Feb 28, 2023 03:10 UTC
  • Lionel Messi
    Lionel Messi

Gwiji wa soka wa Argentina na timu ya PSG ya Ufaransa, Lionel Messi, ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa FIFA 2022, na kuwapiku wapinzani wake wawili wa Timu ya Taifa ya Ufaransa.

Kwa ushindi huo messi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyewahi kuingia kwenye kikosi bora cha FIFA cha mwaka mara nyingi zaidi (16) akifuatiwa na Cristiano Ronaldo aliyeingia mara (15).

Messi ambaye alikuwa nahodha wa Timu ya Taifa ya Argentina, The Albiceleste katika mashindano ya Kombe la Dunia Qatar FIFA 2022, alikuwa anawania tuzo hiyo pamoja na Karim Benzema wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ufaransa na Mfaransa mwingine, Kylian Mbappe.

Pamoja na tuzo hiyo kubwa tuzo nyingine zilizotolewa jana kwenye usiku wa tuzo za FIFA (FIFA The Best) ni ya golikipa bora iliyokwenda kwa golikipa wa Argentina na Aston Villa, Emi Martinez.

Tuzo ya Kocha bora imeenda kwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Scaloni, tuzo ya kikosi bora cha mwaka (Courtois, Hakimi, Cancelo, Van Dijk, Modric, De Bruyne, Casemiro, Messi, Benzema, Haaland na Mbappe.

Kwa upande wa wanawake,  Alexia Putellas, nyota wa Uhispania wa timu ya wanawake ya Barcelona, ​​pia amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa FIFA wa Wanawake.

Wakati huo huo mchezaji kandanda wa Poland, Marcin Oleksy amekuwa mchezaji wa soka aliyepoteza mguu wa kwanza kushinda Tuzo ya FIFA ya goli bora, Puskas mwaka 2022.

Marcin Oleksy

 

Tags