Pomboo wa vita: Wanaweza kufanya nini na je wanaweza kuzilinda meli za Urusi huko Crimea?

dolphins

Chanzo cha picha, Getty Images

Mara kwa mara, vyombo vya habari vinawataja Pomboo wanaoweza kupambana, na ambao Urusi inadaiwa huwatumia kulinda Ghuba ya Sevastopol.

Mara ya mwisho majasusi wa Uingereza kuripoti kuhusu wanyama hao ilikuwa mwishoni mwa Juni. Ikitoa mfano wa picha za satelaiti, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza iliripoti kwamba Warusi wameimarisha ulinzi kwenye kambi yao huko Sevastopol na kuweka nyavu mpya na vizuizi kadhaa, na pia wameongeza mara mbili zaidi idadi ya mamali ama wanyama waliofunzwa, ambao miongoni mwao ni pomboo.

Hapo awali, hii pia iliripotiwa na Naval News.

Lakini je, pomboo wanaweza kuokoa ama kuzilinda meli za Kirusi dhidi ya mashambulizi na ni aina gani ya kazi wanazoweza kufanya? Je, Ukraine hutumia pomboo kwa madhumuni ya kijeshi? Na muhimu zaidi, je, wanyama hawa hawapati madhara kutokana shughuli kama hiyo?

Idhaa ya Kiukreni ya BBC iliuliza wataalam kuhusu haya.

Pomboo wa kijeshi

Pomboo wana rada ya asili ya kipekee - sonar, ambapo wanaweza kugundua watu na vitu vilivyopo chini ya maji kwa umbali mrefu, mtaalam wa kijeshi wa Kiukreni, nahodha wa safu ya 1 ya hifadhi ya Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine Andriy Ryzhenko alielezea BBC.

Dolphines

Chanzo cha picha, ARCHIVE OF THE UKRAINIAN CENTER "STATE OCEANARIUM"

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, uwezo huu wa asili wa Pomboo ulitumiwa kwa madhumuni mawili: kutambua wanaufanya hujuma na meli za mgodi.

Kiliundwa kitengo maalumu kinachohusisha wanyama wa baharini kwenye miaka ya 1970 huko katika Ghuba ya Cossack ya Sevastopol, anakumbuka Ryzhenko, ambaye alitumia utoto wake katika jiji hili.

"Kituo hicho kilikuwa cha siri, lakini kulikuwa na mazungumzo mengi juu yake," asema mwanajeshi huyo wa zamani.

Ilikuwa msingi wa majaribio, ambayo baadaye kikawa kituo cha utafiti "State Oceanarium", tovuti ya "Habari za jeshi la wanamaji" inaelezea kuhusu historia yake.

Hapo awali, pomboo walitumiwa tu kama kielelezo cha kutengeneza meli za haraka ambazo zinaweza kusonga mbele ama kutembea bila kelele.

Hata hivyo, Kitengo hicho katika miaka hiyo hakikufanya kazi kwa shughuli za sayansi tu, bali pia kwa masilahi ya Jeshi la Wanamaji. Hapo ndipo pomboo kadhaa waliofunzwa mafunzo maalum walikabidhiwa kwa kikosi kilichopigana na wahujumu.

Tangu 1975, kitengo cha mapigano cha mamalia wa baharini kilitumika kulinda Ghuba ya Sevastopol, wakifanya kazi karibu na eneo la Konstantinovskaya (ngome kwenye mlango wa kuingilia ghuba hiyo).

Pomboo wanafunzwa kijeshi wakiwa na silaha na kufundishwa kuua watu, ambao ni, wahujumu.

Dolphine

Chanzo cha picha, Getty Images

Mnamo mwaka wa 2013, Pomboo 10 kutoka kitengo hicho walikabidhiwa kwa meli za Kiukreni, wanyama hao walifundishwa kutafuta vitu chini ya bahari.

Baada ya uvamizi wa Ukraine wa kule Crimea mnamo 2014, kambi yao ilishikiliwa na jeshi la Urusi, na wafanyakazi wa kituo hicho walihamia Odessa, ambapo waliendelea na shughuli zao za kisayansi.

Hakuna ushahidi kwamba Ukraine sasa inatumia pomboo kwa madhumuni ya kijeshi.

Huduma kwa warusi

Tangu 2014, Urusi imeanza tena operesheni ya kitengo cha wanyama au mamalia wa baharini, wataalam na mashirika ya kijasusi ya Magharibi yanasema.

Baadhi ya pomboo hao walichukuliwa kutoka kwa hifadhi ya kiraia ya Sevastopol na kukabidhiwa kwa kikosi tofauti ili kutumika kukabiliana na vikosi na makundi ya watu wanaofanya hujuma, alisema mtaalam wa meli Pavel Lakiychuk.

Usiku, wanyama huachiliwa kutafuta wanaotajwa kuwa wahujumu kutoka Ukraine, Lakiychuk alisema.

Mnamo 2022, picha za satelaiti zilionyesha kuwa Warusi walikuwa wameweka mabwawa na pomboo kwenye mlango wa ghuba ya Sevastopol. Kisha, kwa mujibu wa Naval News, kulikuwa kunaonekana pomboo watatu au wanne kwenye ghuba hiyo.

Picha mpya zilizotolewa na shirika la ujasusi Uingereza zimeonyesha kuwa tangu wakati huo kumekuwa na pomboo wengi zaidi.

dolphins

Chanzo cha picha, BRITISH MINISTRY OF DEFENSE

Ingawa hakuna ushahidi wa utumiaji mzuri wa pomboo dhidi ya waogeleaji wa kivita, wataalam wanaona mazoezi haya kuwa ya ufanisi.

Suala jingine ni kwamba tishio kuu kwa meli za Urusi ni ndege zisizo na rubani za chini ya maji na ardhini, sio waogeleaji wahujumu, Lakiychuk alisema.

Baada ya mashambulizi kadhaa ya ndege zisizokuwa na rubani kwenye Ghuba ya Sevastopol, Warusi hawajisikii salama na wanajaribu kuimarisha ulinzi wake kwa njia zote zilizopo.

Pomboo ambao wamefunzwa kwa misheni ya mapigano ni pomboo maalum ya aina ya Black Sea dolphin.

Uhalifu dhidi ya asili

Pomboo walianza kukamatwa katika miaka ya 1960 kwa ajili ya mafunzo na majaribio, lakini wanyama walikufa haraka wakiwa mikononi mwa waliowakamata, anaelezea Rusev, ambaye alifanya kazi kwa muda katika kituo cha utafiti cha Jimbo la Oceanarium huko Odessa.

Dolphins

Chanzo cha picha, Getty Images

li dolphins kufanya kazi vizuri wakati wa mafunzo, hawajalishwa kwa muda mrefu, kama matokeo ambayo wanyama hudhoofika na kuanza kuugua.

Hadi sasa, hakuna ushahidi wa ufanisi wa dolphins za kupambana, lakini gharama za kuendeleza eneo hili na uharibifu wa asili ni kubwa sana, mwanasayansi anaamini. "Huu ni uhalifu dhidi ya maumbile," Rusev anasisitiza.

Kwa maoni yake, matumizi yoyote ya dolphins na wanadamu ni kazi isiyofaa, kwani ni mnyama adimu aliyejumuishwa katika Kitabu Nyekundu, na anapaswa kuishi baharini.

Tangu mwanzo wa vita kamili, kulingana na mahesabu ya Rusev na timu yake, karibu pomboo elfu 50 wa spishi tatu wamekufa katika Bahari Nyeusi.

Wanyama hufa kwa sababu ya mshtuko, ambayo husababishwa na mifumo ya sonar ya meli, kutoka kwa mabomu - kwanza karibu na Kisiwa cha Nyoka, na sasa - karibu na Kinburn Spit, na pia kutoka kwa migodi baharini, mwanasayansi anaelezea.