombea wote waliruhusiwa kuanza kampeni kwa kuzingatia kanuni na sheria za uchaguzi. Kila mgombea alinadi sera zake. Siku ya uchaguzi ilipofika, wapiga kura wote walijitokeza kupiga kura. Muda wa kupiga kura ulipokwisha, Tume ya Uchaguzi ilihesabu kura kwa kushirikiana na mawakala wa wagombea. Faru alipata kura nyingi kuliko wagombea wengine. Alishinda uchaguzi huo kwa kishindo. Tembo alimtangaza Faru kuwa mshindi na mwenyekiti mteule. FOR ONLINE USE ONLY 132 KISWAHILI_STD VII.indd 132 7/23/21 3:29 PM

P:140

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLYSiku iliyofuata, Faru aliaDpOishNwaOkTuwDaUmPwLeICnyAekTitEi na kukabidhiwa ofisi ikiwa chakavu. Aliwaza sana. Alibaini kuwa hali hiyo ilisababishwa na uvivu wa wenzake. Faru alipata wazo la kuwa na mdahalo, ili wanakijiji watoe hoja ambazo zitasaidia kukikwamua kijiji katika hali ile. Baada ya wiki moja, Faru aliamua kuitisha mdahalo wa wanakijiji kujadili namna ya kuleta maendeleo katika kijiji chao. Aliandaa mada ambayo ingetolewa hoja ili kuthibitisha ukweli. Mada ilikuwa, “Kazi ina mchango katika maendeleo ya kijiji.” Alipanga siku ya mdahalo kuwa Jumanne. Hivyo, alimwagiza mtendaji wa kijiji kuwajulisha wanakijiji wote mada na siku ya mdahalo ili wajiandae. Mtendaji alifanya hivyo. Siku ilipowadia, wanakijiji wote waliwasili. Mwenyekiti wa kijiji alifungua mdahalo, kisha alimteua Pundamilia kuwa mwenyekiti wa mdahalo huo. Pundamilia alikaribishwa kusoma mada ya mdahalo mbele ya wanakijiji wenzake. Aliisoma mada hiyo kwa sauti. Baada ya kutambulishwa kwa mada, wajumbe waliruhusiwa kuanza kutoa hoja zao. Simba alikuwa wa kwanza kuchangia mada. Aliunga mkono mada iliyosomwa. Alisema, “Ni kweli kabisa kuwa kazi ina mchango mkubwa katika jamii ya kijiji chetu kwa sababu inasaidia wanakijiji kupata kipato. Hivyo, huwawezesha kuchangia maendeleo ya kijiji. Kwa hiyo, tuchape kazi ndugu zangu.” Simba alimaliza hoja yake na kukaa chini. Ilifika zamu ya Twiga kuwasilisha hoja yake. Aliiwasilisha kwa kupinga mada. Alisema, “Wanakijiji wenzangu, kazi haina mchango wowote katika maendeleo ya kijiji hiki kwa sababu maisha yetu ni mafupi mno. Hakuna haja ya kuhangaikia kazi. Kazi ni utumwa. Bora kuzurura tu.” Chui alinyoosha mkono. Mwenyekiti alimruhusu. Alimwomba Twiga athibitishe ukweli wa hoja hiyo. Twiga alishindwa kuthibitisha hoja yake. Alibaki amesimama kwa muda bila kusema chochote. Aliamua kukaa chini huku akihema kwa nguvu. Sokwe naye aliruhusiwa kuwasilisha hoja yake. Yeye alikubaliana na mada. Alisema, “Ndugu zangu, kazi ni kipimo cha utu wetu. Yeyote asiyefanya kazi hudharaulika. Maendeleo duni ya kijiji chetu yametokana na uvivu wetu. Hali hii ni hatari. Tuache uvivu. Tufanye kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo ya kijiji chetu.” 133 KISWAHILI_STD VII.indd 133 7/23/21 3:29 PM

P:141

FOR ONLINE USE ONLY Wanakijiji wengine walienDdeOleaNkOuTwaDsiUlisPhaLIhCoAjaTzEao. Katibu aliandika kila hoja. Baadaye, alisoma hoja zote upande wa walioafiki na waliopinga mada. Takwimu zilionesha kuwa walioafiki mada walishinda kwa sababu waliwasilisha hoja nyingi zilizothibitika kuliko waliopinga mada. Mwenyekiti wa mdahalo aliwaongoza wajumbe wenzake kuwapongeza washindi. Mwishowe, alimkaribisha mwenyekiti wa kijiji kuhitimisha mdahalo. Mwenyekiti wa kijiji aliwashukuru wajumbe kwa hoja zao walizoziwasilisha. Aliwataka kuzingatia kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo ya kijiji chao. Punde si punde, wanakijiji walianza kufanya kazi mbalimbali kwa bidii. Walipata kipato kikubwa na kufanikiwa kujenga ofisi nzuri ya kijiji, zahanati na shule. Walimshukuru mwenyekiti wao kwa wazo lake la kuitisha mdahalo ambao hoja zake ziliwazindua. Zoezi la kwanza: Ufahamu 1. Wanyama waliishi kijiji gani? 2. Wanyama hao waliishi maisha ya namna gani? 3. Maisha hayo ya wanakijiji yalitokana na nini? 4. Nani aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi? 5. Tume ya Uchaguzi ilikuwa na kazi gani? 6. Wagombea gani walishindwa uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji? 7. Faru alibaini kuwa uchakavu wa ofisi ya kijiji ulisababishwa na nini? 8. Kazi ina mchango gani katika maendeleo ya jamii? 9. Utafanya nini kuleta maendeleo katika jamii yako? 10. Umejifunza nini kutokana na hadithi uliyoisoma? FOR ONLINE USE ONLYZoezi la pili: Msamiati Tumia maneno uliyopewa kutunga sentensi moja kwa kila neno. Mfano: duni Maisha duni husababishwa na umaskini. 1. duni 5. kampeni 9. thibitisha 2. thabiti 6. nadi 10. teua 3. afiki 7. wakala 11. hema 4. gombea 8. kwamua 134 KISWAHILI_STD VII.indd 134 7/23/21 3:29 PM

P:142

FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE Zoezi la 3: Nahau Oanisha nahau na maana zake katika jedwali lifuatalo: Mfano: Kula chumvi nyingi - (d) kuishi miaka mingi au kuwa na umri mkubwa Na. Nahau Maana 1. kula chumvi nyingi (a) tetea au linda mtu dhidi ya jambo fulani 2. angukia pua (b) laghai, danganya au pumbaza mtu 3. chota akili (c) fanya starehe FOR ONLINE4. ingizwa mjini (d) kuishi miaka mingi au kuwa na umri mkubwa USE ONLY 5. kingia kifua (e) vaa vizuri 6. piga pamba (f) konda sana 7. mwaga sifa (g) sema mtu kwa mafumbo 8. kuwa fremu (h) pongeza au sifia mtu sana 9. pasua jipu (i) sema waziwazi tabia mbovu ya mtu 10. piga vijembe (j) shindwa vibaya 11. kula bata (k) tapeliwa Zoezi la 4: Miundo Tunga sentensi mbili tofauti kwa kila muundo. 1. Siku ya ……………………. Mfano: Siku ya mnada, mjomba alinunua ng’ombe na mbuzi. Siku ya kufunga shule, kila mwanafunzi alikabidhiwa ripoti. 2. ………………... mbele ya ……………... Mfano: Mtuhumiwa wa kesi ya wizi aliapa mbele ya hakimu kuwa hakufanya kosa hilo. Nyani walikwanyua mahindi mbele ya watu. 3. …………………... bila ……… Mfano: Mwalimu wetu alichora ramani kwenye karatasi bila kutumia penseli. Mwanafunzi alitembea bila kuvaa viatu. 4. ………………. na ……… wa ………… Mfano: Uvamizi wa kijiji ulisababishwa na ukosefu wa ulinzi shirikishi. Nzige na viwavijeshi ni wadudu waharibifu wa mazao. 135 KISWAHILI_STD VII.indd 135 7/23/21 3:29 PM

P:143

FOR ONLINE FOR ONLINE USE ONLY USE ONLY DO NOT DUPLICATE Zoezi la 5: Mazoezi ya lugha A. Panga herufi zilizochanganywa ili kuunda neno sahihi. Mfano: famlme - mfalme hajo - hoja (i) penikam (ii) gawti (iii) damhalo (iv) babusa (v) shasiliwa (vi) raishe (vii) kalawa (viii) mute (ix) jikiji (x) nduazi B. Panga sentensi zifuatazo ili zilete mtiririko sahihi. (i) Aligundua kuwa kuchapa mitihani mwenyewe kunapunguza gharama. (ii) Baada ya kuona hivyo, mwanafunzi mmoja aliamua kumwomba baba yake amnunulie kompyuta kwa ajili ya masomo yake. (iii) Aliwashawishi wanafunzi wenzake kuwaomba wazazi wao wawanunulie kompyuta ili wazitumie kutafuta maarifa wanapopewa kazi za nyumbani na walimu. (iv) Alitumia kompyuta hiyo kutafuta maarifa na kuchapia kazi zake za nyumbani. (v) Siku moja, mwalimu wetu alinunua kompyuta. (vi) Walihitimu masomo yao wakiwa na ujuzi mkubwa wa kutumia kompyuta. (vii) Alijipatia maarifa ya kutosha kwa urahisi. (viii) Aliifungua na kuiunganisha kwenye umeme. (ix) Alitufundisha namna ya kuitumia. (x) Aliamua kuchapa mitihani kwa kutumia kompyuta yake. (xi) Baba yake alikubali na kumnunulia kompyuta mpakato. (xii) Alikuja nayo darasani. (xiii) Wazazi wengi walikubali na kuwanunulia watoto wao kompyuta mpakato. 136 KISWAHILI_STD VII.indd 136 7/23/21 3:29 PM

P:144

FOR ONLINE USE ONLY C. Andika neno ambDaOlo nNiOtoTfaDutUi nPaLmICeAngTiEne katika safu za maneno yafuatayo: Mfano: mto, anga, bwawa, ziwa, bahari - anga (i) duni, maskini, hohehahe, mnyonge, tajiri____________ (ii) Kiswahili, Kiingereza, Sayansi, Kifaransa, Kichina ___________ (iii) nyati, simba, chui, twiga, ng’ombe___________ (iv) malaria, pepopunda, UKIMWI, kipindupindu, dawa __________ (v) hakimu, seremala, msusi, ufinyanzi, mchungaji___________ (vi) mgomba, mparachichi, papai, mchungwa, mkarafuu_________ (vii) kilimo, biashara, ufugaji, usafirishaji, uzururaji___________ FOR ONLINE USE ONLY(viii) mjukuu, kitukuu, kilembwe, kining’ina, kikaragosi___________ (ix) kutenda, kutendwa, kutendeana, kutendana, kulima_________ (x) msichana, banati, kigori, binti, gulamu___________   D. Andika sentensi zifuatazo katika hali timilifu. Mfano: Hakimu anaamua kesi mahakamani. Hakimu ameamua kesi mahakamani. Mwalimu alibuni zana za kufundishia wanafunzi. Mwalimu amebuni zana za kufundishia wanafunzi. (i) Watu wanaugua ugonjwa wa malaria kutokana na kuumwa na mbu jike aina ya Anofelesi. (ii) Mjomba alifanya biashara ya mtandaoni kwa muda mrefu. (iii) Ninaipenda kalamu yako inavyoandika. (iv) Rais atatoa msamaha kwa baadhi ya wafungwa nchi nzima. (v) Tulilima shamba la bibi kwa bidii. (vi) Watu waliathirika kutokana na mafuriko. (vii) Babu alisoma kitabu chote cha hadithi. (viii) Dada alipika maandazi ya kutosha siku ya mwaka mpya. (ix) Chakula kilipikwa vizuri sana. (x) Mwanafunzi wangu atakimbia upesi kuelekea nyumbani. E. Kanusha sentensi zifuatazo: Mfano: Mimi nimeunda kanuni za lugha ya Kiswahili. Mimi sijaunda kanuni za lugha ya Kiswahili. (i) Bahati atatunga hadithi kuhusu wanyama wa porini. (ii) Mkulima amevuna karanga kwa wingi shambani. (iii) Mhitimu atakunywa soda siku ya mahafali yake baada ya kupokea cheti. 137 KISWAHILI_STD VII.indd 137 7/23/21 3:29 PM

P:145

FOR ONLINE USE ONLY (iv) Baba mkubwa aDnOapeNnOdaTkDulUa PkoLroICshAoTwEakati wa jioni. (v) Mwanafunzi huyu ameanza utoro hivi karibuni. (vi) Juma atakuwa mwandishi mzuri sana wa vitabu vya hadithi za watoto. (vii) Mama hupenda kusafiri wakati wa usiku. (viii) Sisi tutafanya biashara ya kukopesha wakulima zana za kilimo. (ix) Yeye hucheza darasani wakati wa masomo. (x) Dada ananunua samaki sokoni. Zoezi la 6: Kazi ya kufanya Wasilisha hoja kwa wanafunzi wenzako darasani katika mdahalo wenye mada isemayo, “Kumsomesha mtoto wa kike ni ukombozi kwa jamii nzima.” Zoezi la 7: Utungaji Tunga habari yenye maneno yasiyozidi mia mbili (200) yenye kichwa cha habari “Elimu ndio ufunguo wa maisha.” FOR ONLINE USE ONLY 138 KISWAHILI_STD VII.indd 138 7/23/21 3:29 PM

Create a Flipbook Now
Explore more